Tupeane ushauri katika hili: Je, niendelee kujiajiri au niajiriwe?

Kazanazo

JF-Expert Member
Aug 16, 2023
686
1,360
Habari za muda huu wanajamii...

Natumaini humu kuna watu mbalimbali wenye uzoefu katika masuala ya biashara na pia kuna waajiriwa wa serikalini na sekta binafsi au vyote kwa pamoja(waajiriwa ila ni wafanya biashara pia).

Iko hivi, nilimaliza elimu ya juu miaka mitatu iliyopita katika kitivo cha elimu lakini nikiwa chuo niliweza kujishughulisha na vibiashara mbalimbali na nikabahatika kushika kibiashara kimoja nikaganda nacho nikitumia pesa za kujikimu(BOOM) kama mtaji.

Nilipomaliza masomo sikuhangaika kutafuta shule za kujishikiza kufundisha ila niliendeleza kibiashara changu ambacho hadi sasa nashukuru Mungu bili zote nalipa bila wasiwasi.

Sasa mkanganyiko unakuja kwamba kuna baadhi ya ndugu na jamaa wananipambania nipate ajira ya kudumu hivyo kunipa connection mbalimbali ila najikuta sizitilii maanani kwa kuwa nishazoea biashara na ninaona mwanga mzuri mbele kwenye biashara yangu.

Kwa wazoefu wa haya mambo naombeni ushauri nifanyeje ili baadae yasije nikuta majuto kwanini sikufata upandee huu huenda ningetoboa au kwanini niliacha hiki asaivi niko ivi, naombeni ushauri wenu.

Natanguliza shukran.
 
Biashara kitu kipana na Ajira kitu kipana wewe umeeleza in general Sana.

Kwanza ungeeleza Biashara unayofanya ni ipi, faida unapata kihasi gani, growth yake ipoje??

Umesomea Nini, hizo Ajira ni zipi, mshahara wake na future yake ipoje??
Nimefupisha uzi usiwe mrefu sana ila najishughulisha na kuuza vifaa vya simu na katika elimu nimesomea Bachelor of arts with education
 
Habari za muda huu wanajamii...

Natumaini humu kuna watu mbalimbali wenye uzoefu katika masuala ya biashara na pia kuna waajiriwa wa serikalini na sekta binafsi au vyote kwa pamoja(waajiriwa ila ni wafanya biashara pia).

Iko hivi, nilimaliza elimu ya juu miaka mitatu iliyopita katika kitivo cha elimu lakini nikiwa chuo niliweza kujishughulisha na vibiashara mbalimbali na nikabahatika kushika kibiashara kimoja nikaganda nacho nikitumia pesa za kujikimu(BOOM) kama mtaji.

Nilipomaliza masomo sikuhangaika kutafuta shule za kujishikiza kufundisha ila niliendeleza kibiashara changu ambacho hadi sasa nashukuru Mungu bili zote nalipa bila wasiwasi.

Sasa mkanganyiko unakuja kwamba kuna baadhi ya ndugu na jamaa wananipambania nipate ajira ya kudumu hivyo kunipa connection mbalimbali ila najikuta sizitilii maanani kwa kuwa nishazoea biashara na ninaona mwanga mzuri mbele kwenye biashara yangu.

Kwa wazoefu wa haya mambo naombeni ushauri nifanyeje ili baadae yasije nikuta majuto kwanini sikufata upandee huu huenda ningetoboa au kwanini niliacha hiki asaivi niko ivi, naombeni ushauri wenu.

Natanguliza shukran.
Nimekuelewa sana dogo,Iko hivi kwa kuwa umeanza biashara na umekuwa mzoefu,fanya biashara kwa ufanisi mkubwa sana kama miongozo ya biashara inavyotaka.Maana ajira mwisho wake utastaafu na utarudi uraiani.Lakini kama huna uhakika na biashara Yako ajiriwa ila mwisho wa siku utastaafu.Hayo ndio maoni yangu,maana niliajiriwa baadhibya jamaa zangu walikataa ajira kwa Sasa ni watu wenye fedha balaa!
 
Kuajiriwa ni vizuri, Lakini kujiajiri mwenyewe ni vizuri zaidi. Ongeza juhudi, maarifa na bidii. Upo pazuri vizuri na unaelekea pazuri zaidi....
Mwenyezi Mungu abariki nia, juhudi na mipango yako
 
Nimekuelewa sana dogo,Iko hivi kwa kuwa umeanza biashara na umekuwa mzoefu,fanya biashara kwa ufanisi mkubwa sana kama miongozo ya biashara inavyotaka.Maana ajira mwisho wake utastaafu na utarudi uraiani.Lakini kama huna uhakika na biashara Yako ajiriwa ila mwisho wa siku utastaafu.Hayo ndio maoni yangu,maana niliajiriwa baadhibya jamaa zangu walikataa ajira kwa Sasa ni watu wenye fedha balaa!
Kuhusu uhakika wa biashara siwezi kujua kwa sasa mkuu japo napambana na naona mwanga kwa mbali

Kinachonifanya niombe ushauri ni kwa kuwa nipo 50/50 na wahenga wanasema majuto ni mjukuu nisije kujuta baadae kwanini nilikataa ajira
 
Hakuna kujuta mkuu, biashara ni muhimu pia fuata kule moyo wako unakusukuma.Maana hazina Yako ilipo ndipo na moyo wako ulipo!
 
Kama unahela kunzidi abood wa abood bus usiajiriwe. Kama unahela sawa na abood au pungufu kidogo kaajiriwe Kwa sababu abood ameajiriwa na bunge la Tanzania baada ya kufanyiwa usaili na wananchi wa morogoro mjini.

Bunge humlipa 11,600,500.50 Kwa mwezi na kamuni ya abood bus huingiza faida ya 12,300,400.29 Kwa siku.

Je, wewe unapata faida ya 771,000 Kwa mwezi?
 
Back
Top Bottom