Wana wa Mungu waliwaoa binti za binadamu!

Yaleyale

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
1,789
2,383
Wasalaam wanaJf. Naomba msaada juu ya Mwanzo 6:1-4. Ukisoma hii andiko unakutana na wanadamu, wana wa Mungu na Wanafili. Biblia inasema wana wa Mungu waliwaoa binti za binadamu na wakazaa nao. Muunganiko huu ulizaa majitu makubwa sana tena hodari walioitwa Wanefili.Suali langu ni kuwa hawa wana wa Mungu ni nani hasa, ni malaika au?
Mungu alichukizwa na matendo ya binadamu na akaamua kugharikisha watu wote isipokuwa familia moja watu wanane. Cha ajabu haya majitu makubwa wanaonekana kuwepo hata baada ya gharika. Ushahidi upo Hesabu 13:31-33. Hawa wana wa Anaki waliponaje kwenye gharika?
 
Nami niliwahi kuuliza kuhusu kuendelea kuoneka kwa majitu. lakini sikujibiwa! ilikuwa kwenye jukwa hili hili. kuna uzi uliletwa na mdau. kuhusu Rockaferal family.
 
roho zao ndo bado zipo na ndizo zinazowa control binadam wengine kuhamasisha mambo ya kumwabudu shetani
 
Bwana Yesu alisema kipindi cha mwisho dunia itakuwa kama enzi za nuhu. Watu walikunwa na kula.;walioa na kuolewa. Kwakifupi haya majitu yapo hata leo japo kisiri sasa. Ndio maana unasikia kundi secret society linalo panga mikakati ya kuteka akili na hatimae roho za kila mwanadamu aliye hai leo Kwa mbinu za kuwa keep bize na mambo ya dunia na maisha ya vishawishi na hanasa kibao kila siku ilimradi akili na mioyo yao usimuwaze wala kumuelekea Mungu.
Na inasemekana wanatengeneza katika mahabara yao kisiri ile blood line ya pure nefilin ili waweze kuiintroduce ndani ya dunia yote.
Dunia si mahala salama bila kuwa na Yesu. Huwezi kujiokoa na haya majitu Kwa maana yanapigana Kwa siri (rohoni). Tunamuhitaji Yesu anaejuwa yote na anaweza yote na akajitoa ili tumpokee tuwe huru na mitego yote hapa duniani.
Bila hivyo ni kujiandaa kwa maangamizo.
 
Mkuu tafuta kitabu cha Ennoch ' The book of Ennoch. au documentary zake. kinaeleza kwa kina kuhusu hii story.
 
