Mtumishi Wetu
JF-Expert Member
- Oct 12, 2010
- 5,712
- 1,906
Ni kweli mkuu umeeleweka vizuri maendeleo ya Kagera si lazima wawe Wahaya peke yao kuchangia hata watu wenye interest hasa vested interest wanaweza kuchangia!!! Kuhusu lugha hata mimi nilijisahau familia yangu ni kubwa na si wote wanaongea kihaya, from my wife my kids and others, ahsante kwa kutufungua. Ubarikiwe!!!Mkuu huu uzi ni mzuri ila ujue ubinafsi ndo uliotuponza tukafika hapa tulipo.
Naomba huu uzi tutumie lugha ambazo wengi wanazifahamu yaani kiswahili na kiingereza.
Naamini kuna wengi ambao sio Wahaya ambao wanaupenda mkoa wa Kagera sasa tukiendelea kutumia kihaya ndo tutazidi kuwatenga. Tanzania ni yetu sote na tuna wajibu wa kuijenga kwa kushirikiana
Naamini hata hao wa Shinyanga sio wote waliosaidia mabadiliko ni wenyeji wa huko. Mfano mimi ni Mhaya lakini naishi Mtwara, naamini wale makabila mengine ambayo watu wake wanafanya kazi zao huko kagera wanaweza kuwa na michango yenye afya zaidi kuliko watu kama sisi tulio mbali.
Kitu ambacho huwa kinatuponza sie wa kagera ni ujuaji na umimi. Tukirekebisha hayo, naamini tutapiga hatua haraka