The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 5,464
- 17,293
Historia ya biblia inasema Mungu alimpa Musa amri zake 10 kuu, kati ya amri hizo iko amri ya 6 ya usiue.
Hii amri Mungu aliwakataza binadamu kuua ama kukatisha uhai wa binadamu wenzao.
Cha kujiuliza na kushangaza, Mungu huyo huyo akaamuru wana wa Israel kuua watu wa mataifa mengine kama walipokua njiani kuelekea kaanani.
Mungu aliamua waue wanaume wote wanaokutana nao na kisha kuchukua wanawake zao na kuwafanya wake zao, kwa maana nyingine kuwabaka na mwanamke ambae angekataa kubakwa Mungu aliagiza auwawe bila huruma.
Kwa amri ama maagizo hayo ya Mungu wana wa Israel walifanya ubakaji na mauaji ya kutisha kwa jina la Mungu wao.
Swali, kama Mungu alikataza binadamu kuua ama kukatisha uhai wa binadamu mwenzake, kisha mungu huyo huyo akaagiza binadamu wale aliowakataza kuua, na kuwapa amri ya kuua, je amri yake hii ya pili haipingani na amri yake ya kwanza ya usiue na hivyo yeye mwenyewe kujikanganya?
Ama mungu alipotoa maagizo ya kuua alikua kasahau kwamba alishatoa maagizo mengine ya kutokuua huko nyuma?
Je huku ni kujichanganya kwa Mungu ama Mungu hakua na kumbukumbu ya alichokisema hapo awali?