kwanza nianze kwa kukupongeza mleta swali hili zuri sana na majibu yake ni kama ifuatavyo:-
kwanza naomba niweke fungu lote hapa kwa ushahidi zaidi (6 Sasa ikawa kwamba hesabu ya wanadamu ilipoanza kuongezeka usoni pa nchi nao wakazaa mabinti,+ 2 ndipo wana wa Mungu wa kweli+ wakaanza kuwaona+ mabinti wa wanadamu, kwamba ni wenye sura ya kupendeza; nao wakajichukulia wake, yaani, wote waliowachagua. 3 Baada ya hapo Yehova akasema: “Roho yangu+ haitavumiliana sikuzote+ na mwanadamu kwa kuwa yeye pia ni mwili.+ Kwa hiyo siku zake zitakuwa miaka 120.”+ 4 Wanefili walikuwa duniani siku hizo, na pia baada ya hapo, wakati wana wa Mungu wa kweli walipoendelea kulala na binti za wanadamu nao wakawazalia wana, hao ndio waliokuwa watu wenye nguvu wa kale, wanaume wenye sifa. 5 Basi Yehova akaona kuwa ubaya wa mwanadamu ulikuwa mwingi duniani na kila mwelekeo+ wa fikira za moyo wake ulikuwa mbaya tu wakati wote.+ 6 Yehova akajuta+ kwamba amewafanya wanadamu duniani, naye akaumia moyoni+ mwake. 7 Kwa hiyo Yehova akasema: “Nitawafutilia mbali kutoka usoni pa nchi wanadamu ambao nimeumba,+ mwanadamu na mnyama wa kufugwa, na mnyama anayetembea na kiumbe kinachoruka cha mbinguni,+ kwa sababu ninajuta kwamba nimevifanya.”+ 8 Lakini Noa akapata kibali machoni pa Yehova.)
hao waliozungumzwa kuwa wana wakweli walikuwa ni malaika walioasi kutoka mbinguni na kuja duniani ona vifungu vya ushahidi kuhusu hilo (yuda 1:6 > 6 Na malaika ambao hawakubaki mahali pao pa kwanza bali wakayaacha makao yao wenyewe yanayofaa+ amewaweka akiba wakiwa na vifungo vya milele+ chini ya giza zito kwa ajili ya hukumu ya ile siku kuu.+)
kuhusu swali la pili kuwa hawa wanefili walionekana kwenye nchi ya kaanani majibu ya swali hili ni kuwa si kweli bali kilichokuwa kinazungumzwa zilikuwa ni ripoti za watu waliotumwa kwenda kuipeleza nchi ya kaanani sasa wakati wa kuleta ripoti hawa wapelelezi kati ya kalebu na wale wnegine walitofautiana kuwasilisha ripoti yao ambapo kalebu alisema nchi ile yafaa sana kwenda kuishi na ndiyo ilikuwa ripoti sahihi lakini hawa wapepelezi wengine wakasema kuwa nchi ile haifai kuishi kwakua kuna wanefili na haya yalikuwa maneno ya kuwaogopesha na kuwatisha waisraeli. sasa nikuombe mpendwa usome kifungu chote cha hesabu 13 utapata ukweli wa haya. soma hapa (13 Sasa Yehova akasema na Musa, na kumwambia: 2 “Tuma watu kwa ajili yako wapate kuipeleleza nchi ya Kanaani, ninayowapa wana wa Israeli.+ Mtamtuma mtu mmoja kwa ajili ya kila kabila la baba yake, kila mmoja wao mkuu+ kati yao.” 3 Basi Musa akawatuma kutoka katika nyika ya Parani+ kwa agizo la Yehova. Wanaume wote hao walikuwa vichwa vya wana wa Israeli. 4 Na haya ndiyo majina yao: Wa kabila la Rubeni, Shamua mwana wa Zakuri; 5 wa kabila la Simeoni, Shafati mwana wa Hori; 6 wa kabila la Yuda, Kalebu+ mwana wa Yefune; 7 wa kabila la Isakari, Igali mwana wa Yosefu; 8 wa kabila la Efraimu, Hoshea+ mwana wa Nuni; 9 wa kabila la Benyamini, Palti mwana wa Rafu; 10 wa kabila la Zabuloni, Gadieli mwana wa Sodi; 11 wa kabila la Yosefu,+ kwa ajili ya kabila la Manase,+ Gadi mwana wa Susi; 12 wa kabila la Dani, Amieli mwana wa Gemali; 13 wa kabila la Asheri, Sethuri mwana wa Mikaeli; 14 wa kabila la Naftali, Nabi mwana wa Vofsi; 15 wa kabila la Gadi, Geueli mwana wa Maki. 16 Hayo ndiyo majina ya wanaume ambao Musa aliwatuma wakaipeleleze nchi. Na huyo Hoshea mwana wa Nuni, Musa akamwita Yehoshua.+ 17 Musa alipokuwa akiwatuma kuipeleleza nchi ya Kanaani, aliwaambia: “Pandeni hapa na kuingia Negebu,+ nanyi mtapanda na kuingia katika eneo lenye milima.+ 18 Nanyi mtaona jinsi nchi ilivyo+ na watu wanaokaa humo, ikiwa wana nguvu au ni dhaifu, ikiwa ni wachache au ni wengi; 19 na jinsi nchi wanayokaa ndani yake ilivyo, iwapo ni nzuri au ni mbaya, na jinsi majiji wanayokaa ndani yake yalivyo, iwapo ni katika kambi au ni katika ngome; 20 Na jinsi nchi ilivyo, iwapo ni nono au imekonda,+ iwapo kuna miti ndani yake au hakuna. Nanyi mjionyeshe kuwa hodari+ na kuchukua baadhi ya matunda ya nchi hiyo.” Sasa siku hizo zilikuwa siku za matunda yaliyoiva ya kwanza ya zabibu.+ 21 Basi wakapanda na kuipeleleza nchi kutoka katika nyika ya Zini+ mpaka Rehobu+ mpaka mahali pa kuingilia pa Hamathi.+ 22 Walipopanda kuingia Negebu,+ ndipo wakafika Hebroni.+ Sasa Ahimani, Sheshai na Talmai,+ wale waliozaliwa kwa Anaki+ walikuwa huko. Hebroni+ lilikuwa limejengwa miaka saba kabla ya Soani+ la Misri. 23 Walipofika kwenye bonde la mto la Eshkoli,+ wakakata chipukizi lenye kishada kimoja cha zabibu.+ Na wawili kati ya wanaume hao wakalichukua kwa ufito, na pia baadhi ya makomamanga+ na baadhi ya tini. 24 Wakapaita mahali hapo bonde la mto la Eshkoli,+ kwa sababu ya kile kishada ambacho wana wa Israeli walikata kutoka huko. 25 Mwishowe, mwishoni mwa siku 40+ wakarudi kutoka kuipeleleza nchi. 26 Basi wakatembea na kuja kwa Musa na Haruni na kusanyiko lote la wana wa Israeli katika nyika ya Parani, huko Kadeshi.+ Nao wakaleta neno kwao na kwa kusanyiko lote na kuwaonyesha matunda ya nchi. 27 Nao wakampa habari na kusema: “Tuliingia katika nchi uliyotutuma, nayo kwa kweli inatiririka maziwa na asali,+ na haya ni matunda yake.+ 28 Hata hivyo, mambo ya hakika ni kwamba watu wanaokaa katika nchi hiyo ni wenye nguvu, na majiji yenye ngome ni makubwa sana;+ na, pia, wazao wa Anaki tuliwaona huko.+ 29 Waamaleki+ wanakaa katika nchi ya Negebu,+ na Wahiti na Wayebusi+ na Waamori+ wanakaa katika eneo lenye milima, na Wakanaani+ wanakaa kando ya bahari na kando ya ukingo wa Yordani.” 30 Ndipo Kalebu+ akajaribu kuwatuliza watu mbele ya Musa naye akasema: “Na tupande moja kwa moja, nasi tutaimiliki, kwa sababu kwa hakika tunaweza kuishinda.”+ 31 Lakini wale watu waliopanda pamoja naye wakasema: “Hatuwezi kupanda kupigana na watu hao, kwa sababu ni wenye nguvu kuliko sisi.”+ 32 Nao wakazidi kuwaletea wana wa Israeli habari mbaya+ juu ya nchi waliyokuwa wameipeleleza, na kusema: “Ile nchi, tuliyoipitia ili kuipeleleza, ni nchi ambayo inakula wakaaji wake; na watu wote tuliowaona katikati yake ni watu wenye ukubwa usio wa kawaida.+ 33 Na humo tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki,+ waliotoka kwa Wanefili; hivi kwamba sisi tukawa machoni petu wenyewe kama panzi, na machoni pao sisi tukawa vivyo hivyo.”+
 
