Wamiliki wa mabasi fursa mmetengenezewa hiyo hapo chukueni hela

Hawa jamaa wanaanzisha kodi za ajabu ajabu kila kukicha sijui kwa sababu ya uwezo wao wa kufikiri au roho mbaya tuu sipati jibu unawezaje kuwaongezea gharama watu wapo kwenye mpito wa Covid 19 mitaji imepukutika mno watu wanalinda afya badala ya kuwapa hauweni ninyi ndio mnakuja kuwaua tena...Mungu awasamehe kwa kweli ila hii itabaki kwenye kumbukumbu kwa vizazi vijavyo kwa yaliyowahi kujiri Tanzania..
 
Hiyo mbinu nayo inakaugumu kake. Kutokana na wizi na ujambazi uliokuwa umekithiri kwa maboat ya abilia goziba walianza kutumia mbinu hii miaka mingi tu. Ili mtu asisafiri na pesa ila tatizo linakuja kuwa kuna mazingira ambayo yanapokea pesa ila hayatoi na kuna mazingira yanatoa sana pesa kuliko kupokea. Endapo hiyo kampuni itafanya hivyo kuna muda itabidi yenyewe itumie tena miamala ambayo imewakwepesha nyinyi.

Mfano
Watu wengi hutuma sana pesa kutoka dar kwenda mkoani ila hawatumi kutoka mikoani kuja dar. Hivyo ofisi za kampuni za mikoani zitagawa zile pesa mpaka zinaishiwa huku ofisi ya dar ya kampuni ikiwa imejaza magunia ya noti ndani. Hivyo kampuni itahitaji kusafirisha tena hizo noti ama itumie miamara ya kibenk ama miamala ambayo imewakwepesha nyinyi. Kwakifupi huo mchakato unaharufu ya kufirisi mtu

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Umeleta wazo zuri mkuu ila hili naona linahitaji kuanzisha system mpya ..kitu ambacho kitachukua muda kuanza kutoa huduma ya uhakika maskini tutakuwa tushaumizwa sana na haya makato..

WAZO LANGU: bado kuna mwanya kwa mawakala kuokoa hii system kandamizi. Nijuavyo mimi wakala kutuma pesa kwa wakala mwenzie hakuna makato hivyo basi anaetuma pesa aende kwa wakala na anaepokea pesa nae aende kwa wakala aliepo karibu nae kisha hawa mawakala watumiane pesa wao kwa wao .
Kisha wakala alietumiwa anatoa cash kwa yule aliekuwa anatumiwa hizo pesa na kwakua hakuna makato yoyote basi hawa mawakala watachaji makato yao kwa cash pale pale. Kwa kufanya hivi wakala atakuwa ameokoa biashara yake na wateja wataokoa pesa zao zinazokwenda na haya makato mapya.
Kumbe huwajui wa mitandao,ukituma mbali Sana wanakukata kuwa umefanya fraud labda ishu wachonge zile za lipa hapa kwa namba Fulani Kama mpesa.
Huwezi unamtumia wakala uko dar afu ukamtumia aliyeko mbeya hata wale wa line ya wakala kubwa inakatazwa.
Sema pia na benki inabidi watoe SoMo kuwa naweza nikakutumia hela ukapewa na Kodi afu ukaenda kwa atm ya karibu unachukua hela.
Kumbuka makato ya atm yalikuwaga ni 900 wanasiasa wakaongeza za kwao zikawa 1200.
Yaani Hawa jamaa eti tunawachagua wenyewe afu eti tunawaogopa.
Mzee mangula alisema haya maneno
 
Hiyo mbinu nayo inakaugumu kake. Kutokana na wizi na ujambazi uliokuwa umekithiri kwa maboat ya abilia goziba walianza kutumia mbinu hii miaka mingi tu. Ili mtu asisafiri na pesa ila tatizo linakuja kuwa kuna mazingira ambayo yanapokea pesa ila hayatoi na kuna mazingira yanatoa sana pesa kuliko kupokea. Endapo hiyo kampuni itafanya hivyo kuna muda itabidi yenyewe itumie tena miamala ambayo imewakwepesha nyinyi.

Mfano
Watu wengi hutuma sana pesa kutoka dar kwenda mkoani ila hawatumi kutoka mikoani kuja dar. Hivyo ofisi za kampuni za mikoani zitagawa zile pesa mpaka zinaishiwa huku ofisi ya dar ya kampuni ikiwa imejaza magunia ya noti ndani. Hivyo kampuni itahitaji kusafirisha tena hizo noti ama itumie miamara ya kibenk ama miamala ambayo imewakwepesha nyinyi. Kwakifupi huo mchakato unaharufu ya kufirisi mtu

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
Usiogope si zikijaa wanawatumia hao wa mkoani afu wanachukulia benki huko huko mkoani.
Yaani mie naenda kwa ofisi kuwa bana wape pesa hapo afu mie nipo hapa ofisini napewa.
Akimpa tu simu inapigwa napewa.
So Ina Mana nikimwambia jamaa mwenye duka pale home kwetu kuwa Mpe maza kilo hapo afu mie nakuwekea benki kwa akaunti yako so atakamatwaje ama wataanza kuwafuatilia wananchi wanaongea Nini.
 
Acha kukaza fuvu ilo....

Shotly anamaanisha wamiliki wa mabus ya mkoa waanze kutoa huduma ya miamala. Mf. Wewe unakwenda pale Shekilango kwa Kilimanjaro express unawapa laki 1 huku babe wako anaenda Kilimanjaro express Arusha kuchukua hizo pesa.
Hii idea ni kama niliyoipendekeza kwenye uzi mmoja hapo awali.

Sio lazima iwe Kampuni ya Basi, hata hao Watoa huduma wanaweza kuunda umoja wao Mikoa yote na Vitongoji kama ilivyo hao kina Airtel, Voda, Tigo n.k.

Na ndani ya muda mfupi tayari Jamii watakua wametambua Kampuni ya/za kuziamini na pesa zao...hivyo Mtu akikuwekea pesa kwa Wakala hapo Dar, Wakala Mshirika aliyepo Arusha atahakikisha Muhusika anapata pesa yake bila kupitia mtandaoni kwa gharama robo ya zile ambazo zingekatwa mtandaoni..huku wao kwa wao watakuwa wanamalizana kupitia Bank account.

Mtumaji atakujulisha kuwa pesa inatumwa na Unayetumiwa utachukua bodaboda ya buku kwenda kwa Wakala kupokea kwa kulipa 2000 na Mtumaji naye atakuwa keshalipa kule 2000.

Yaani kiufupi Mtu unaendesha shughuli zako kwa amani huku ukibaki Mzalendo unayeipenda Serikali na usiyeitukana Serikali bila ya sababu.
 
Wakiona traffic ya hivyo wataweka zuio kwa limits maybe hamna kurushiana zaidi ya kiwango flani kwa siku ama mwisho mara 3 kuhamishiana mpaka baada ya masaa 24!
Wakiziba hapo bado kuna njia nyingne.. tukiwa siriaz hata hili litapatiwa ufumbuzi kama kwenye mabando
 
Acha kukaza fuvu ilo....

Shotly anamaanisha wamiliki wa mabus ya mkoa waanze kutoa huduma ya miamala. Mf. Wewe unakwenda pale Shekilango kwa Kilimanjaro express unawapa laki 1 huku babe wako anaenda Kilimanjaro express Arusha kuchukua hizo pesa.
Sheria haiwaruhusu wakibainika watajuta kufanya hivyo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom