Waliosikia kutukanwa Batilda washinda kesi bila alietukanwa kushitaki - imetokea Tanganyika

Alichoacha jaji ni kumfunga Lema Kama Mandela ilimapinduzi Yanze Kama Bengazi. Shame on them
 
Namuomba Mh. Lema na CHADEMA waingie kwenye uchaguzi watalikomboa tu hili Jimbo na CCM na serikali yake ndo watajua Watanzania wamewachoka. VIVA CHADEMA mapambano ya ukombozi wa nchi hii yaendelee na Mola yuko nanyi.
 
Hivi Lema kahukumiwa kwa kumtukana nani?. Aliyetukanwa hakushitaki, na hata mahakamani hakufika ila waliosikia wameshinda kesi. Walioshitaki ni wasikilizaji, hawa wasikilizaji wanaenda mahakamani bila evidence yoyote zaidi ya midomo yao. Yani sijawahi kuona ila imetokea Tanganyika. Na wanasema mahakama zina haki na usawa. Katika ushahidi ilitakiwa walioshitaki kuwa walisikia lema akitukana watoe ushaidi wa Tape yani maneno yaliyorekodiwa yakisikika lema akitamka ivyo au video iliyorekodiwa ikimwonyesha na kusikika maneno. Hapa ndio lema angepatikana na hatia. Kwasababu kwa upande wa lema napo kuna watetezi wake wanaosema kuwa lema hakutukana. sasa iweje hakimu awe upande mmoja?, ina maana kawaonea huu upande wa mashaidi wa lema ambao nao ushaidi wao ulikuwa ni mdomo. Kilichotakiwa hapa upande unaodai kusikia matusi watoe tape/video kuihakikishia mahakama ushaidi wao. Kwakweli kwa kesi ya lema hata kwa hakimu alieanza kazi juzi asingemhukumu lema, angetupilia mbali. Kwasababu upande wa walalamikaji ushaidi wao hakutosheleza. Tuko kwenye karne ya sayansi na technologia mikutano yote kuna tv, kuna wenye simu, video kamera na hata Phillips ndie yenyewe sauti safi sauti kubwa. Washtaki walitakiwa wawe na ushaidi wa kisasa kama ivyo. Sio kuibuka tu kuwa nilimsikia lema akitukana na Jaji anasema sawa mfungeni huyu. Wote wenye kesi na watetezi walikuwa sawa upande huu wanasema hakusema, upande mwingine wanasema alisema, kupata upande unaosema ukweli iliitajika tape ya maneno na video ya picha ikiambatana anayoyasema mshtakiwa (lema). Kwa namna hii serikali,ya Tanganyika kweli hakuna Majaji kama wapo basi wameongwa na watawala. Hivyo katika nchi hii haki haitapatikana mpaka siku katiba mpya itakapopatikana na kupata chama makini wa kuisimamia. Kwani sio kwamba sheria hazipo sheria zipo lakini zimechukuliwa na watawala wa chama cha mafisi. Majaji, Mahakimu wamekubali kuidhalilisha taaluma yao kwa ajili ya tamaa yao ya kuishi au kuganga njaa ya siku moja huku wananchi wakiteseka, na kulalamika kutokana na hukumu zao zisizofuata haki. Lakini nasema yana mwisho hata ipite miaka mingapi, haki itapatikana na ninawaonea huruma hao Majaji, Mahakimu wanaaopindisha sheria kwani, wapo akina lema waliozaliwa leo na wenye umri wa kujua ni nini kinafanyika leo. Hivyo usije ukaona/kusikia huyo Jaji/hakimu akifia jela kwa makosa aliyoyatenda miaka 20 nyuma. Mungu yupo yeye ndio muamuzi wa yote.

Juu ya hayo kweli Pesa iliyo tumika kumwangusha Lema ubunge wa arusha mjini ilikuwa ni kubwa muuuno kupita maelezo na matokeo yake pesa ilitafunwa na CCM kushindwa kwa nguvu zote walizo tumia sasa kiliwauma sana kweli umefika wakati hiyo kesi ingesikilizwa kwa Video au Tape mahakama kujiridhisha, Matokeo yake tume hukumu kwa kutumia hadithi wakati fika mikutano yote ilikuwa ina recodiwa.