Kiukweli nami nisomapo hiyo verse ya kitabu cha mwanzo kuhusu hayo majitu huwa napata maswali mengi.
Kikawaida kabisa walipoona duniani kuna wanawake wazuri wakaja na kuzaa nao inamaana huko mbinguni walikuwa wanaishije!? Je, waliishi na wake zao au walikuwa ni watumishi wa mwenyezi MUNGU na hawakuruhusiwa kuoa kabisa.
Walishukaje, shukaje huku ulimwenguni walikuja in form of spirit then baadaye wakaanza kuonekana physically! reaction ya wanadamu ilikuwaje baada ya kuwaona watu waajabu waliotofauti na wao kimaumbo maana wanatajwa kwamba walikuwa warefu sana na miili yao ilikuwa mikubwa pia. Hawakuwa na chimbuko lolote hapa ulimwenguni yaani Hawakuwa na wazazi, bali waliumbwa na MUNGU ili wamtumikie yy huko walipo.
Maisha ya dunia huku walipokuwa wanaishi waliyazoea tofauti na kule walipotoka, sabu mbinguni ni sehemu inayotajwa kuendelea sana kwa kila kitu na hivyo ndivyo tunavyojuzwa kwenye nyumba za ibada ss kama walikuja na kuishi huku iliwawia vigumu kukopi mazingira ya kizamani au walikuwa radhi kuishi hivyo hivyo tu ili mradi wamefanikiwa azma. Pia walipokuwa wanaishi huku duniani walikuwa na uwezo wa kwenda kuondoka kwenda mbinguni na kurudi tena ulimwenguni. Yaani nina maswali mengi!? Wataalamu nasubiri majibu yenu plz
 
