Wana jf naombeni ushauri please!!

KANCHI

JF-Expert Member
Sep 3, 2011
1,533
230
Nimepata kazi katika chuo kikuu kimoja kama tutorial assistant na pia bado nasubiria ajira za serikali (ualimu) naona zipo karibu pia.Sasa nipo njia panda niende kupiga mzigo katika Chuo hichi au nisubirie za serikali nadhani mnafahamu faida za kuwa serikalini.

Ahsanteni sana!
 
Ngoja ngoja yaumiza matumbo alafu mambo hayakawii kubadilika mkuu.
Nenda kapigishe pindi katika hiko chuo, huko Serikali patajulikana mbele kwa mbele.
 
kapige mzigo wa T.A mkuu ,kazi za JK saiv hazina maslahi utasubiria hlf utaishia kufa njaa.....stuka acha kuremba.
 
Nenda hiyo ya T.A kwanza ujijenge upate experience. Serikali will come baadae
 
Angalia maslahi Kaka!!
Nenda kaanza maisha huko wakati unapata experience then later on utajiunga na serikali!!
Na advantage ya chuo pia wanaweza wakakusomesha ndo huwaga program zao hizo!!
KAPIGE KAZI KAKA!!
 
Kama nitakuwa nimekosea utaniwia radhi mkuu, umesema umepata kazi katika chuo kikuu kimoja kama T.A, lakini wakati huo huo unasubiri kazi ya Ualimu toka serikalini, napata wakati mgumu kidogo kutokana na maelezo yako kwa sababu moja kuu, serikali huwa haiwapangii kazi walimu kwenda kufundisha vyuo vikuu labda kama utaratibu umebadilika ama ni kutokujua kwangu ila nijuacho mimi serikali huwapanga walimu wa sekondari na sitaki kuamini kwamba Ajira ya serikali unayoisubiri ni kwenda kufundisha A-Level.

Other things remain constant, ulicho nacho mkononi ndio chako.................. nenda kafanye kazi zikitoka hizo za serikalini utaangalia ulikopangiwa na mkataba wa hapo ulipo ukoje then itakuwa rahisi kufanya maamuzi.
 
Back
Top Bottom