NB;

Fitna za Matusi ya kumtukana Batlda yalianzia kur za maoni ndani ya CCM na hayo yote ndiko yalipo patikana leo hii imekuwa ni Lema kayasema kawaulizeni wana CCM wakati wa kura za Maoni Batilda alikuwa anasemwaje na wapinzani wake leo hii imekuwa Mtu wa Chadema aliyasema hayo?????

My Take;
Mahakama imfumbie fumbo mjinga
Jaji aliye hukumu kesi ya Lema alishinikizwa na ndio maana aliachia hukumu hewani kwa vifungu tata ili asije onekana mbaya alifanya kusudi kuwepo mkanganyiko.

Aibu kwa MAHAKAMA NA MAJAJI


 
Makosa yako kwenye kifungu cha sheria za uchaguzi namba 108(II) (a) Jaji kwa kudhamiria katumia kifungu cha sheria za uchaguzi namba 114 ambacho kinahusu makosa yaliyotokana na rushwa tu halafu ikulu inataka tuamini kwamba mahakama ni muhimili ulio huru? Dhamira yao Ilikuwa Lema akate rufaa, kesi ichukue muda mrefu, Arusha isiwe na mbunge kipindi chote hicho cha kesi. Kwa makusudi kabisa pamoja na kifungu hicho cha 114 kutoruhusu Yule aliye patikana na hatia kutokugombea kwa kipindi kisichozidi miaka mitano Jaji hakutamka adhabu hiyo, Kaacha hukumu inaelea. Ukombozi unakuja na ndio muda wake huu
 
Makosa yako kwenye kifungu cha sheria za uchaguzi namba 108(II) (a) Jaji kwa kudhamiria katumia kifungu cha sheria za uchaguzi namba 114 ambacho kinahusu makosa yaliyotokana na rushwa tu halafu ikulu inataka tuamini kwamba mahakama ni muhimili ulio huru? Dhamira yao Ilikuwa Lema akate rufaa, kesi ichukue muda mrefu, Arusha isiwe na mbunge kipindi chote hicho cha kesi. Kwa makusudi kabisa pamoja na kifungu hicho cha 114 kutoruhusu Yule aliye patikana na hatia kutokugombea kwa kipindi kisichozidi miaka mitano Jaji hakutamka adhabu hiyo, Kaacha hukumu inaelea. Ukombozi unakuja na ndio muda wake huu

Hii yote ni kutaka kuonekana kuwa CDM ni wakorofi katika Jimbo la arusha IKULU hawajui ni njia ipi ya kutumia kupambana na upinzani hawa kujua kuwa kadri siku zinavyo kwenda wananchi wanakuwa na mwamko tena mkubwa sana wakidhani skills zao za kijasusi zitawasaidi nawambieni hawa wanao jiiita Stategist wa kisiasa huko IKULU ni zero kabisa yaani hawasomi alama za nyakati au wanajaribu kuwadanganya walioko madarakani kuwa wananchi wako hivi.
IKULU ilitaka jaji ajifanye amekosea na kusema Lema hatoruhusiwa kugombea ila JAJI akastuka akona hapo sipo akaiachia hukumu juu kwa juuu ijikanganye ili na awe kwa safe side.

Political curiosity imeiweka MAHAKAMA kama muhimili mkuu wa taifa pabaya ni aibu sana kama wasomi waliosomeshwa kwa kodi za wananchi kupindisha mambo tuu just kwa kuridhisha wa puuzi fulani IKULU ni ujinga huo na kuiweka Tanganyika kwenye ramani ya wajinga fulani.