kwanza nianze kwa kukupongeza mleta swali hili zuri sana na majibu yake ni kama ifuatavyo:-
kwanza naomba niweke fungu lote hapa kwa ushahidi zaidi (6 Sasa ikawa kwamba hesabu ya wanadamu ilipoanza kuongezeka usoni pa nchi nao wakazaa mabinti,+ 2 ndipo wana wa Mungu wa kweli+ wakaanza kuwaona+ mabinti wa wanadamu, kwamba ni wenye sura ya kupendeza; nao wakajichukulia wake, yaani, wote waliowachagua. 3 Baada ya hapo Yehova akasema: “Roho yangu+ haitavumiliana sikuzote+ na mwanadamu kwa kuwa yeye pia ni mwili.+ Kwa hiyo siku zake zitakuwa miaka 120.”+ 4 Wanefili walikuwa duniani siku hizo, na pia baada ya hapo, wakati wana wa Mungu wa kweli walipoendelea kulala na binti za wanadamu nao wakawazalia wana, hao ndio waliokuwa watu wenye nguvu wa kale, wanaume wenye sifa. 5 Basi Yehova akaona kuwa ubaya wa mwanadamu ulikuwa mwingi duniani na kila mwelekeo+ wa fikira za moyo wake ulikuwa mbaya tu wakati wote.+ 6 Yehova akajuta+ kwamba amewafanya wanadamu duniani, naye akaumia moyoni+ mwake. 7 Kwa hiyo Yehova akasema: “Nitawafutilia mbali kutoka usoni pa nchi wanadamu ambao nimeumba,+ mwanadamu na mnyama wa kufugwa, na mnyama anayetembea na kiumbe kinachoruka cha mbinguni,+ kwa sababu ninajuta kwamba nimevifanya.”+ 8 Lakini Noa akapata kibali machoni pa Yehova.)
hao waliozungumzwa kuwa wana wakweli walikuwa ni malaika walioasi kutoka mbinguni na kuja duniani ona vifungu vya ushahidi kuhusu hilo (yuda 1:6 > 6 Na malaika ambao hawakubaki mahali pao pa kwanza bali wakayaacha makao yao wenyewe yanayofaa+ amewaweka akiba wakiwa na vifungo vya milele+ chini ya giza zito kwa ajili ya hukumu ya ile siku kuu.+)
kuhusu swali la pili kuwa hawa wanefili walionekana kwenye nchi ya kaanani majibu ya swali hili ni kuwa si kweli bali kilichokuwa kinazungumzwa zilikuwa ni ripoti za watu waliotumwa kwenda kuipeleza nchi ya kaanani sasa wakati wa kuleta ripoti hawa wapelelezi kati ya kalebu na wale wnegine walitofautiana kuwasilisha ripoti yao ambapo kalebu alisema nchi ile yafaa sana kwenda kuishi na ndiyo ilikuwa ripoti sahihi lakini hawa wapepelezi wengine wakasema kuwa nchi ile haifai kuishi kwakua kuna wanefili na haya yalikuwa maneno ya kuwaogopesha na kuwatisha waisraeli. sasa nikuombe mpendwa usome kifungu chote cha hesabu 13 utapata ukweli wa haya. soma hapa (13 Sasa Yehova akasema na Musa, na kumwambia: 2 “Tuma watu kwa ajili yako wapate kuipeleleza nchi ya Kanaani, ninayowapa wana wa Israeli.+ Mtamtuma mtu mmoja kwa ajili ya kila kabila la baba yake, kila mmoja wao mkuu+ kati yao.” 3 Basi Musa akawatuma kutoka katika nyika ya Parani+ kwa agizo la Yehova. Wanaume wote hao walikuwa vichwa vya wana wa Israeli. 4 Na haya ndiyo majina yao: Wa kabila la Rubeni, Shamua mwana wa Zakuri; 5 wa kabila la Simeoni, Shafati mwana wa Hori; 6 wa kabila la Yuda, Kalebu+ mwana wa Yefune; 7 wa kabila la Isakari, Igali mwana wa Yosefu; 8 wa kabila la Efraimu, Hoshea+ mwana wa Nuni; 9 wa kabila la Benyamini, Palti mwana wa Rafu; 10 wa kabila la Zabuloni, Gadieli mwana wa Sodi; 11 wa kabila la Yosefu,+ kwa ajili ya kabila la Manase,+ Gadi mwana wa Susi; 12 wa kabila la Dani, Amieli mwana wa Gemali; 13 wa kabila la Asheri, Sethuri mwana wa Mikaeli; 14 wa kabila la Naftali, Nabi mwana wa Vofsi; 15 wa kabila la Gadi, Geueli mwana wa Maki. 16 Hayo ndiyo majina ya wanaume ambao Musa aliwatuma wakaipeleleze nchi. Na huyo Hoshea mwana wa Nuni, Musa akamwita Yehoshua.