wee una mtakia nini lakini?
akhu!
Mwalimu Kichuguu mzima jamani...
.... Mkjj, natumaini huko aliko yu salama; ila inatia wasiwasi, Mwl.Kichuguu kapotea kweli kweli...(isije ikawa nguchiro na michwa wamesiriba matundu yote na kufia humo humo ndani na kichuguu kuishia kudumaa kisirefuke tena.... lol )
..... Msanii naye katowekea wapi tena?! Baada ya harusi yake alijitokeza mara kadhaa, ghafla huyoooo.... sijui majukumu katika ndoa.... i don't know, but i hope yu mzima kokote alipo..
sijamuona FD muda mrefu kidogo..........sijui naye kapotelea wapi
FD kwema lakini huko uliko?
Unajua kunakuwa na baadhi ya wanachama humu ndani lazima usikie kasema kitu kila siku, sasa akipotea ghafla, unaanza kujiuliza, kapotelea wapi, nini kilichomsibu? Ndio hayo ya mkuu Game Theory......Sijamsikia siku kadhaa humu ndani, au ndo mambo ya kubadilisha majina?
MKUU GAME THEORY....Nani kati ya hawa aliyekupiga marufuku tena??? Ili tukuombee ruhusa?
1) Mama watoto (Shemeji mkubwa).
2) Nyumba ndogo (Binti Maringo).
3) Bosi (Unazembea mzigoni).
4) Admin (Unabishana sana)
5) Name change (Uzime mabifu na watu).