Asante sana kwa kutuwekea mada mahsusi kwa ustawi wa mkoa wetu pendwa-Kagera. Naomba nichangie hapa:
Kuna tatifi mbalimbali zilikwisha fanyika kuhusiana na tatizo hili. Fuatilia hapa: Reduced cost of tissue culture banana can help control spread of Banana Bacterial Wilt in Great Lakes region na Farmer Capacity Building in Tissue Culture Banana Cultivation labda walakini uko katika uwezo wa mtu wa Morogoro kumfundisha mzaliwa wa Dar es Salaam kuogelea Baharini!
Niwazo zuri sana ambalo hata mimi nililiwaza siku nyingi na nikaanzisha group humu JF ila emyaga ekakanya nikashindwa kuliweka active!Kagera development - JamiiForums | The Home of Great Thinkers Nilitamani kitu kama hicho sasa naona tunaweza kuanzia hapo!!Ndugu,
bakuza, Bigaraone, Chaimaharage, evoddy, Gagnija, Hagga, Jaji, james chapacha, Kagalala, Kaitampunu, kanyagio, Kibera, Lonestriker, Mkomamanga, MPIGA ZEZE, MUGUNDA, naivasha, Ngeleshi, PrN-kazi, Qixima mQiqa, RUBERTS, Rwamarungu, Rweza, sangija, Seneta,mukama talemwa,Speedy, timbilimu, Tukundane, Yakuza,rugumisa,GALIMA,BigTime,Kakalende,PrN-kazi, Alexism+, kilikiliani,kanyagio,BUSHAIJABWE, Libaba, Smarty, Baba Collins,Eddy M, BUBE, Tata, KASHOROBANA na wengine nyote mnaoipendea mema na maendeleo Kagera
Hapo chini ni mabadiliko yanayoendelea kutokea nchini. Yameninyong'onyesha na kunifedhehesha sana nilipojaribu kulinganisha Shinyanga na Kagera.
Nawaomba mje hapa tufanye mjadala mpana utakaoishia katika maamuzi na kuchukuliwa hatua kivitendo juu ya nini kifanyike toka sasa mpaka 2015 ili nasi walau tuweze kuwemo kwenye basi la Mabadiliko na Ukombozi wa Tanganyika
Omutwale tukuwe olabasa?
.
WATU WENYE NJAA SIO RAHISI KUCHAGUA UPINZANI, WATADAGANYIKA KIRAHISI KWA WALI NA KOFIA. TATIZO LILILO LA MSINGI NI UCHUMI WA KAGERA ULIODUMAA.
KUNAWEZA KUWAPO SBB NYINGI ZA KUENDELEA KUSHUKA KWA UCHUMI KATIKA ENEO HILO (mnawazidi DODOMA na SINGIDA TU) .Mimi naona Uvivu uliokithiri na kutojituma ndio sababu kubwa.Hakuna chakula,migomba haikubali (awali mlizoea kutifua udongo kidogo tu na kuisimika aridhini, JEMBE HAMJUI KUSHIKA, MNANYOFOA MAGUGU SHAMBANI MKIWA MMEKAA,KUSOGEA HATUA NYINGINE MNAJIVUTA).
Wakati wa kulima mahindi na mtama kama zao la chakula umefika. jifunzeni kukamata jembe au mnasubiri matrekta ya kilimo kwanza? Kahawa haina soko tena( mikahawa yenyewe ilikuwa kama miti ya miembe,haifanyiwi chochote mnasubiria msimu tu.Na hakukuwa na jitihada ya kupanda mipya) samaki wanapelekwa nje tu.Kuna wakati nilisikia vanila inakubali sana huko, ila kwa kuwa inahitaji sana matunzo watu wavivu mkashindwa.
Mtu mvivu sio rahisi kupenda au kukubali mabadiliko na hatimaye akawa na mawazo ya kukabili changamoto mpya kama kuhama au kuchagua chama kingine cha siasa, anaona uvivu. mnapenda sana kula bata ndugu.hampendi kazi ngumu.komaeni,pigeni kazi, enzi za ulangila kwishinei.Wavivu kiasi kwamba hadi mambo yenu yaleeeeee ya SHULE yanawashinda siku hizi.
Chadema walituangusha kutosimamia na kuangalia mtu ambae anagombea ubunge anamtazamo gani,wakachukua dj wakamsimamisha agombee ubunge uko nkenge mwisho wa kampeni akaondoa jina akamuachia nafasi Mushamu atambe nkenge peke yake,ila yote ii ni kwasababu tulimpoteza mtu ambae alikuwa mpiganaji Julius Ndyanabo Mungu amuweke pema,viongozi wa chadema geukia uko ISHOZI,ISHUNJU,GERA,BWANJA,KANYIGO,BUYANGO,BUGANDIKA,KYAKA,BUNAZI,KAKUNYU,MUTUKULA,NK