+ 17 Musa alipokuwa akiwatuma kuipeleleza nchi ya Kanaani, aliwaambia: “Pandeni hapa na kuingia Negebu,+ nanyi mtapanda na kuingia katika eneo lenye milima.+ 18 Nanyi mtaona jinsi nchi ilivyo+ na watu wanaokaa humo, ikiwa wana nguvu au ni dhaifu, ikiwa ni wachache au ni wengi; 19 na jinsi nchi wanayokaa ndani yake ilivyo, iwapo ni nzuri au ni mbaya, na jinsi majiji wanayokaa ndani yake yalivyo, iwapo ni katika kambi au ni katika ngome; 20 Na jinsi nchi ilivyo, iwapo ni nono au imekonda,+ iwapo kuna miti ndani yake au hakuna. Nanyi mjionyeshe kuwa hodari+ na kuchukua baadhi ya matunda ya nchi hiyo.” Sasa siku hizo zilikuwa siku za matunda yaliyoiva ya kwanza ya zabibu.+ 21 Basi wakapanda na kuipeleleza nchi kutoka katika nyika ya Zini+ mpaka Rehobu+ mpaka mahali pa kuingilia pa Hamathi.+ 22 Walipopanda kuingia Negebu,+ ndipo wakafika Hebroni.+ Sasa Ahimani, Sheshai na Talmai,+ wale waliozaliwa kwa Anaki+ walikuwa huko. Hebroni+ lilikuwa limejengwa miaka saba kabla ya Soani+ la Misri. 23 Walipofika kwenye bonde la mto la Eshkoli,+ wakakata chipukizi lenye kishada kimoja cha zabibu.+ Na wawili kati ya wanaume hao wakalichukua kwa ufito, na pia baadhi ya makomamanga+ na baadhi ya tini. 24 Wakapaita mahali hapo bonde la mto la Eshkoli,+ kwa sababu ya kile kishada ambacho wana wa Israeli walikata kutoka huko. 25 Mwishowe, mwishoni mwa siku 40+ wakarudi kutoka kuipeleleza nchi. 26 Basi wakatembea na kuja kwa Musa na Haruni na kusanyiko lote la wana wa Israeli katika nyika ya Parani, huko Kadeshi.+ Nao wakaleta neno kwao na kwa kusanyiko lote na kuwaonyesha matunda ya nchi. 27 Nao wakampa habari na kusema: “Tuliingia katika nchi uliyotutuma, nayo kwa kweli inatiririka maziwa na asali,+ na haya ni matunda yake.+ 28 Hata hivyo, mambo ya hakika ni kwamba watu wanaokaa katika nchi hiyo ni wenye nguvu, na majiji yenye ngome ni makubwa sana;+ na, pia, wazao wa Anaki tuliwaona huko.+ 29 Waamaleki+ wanakaa katika nchi ya Negebu,+ na Wahiti na Wayebusi+ na Waamori+ wanakaa katika eneo lenye milima, na Wakanaani+ wanakaa kando ya bahari na kando ya ukingo wa Yordani.” 30 Ndipo Kalebu+ akajaribu kuwatuliza watu mbele ya Musa naye akasema: “Na tupande moja kwa moja, nasi tutaimiliki, kwa sababu kwa hakika tunaweza kuishinda.”+ 31 Lakini wale watu waliopanda pamoja naye wakasema: “Hatuwezi kupanda kupigana na watu hao, kwa sababu ni wenye nguvu kuliko sisi.”+ 32 Nao wakazidi kuwaletea wana wa Israeli habari mbaya+ juu ya nchi waliyokuwa wameipeleleza, na kusema: “Ile nchi, tuliyoipitia ili kuipeleleza, ni nchi ambayo inakula wakaaji wake; na watu wote tuliowaona katikati yake ni watu wenye ukubwa usio wa kawaida.+ 33 Na humo tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki,+ waliotoka kwa Wanefili; hivi kwamba sisi tukawa machoni petu wenyewe kama panzi, na machoni pao sisi tukawa vivyo hivyo.”+
Aksante kwa majibu mzuri hasa suali la kwanza. Mpendwa naomba kutofautiana na wewe kuhusu suali la pili. Sioni kama wapelelezi 10 walikuwa na lengo la kuogopesha wana Waisraeli kwa kusema uwongo. Naamini hawa wapelelezi waliwakuta/ kuwaona wanefili walikotumwa. Kumbukumbu la Torati 3:11 inamrekodi Ogu mfalme wa Beshani kama mtu wa mwisho kwenye uzao as Wanefili. Hii inathibitisha kuwa haya majitu yaliendelea kuwepo mpaka baada ya Gharika. Hili unalizungumziaje mtumishi.
 