Leo hii kweli inaingia akilini kusema kweli JAJI hakujua hivyo vifungu??????? tayari ilisha leta taswila isiyo kuwepo na IMANI kati ya MAHAKAMA na wananchi kwa kosa la JAJI la Kipuuzi ati jaji kakosea kweli


 
Mahakama zote zipo upande wa ccm, lakini kama ulivyosema siku magamba wakipgwa chini lazima hawa majaji wahukumiwe kwa kupindisha sheria
 
Apparently, sioni haja ya kuwa na Law school kama ethics zao ziko hivi. ni matumizi mabaya ya rasilimali za serikali, na kuwapotezea muda watu tu. na kama wao wameguswa na hii kesi kama mahakimu tunawaomba watoe tamko. Ni udhalilishaji wa taaluma za watu. Reputation ya mahakama ikiharibika kama alivyofanya huyu hakimu; wote mtaonekana makanjanja. hatari yake, wananchi watatafuta njia mbadala ya kudai haki zao ambayo haitabagua kati ya ethical and non ethical lawyers. The time will tell.
 
Ila iliotumika katika hukumu ya kesi ya lema inawezekana nchini tanganyika tu chini ya serikali ya mafisi, Duniani kote ushahidi huu huwezi kupata ushindi hata kwa kumtumia maji marefu
 
Siajabu kwani hata meya wa Dar es Salaam aliwahi kusema kuwa watu wengine wanafikiri kwa ma... hakukosea kwani hata mtu ambaye hana ufahamu mkubwa wa kisheria hawezi kubali kwamba jaji aliyehitimu anaweza kutoa hukumu ya aina ile; Let's wait to see what will happen
 
Mungu yupo! Haki zetu zinaporwa na hawa wala roho za watu, ulevi wa madaraka ni mbaya kuliko ulevi wa pombe

Kweli mkuu sidhani kama ulivi wa pombe unaweza kuleta madhara makubwa kama haya yanayokuja kama hasara ya kurudia uchaguzi na haki za wanyonge kutosikilizwa
 
Nimesoma posti karibuni zote na kujidhihirisha kwa nini wanasheria wanaitwa learned brothers/sisters.

Mtu Kama hujui sheria basi utabaki kuwa na hisia zako ambazo hazina uthibitisho mahakamani.
Wengine wanaenda mbali kudai kuwa mbona Batilda hakuwepo mahakamani, nami nauliza mtu aliyeuwawa na mtu mwingine huwa anakuja kutoa ushahidi?

Sheria ni kitu ingine bana, na ukiingia na ujuaji waweza kula mvua bila kujielewa.
Watu tuliowahisi wauaji Kama Zombe wametumia mwanya wa sheria kwa ufanisi mkubwa na hivyo kukwepa kitanzi.

Tukumbuke umaarufu wa kisiasa si kipingamizi cha kutochukuliwa hatua za kisheria.

Nyie mnao tetea sana hili hebu muungane kumpeleka Lusinde (aka mheshimiwa wa matusi)lupango.
 
Wana JF na wapenda CDM popte mlipo,

Vyovyote ilivyo,hukumu hii ya kutengua Ubunge wa Mhe. G.Lema imeacha maswali mengi sana kuliko majibu! Hili liko wazi kwa kila Mtanzania mwenye kujua SHERIA na asiyejua. Haya ni mambo ya kijinga kabisa kabisa. Haiwezekani kweli anayedaiwa kuwa MLALAMIKAJI katika kesi hii ambaye ni MATILDA BURIAN hakupeleka malalamiko yake NEC wala hakufungua MASHTAKA BINAFSI!
Hata baada ya kesi kuendeshwa kwa muda wote huu MATILADA BURIAN hakuwahi kuitwa Mahakamani hata siku moja kuthibitisha kuwa kweli ALITUKANWA AU KUDHALILISHWA kulingana na madai ya wale wehu 3 waliofungua kesi hiyo Mahakamani kwa niaba yake.

