Wana JF naombeni MNIFUNDE

Nazjaz

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
7,684
8,833
Nina ujauzito wa miezi saba na nusu sasa.
Leo nikiwa saluni kutengeneza nywele , kuna dada kaja na mpya ananiambia eti kitovu ni hatari sana.
Kikiwa kinakatikia kikimdondokea mtoto anaweza kuwa tasa na kama mtoto wa kiume anakuwa *******.
Pia nimeambiwa eti mama mkwe wangu asikione kabisa sehemu nitakakokifukia.
Kwa bahati mbaya sana yule dada akaondoka akiwa hajamaliza kunipa shule.
Ndugu zangu wana JF naombeni mnifunde.
 
Kuna maelezo ya kisayansi kuthibitisha hayo au ni mambo ya superstitions tu?
 
Hakuna ukweli kisayansi.

achana na Imani hizo

Lea mimba yako na uzae ukiwa na amani
 
Usiogope sana story za kutengenezwa tengenezwa bila scientific support.
 
Nazjaz, unataka kumfanyia mwanao majaribio????

Kama unataka uwe sampo, anza kukaa mlangoni hadi siku ya kujifungua ndio utajua wahenga wana la maana ama lah.

Wazungu kukosa evidence haimaanishi kitu hakipo.

Kwa maelezo zaidi nenda jukwaa la dokta hii mada imejadiliwa kwa kirefu.

Natumia mchina siwezi weka link hapa.
 
Last edited by a moderator:
Kongosho, ukikaa mlangoni utakumbwa na nini?
Hakika nina mengi sana ya kujifunza, naomba msaada wenu wapendwa
Nazjaz, unataka kumfanyia mwanao majaribio????

Kama unataka uwe sampo, anza kukaa mlangoni hadi siku ya kujifungua ndio utajua wahenga wana la maana ama lah.

Wazungu kukosa evidence haimaanishi kitu hakipo.

Kwa maelezo zaidi nenda jukwaa la dokta hii mada imejadiliwa kwa kirefu.

Natumia mchina siwezi weka link hapa.
 
Last edited by a moderator:
Dada yangu angalia hao wapita njia wasikudanganye ukaingia mahali ambapo sio. Mwisho watakwambia ukifikia wakati wa kujifungua nenda kwa mganga wa kienyeji ukajifungulie huko. Peleka IMANI yako kwa Mungu.
 
Sangari wanawake wengi wanakuwa na hofu sana wakikaribia kujifungua, hasa mtoto wa kwanza.
Tatizo ni kwamba wakati nchi nyingine uzazi ni neema, huku kwetu uzazi ni nusu ya kifo

mimi nilikuwa nafikiri Nasjaz ni mmoja wa 'makungwi' hapa jf..
ametoka Tanga na si mtoto mdogo ....

kumbe bado still unahitaji kufundwa pia?

kuna member anaitwa Shosti hapa jf

muulize zaidi....yeye ni kungwi pia lol
 
jifanyie majaribio, utapata jibu zuri bila changa.

oh no way.mi huwa naogopa sana kujifanyia experiment. eti nilisikia pia kuwa hata mtu akifunga upande wa khanga yake mjamzito hajifungui je ni kweli? na pia wanasema eti si vizur kuwatajia watu tarehe ya kujifungua?
 
Sangari wanawake wengi wanakuwa na hofu sana wakikaribia kujifungua, hasa mtoto wa kwanza.
Tatizo ni kwamba wakati nchi nyingine uzazi ni neema, huku kwetu uzazi ni nusu ya kifo

Ni kweli kabisa ndugu yangu..
Yaani mtu wako akiwa na mimba roho mkononi...
 
Back
Top Bottom