Suala la wapelelezi kuleta habari mbaya au la kwa mujibu "terms of reference" walizopewa tutaiwekea mada pia next time .@ Michael Chairman
 
Ndo maana Biblia inatakiwa isomomwe kama inavyotakiwa na sio kuleta mstari mmoja ili kupotosha. soma mstari wa Biblia then fuatilia unakupeleka wapi. sio kuchukua verse moja na kukimbia nayo .
 
Aksante kwa majibu mzuri hasa suali la kwanza. Mpendwa naomba kutofautiana na wewe kuhusu suali la pili. Sioni kama wapelelezi 10 walikuwa na lengo la kuogopesha wana Waisraeli kwa kusema uwongo. Naamini hawa wapelelezi waliwakuta/ kuwaona wanefili walikotumwa. Kumbukumbu la Torati 3:11 inamrekodi Ogu mfalme wa Beshani kama mtu wa mwisho kwenye uzao as Wanefili. Hii inathibitisha kuwa haya majitu yaliendelea kuwepo mpaka baada ya Gharika. Hili unalizungumziaje mtumishi.
maana ya neon wanefili ni (waangushaji) malaika waliovaa mwili wa mwanadamu tukisema kuwa hawa walibaki tutakuwa tunakinzana na biblia yenyewe mwanzo 6:3-5 ambapo hapa Mungu amesema atamwangamiza kabisa huyu mwanaadamu na kuhusu fungu ulilisoma si sahihi kuwa huyo mfalme alikuwa mnefili bali yeye alikuwa warefai hawa ni tofauti na wanefili kaka soma vizuri inasme ( 11 Kwa maana Ogu mfalme wa Bashani ndiye tu aliyebaki kati ya mabaki ya Warefaimu)
 
Hao "watu" mnaowazungumzia walikuwa malaika wa mbinguni.

Walipokuwa dunia (katika hali ya umalaika), waliwaka tamaa juu ya mabinti za dunia.

Wakajibadili na kuchukua mwili wa binadamu (ingawa walikuwa tofauti nasi kimaumbo)

Wakazaa na mabinti wa hapa duniani (ndio hao manefili).