Swali ni JE, MAHAKAMA INAWEZA KUENDESHA KESI YA MLALAMIKAJI MWANZO MPAKA MWISHO BILA YA MLALAMIKAJI KUITWA MAHAKAMANI? JE,SHERIA INASEMAJE KATIKA HILI. Najua kwa mshtakiwa anaweza kushtakiwa Mahakamani bila ya yeye kuwepo lakini mwisho wa Hukuma lazima awepo ili asomewe hukumu yake kama ni viboko,kulipa faini au kifungo ili atekeleze hukumu ya Mahakama. Wataalamu wa Sheria wanaita: DEFENDANT TRIAL IN ABSENTIA! Je Wanasheria mwaweza kutuambia kama kuna kipengele cha JUDGEMENT IN PLAINTIFF ABSENTIA??

Kwamba aliyetukanwa hakwenda Mahakamani baali wakawepo wawakilishi wake tu kuanzia mwanzo wa keshi mpaka hukumu bila ya mdai kuwepo Mahakamani! Hii yawezekana kisheria au ipo Tanzania tu kwa ajili ya kukomoa upinzani??

Naamini CHADEMA ina wanasheria wazuri sana akiwemo Tundu Lissu na Prof. Safari. Hebu watuchambulie hukumu hii na watoe mwelekeo wa Chama ili tujue kama Mhe. Lema atogombea tena na kama atakata rufaa.

Nini kinajiri hapo NMC???
 
Under such circumstancial atmosphere the integrity of the judiciary is held ransom and is extremelyquestionable. There is an interlinkage between the court ruling and the interests of the clientele . I can assume the interest of the court at the hands of the state superceeded the interests of the clientele who tended not to engage herself completely neither to appear to the courtrooms. This is indeed a complete ridicule to the contemporary court rulling in the world. Probably this needs a register to the guiness book of records!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
hivi lema kahukumiwa kwa kumtukana nani?. Aliyetukanwa hakushitaki, na hata mahakamani hakufika ila waliosikia wameshinda kesi. Walioshitaki ni wasikilizaji, hawa wasikilizaji wanaenda mahakamani bila evidence yoyote zaidi ya midomo yao. Yani sijawahi kuona ila imetokea tanganyika. Na wanasema mahakama zina haki na usawa. Katika ushahidi ilitakiwa walioshitaki kuwa walisikia lema akitukana watoe ushaidi wa tape yani maneno yaliyorekodiwa yakisikika lema akitamka ivyo au video iliyorekodiwa ikimwonyesha na kusikika maneno. Hapa ndio lema angepatikana na hatia. Kwasababu kwa upande wa lema napo kuna watetezi wake wanaosema kuwa lema hakutukana. Sasa iweje hakimu awe upande mmoja?, ina maana kawaonea huu upande wa mashaidi wa lema ambao nao ushaidi wao ulikuwa ni mdomo. Kilichotakiwa hapa upande unaodai kusikia matusi watoe tape/video kuihakikishia mahakama ushaidi wao. Kwakweli kwa kesi ya lema hata kwa hakimu alieanza kazi juzi asingemhukumu lema, angetupilia mbali. Kwasababu upande wa walalamikaji ushaidi wao hakutosheleza. Tuko kwenye karne ya sayansi na technologia mikutano yote kuna tv, kuna wenye simu, video kamera na hata phillips ndie yenyewe sauti safi sauti kubwa. Washtaki walitakiwa wawe na ushaidi wa kisasa kama ivyo. Sio kuibuka tu kuwa nilimsikia lema akitukana na jaji anasema sawa mfungeni huyu. Wote wenye kesi na watetezi walikuwa sawa upande huu wanasema hakusema, upande mwingine wanasema alisema, kupata upande unaosema ukweli iliitajika tape ya maneno na video ya picha ikiambatana anayoyasema mshtakiwa (lema). Kwa namna hii serikali,ya tanganyika kweli hakuna majaji kama wapo basi wameongwa na watawala. Hivyo katika nchi hii haki haitapatikana mpaka siku katiba mpya itakapopatikana na kupata chama makini wa kuisimamia. Kwani sio kwamba sheria hazipo sheria zipo lakini zimechukuliwa na watawala wa chama cha mafisi. Majaji, mahakimu wamekubali kuidhalilisha taaluma yao kwa ajili ya tamaa yao ya kuishi au kuganga njaa ya siku moja huku wananchi wakiteseka, na kulalamika kutokana na hukumu zao zisizofuata haki. Lakini nasema yana mwisho hata ipite miaka mingapi, haki itapatikana na ninawaonea huruma hao majaji, mahakimu wanaaopindisha sheria kwani, wapo akina lema waliozaliwa leo na wenye umri wa kujua ni nini kinafanyika leo. Hivyo usije ukaona/kusikia huyo jaji/hakimu akifia jela kwa makosa aliyoyatenda miaka 20 nyuma. Mungu yupo yeye ndio muamuzi wa yote.
 