Sasa baada ya hapo wakataka kujibadili tena kurudi kwenye hali ya umalaika. Jeshi la mbinguni likiongozwa na malaika mkuu Mikael likapigana nao vita na likawakamata na likawapeleka kuzimu.

Hao "malaika" wamefungiwa kuzimu, na wapo huko mpaka siku ya hukumu.

Kuzimu ni paala pabaya sana, na ndio maana ukiwa unatoa pepo na kumuamuru aende kuzimu, litapiga kalele sana ya kukataa kwenda huko. Mapepo yanatoa ushuhuda kuwa kuzimu kupo na watu huko wanaunguzwa vibaya mno na wamekuwa kama mkaa hivi, wana ulimi mrefuuu, ulimi unatafuta hata tone la maji lakini haupati.

Kuzimu kupo kwa asiyeamini. Lakini kama unataka kuamini Mimi naweza Ku prove.
 
Wasalaam wanaJf. Naomba msaada juu ya Mwanzo 6:1-4. Ukisoma hii andiko unakutana na wanadamu, wana wa Mungu na Wanafili. Biblia inasema wana wa Mungu waliwaoa binti za binadamu na wakazaa nao. Muunganiko huu ulizaa majitu makubwa sana tena hodari walioitwa Wanefili.Suali langu ni kuwa hawa wana wa Mungu ni nani hasa, ni malaika au?

Mungu alichukizwa na matendo ya binadamu na akaamua kugharikisha watu wote isipokuwa familia moja watu wanane. Cha ajabu haya majitu makubwa wanaonekana kuwepo hata baada ya gharika. Ushahidi upo Hesabu 13:31-33. Hawa wana wa Anaki waliponaje kwenye gharika?

Swali la Kibiblia litajibiwa kwa sehemu kubwa Kibiblia. Nitajitahidi. Neno "wana wa Mungu" katika Biblia lina maana ya watoto wa Mungu. Hao ni wale wanaomcha Mungu miongoni mwa wanadamu (Yoh 1:11-12) hata na malaika (Ayubu 1:6, 2:1; 38:7) ukitofautisha na wale malaika walioasi ama wale wanadamu waliomwasi Mungu kabisa. Hao wote wanapoteza ile heshima ya kujumuishwa katika nyumba ya Baba Mungu (Ufu 12: 7-12).

Kabla ya gharika na baada ya anguko la Adamu kilitokea kizazi ambacho kiliamua "kuliitia tena Jina la Mungu," yaani kumgeukia Mungu na kumwabudu katika kweli (Mwa 4:36). Daima Mungu hutafuta kizazi cha aina hii kila mara; ama watu wa jinsi hii kila mara panapotokea shida ya uasi kuwaokoa wengine watakaopenda kurejea kwa Mungu(Yeremia 5:1).

Kibiblia wana wa Mungu basi ni wale miongoni mwa wanadamu wanaomcha Mungu. Hao hawakuruhusiwa kuoa nje ya wenzao walio "wana wa Mungu" yaani wachaji Mungu pia. Hili pia lilikuwa katazo kwa Israeli wasioe miongoni mwa wageni ama makabila yaliyopo Kanaani (Kumb 7:1-5). Hilo likifanyika linaleta hasira ya Mungu kama iliyotokea kwa Sulemani alipooa wanawake wa Kanaani (I Fal 11:1-13). Mungu alimwondosha katika Ufalme na akafutika kwa kiasi fulani.

Kwa maana hiyo inakuja laana, yaani kukosekana kwa Baraka ya Mungu. Basi chochote chaweza kutokea kama matokeo ya anguko hilo. Uzao unaweza kuharibika, vizazi vinavyokuja vikafikiwa na matokeo ya matendo maovu ya babu zao. Ndivyo ilivyokuwa katika Mwa 6. Wasomi wa Biblia wanasema hao wana wa Mungu ni ule uzao wa Sethi ulioamua kumgeukia Mungu. Waliendelea vizuri lakini wakaja kuharibika na kujitwalia wake miongoni mwa jamii isiyomcha Mungu (Mwa 6:1-4). Hao Wanefili (majitu) ni mbegu mbaya iliyotokana na mchanganyiko huo. Mungu aliumba mwanadamu kamili maana uumbaji wake wote ulikuwa mwema (Mwa 1:1-31). Hivyo wacha Mungu wakawaoa wasio wacha Mungu na kuzaa nao. Malaika hawezi kuoa na kuzaa Yesu anatuambia (Luka 20: 29-36)

\v 29 Basi, kulikuwa na ndugu saba. Wa kwanza alioa mke, akafa hana mtoto; \v 30 na wa pili [akamtwaa yule mke, akafa hana mtoto;] \v 31 hata wa tatu akamwoa, na kadhalika wote saba, wakafa, wasiache watoto. \v 32 Mwisho akafa yule mke naye. \v 33 Basi, katika ufufuo atakuwa mke wa yupi? Maana aliolewa na wote saba. \v 34 Yesu akawaambia, Wana wa ulimwengu huu huoa na kuolewa; \v 35 lakini, wale wahesabiwao kuwa wamestahili kuupata ulimwengu ule, na kule kufufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi; \v 36 * wala hawawezi kufa tena; kwa sababu huwa sawasawa na malaika, nao ni wana wa Mungu, kwa vile walivyo wana wa ufufuo.

Malaika watakatifu ama wale waasi (mashetani) hawana miili kama ya kwetu. Wana miili ya roho naweza kusema – miili ya roho iliyotukuka (Malaika watakatifu) na miili ya roho iliyolaaniwa (mashetani). Paulo anafafanua sana juu ya tofauti ya hii miili. Anaita mwili wa asili na mwili wa roho (1 Kor 15: 35-49). Hivyo, ndoa ni ya hapa duniani. Wawili watakuwa mwili mmoja. Basi malaika haoi wala haolewi.

Kwa hiyo wanaohusika na Mwanzo 6 ni wanadamu tu – wachaji wa Mungu na wale wasiomcha Mungu kuoana na hatimaye mbegu tofauti kutokea.

Sasa kwa mtazamo wa kibiblia uharibifu ukiisha ingia ulimwenguni huendelea kuwepo mpaka mwisho wa mambo yote (2 Pet 1: 1-4). Kwa mfano mauti iliingia nayo bado ipo, ila kuna ahadi ya ufufuo wa baadaye (Yoh 6:39-40). Magonjwa bado yapo (ila uponyaji wa Mungu nao upo - Marko 16:15-20). Umaskini bado upo ila mtu akifanya kazi kwa bidii ataondokana nao (Mith 6: 6 -11). Ilibidi Israeli wakae Misri miaka mia nne mpaka pale uovu wa Waamori utakapotimia (Mwa 15:13 -16). Ndio maana hata Shetani yupo vile vile akiendeleza uovu wake mpaka wakati wake utimie. Wana theolojia na wanafalsafa wa dini wanajadiliana sana juu ya hili. Kwa nini Biblia inasema Shetani anao muda mchache (Ufu 12: 1 -9). Yesu naye alikuja pale utimilifu wa wakati uliomhusu ulipotimia (Gal 4:4). Tunajiuliza kwa nini Yesu alisema usiwatoe ulimwenguni bali uwalinde na yule mwovu (Yoh 17:15). Majitu hayo, na wote watendao mabaya, ma-Anti Kristo na wengineo wataendelea kuwepo hadi wakati husika ulioamriwa. Cha msingi hawana uwezo wa kuyadhuru maisha ya yule aaminiye ambaye daima hulindwa na nguvu za Mungu.

Mkumbuke Daudi alimuua Goliath. Hao wana wa Anaki, hawakuwazuia israeli kusafiri kuelekea Kanaani. Uharibifu huo ni pamoja na ule wa watu wafupi sana yaani mbilikimo. Hawa nao tusemeje. Namfahamu mhubiri ambaye ni mlemavu kabisa na anawaombea walemavu wapone yeye yupo hapo hapo. Paulo alikuwa na shida katika mwili wake ikimtatiza. Aliomba Mungu itoke, na Mungu akamwambia endelea na udhaifu huo maana hapo ndipo penye nguvu na uweza wangu (1 Kor 12:7 - 10)
 
Back
Top Bottom