Ningependa Iwe kama katiba Mpya ya Kenya Majaji wanachaguliwa na Rais, lakini wanadhihirishwa au kutodhihirishwa na Bunge la Nchi; wanachambuliwa wanaangaliwa makosa yao na mazuri yao ndipo wanapitishwa na bunge

Sio lelemama; Kama sasa oh tulikuwa hatuna Jaji Mkuu wa Dini fulani; Tulikuwa hatuna Jaji Kiongozi wa Dini Fulani; Tulikuwa hatuna Jaji Mfawidhi wa Dini Fulani... Sheria ni haki ya Mwananchi Sio haki ya tabaka moja


 
Mie si Mwanasheria lakini jambo moja nalifahamu kidogo katika hili! Kwamba, ikiwa X yupo na Y peke yao, halafu X akamtusi Y kisha Y akaenda mahakamani kwamba ametukanwa na X....hapo hakuna kesi unless X akubali mwenyewe kwamba ni kweli alitenda kosa!!!!

Kwa upande mwingine, ikiwa palikuwapo watu wakati X anamtukana Y, na watu hao wakaenda kutoa ushahidi.....basi hapo kesi ipo na wala hapahitajiki CD au Kaseti kuthibitisha!!

Tusisahau kwamba, HAKI na SHERIA na vitu tofauti.....pale kinacho-apply ni namna gani wahusika (upande wa mashitaka na washitakiwa) wanavyoweza kucheza na maneno na vifungu!! Na hiki ndicho kinachofanywa na wakili! Wakili anafahamu wazi kwamba jambo fulani umefanya.....lakini yeye atatumia udhaifu wa upande wa pili wa kushindwa kucheza na maneno na vifungu vya sheria ili mteja wake aonekane hajatenda kosa ingawaje anafahamu ametenda kosa!!

Hivyo basi, inategemea ni jinsi gani upande wa CCM walikuwa ni wataalamu wa kujenga hoja na ni namna gani upande wa CHADEMA walishindwa kujenga hoja!

Hoja kwamba, Dr. Buriani hakwenda mahakamani au sio aliyeshitaki, haina msingi kisheria!! Hata wewe kama umekerwa na ile hotuba ya Joseph Lusinde kule Arumeru, unaweza kwenda mahakamani na kumshitaki……!
 
Nimesoma posti karibuni zote na kujidhihirisha kwa nini wanasheria wanaitwa learned brothers/sisters.

Mtu Kama hujui sheria basi utabaki kuwa na hisia zako ambazo hazina uthibitisho mahakamani.
Wengine wanaenda mbali kudai kuwa mbona Batilda hakuwepo mahakamani, nami nauliza mtu aliyeuwawa na mtu mwingine huwa anakuja kutoa ushahidi?

Sheria ni kitu ingine bana, na ukiingia na ujuaji waweza kula mvua bila kujielewa.
Watu tuliowahisi wauaji Kama Zombe wametumia mwanya wa sheria kwa ufanisi mkubwa na hivyo kukwepa kitanzi.

Tukumbuke umaarufu wa kisiasa si kipingamizi cha kutochukuliwa hatua za kisheria.

Nyie mnao tetea sana hili hebu muungane kumpeleka Lusinde (aka mheshimiwa wa matusi)lupango.

Mkuu umejitahidi kueleza vizuri! Lakina sheria inaweka wazi kabisa kwa kesi kama ya Lema ya kwamba, Mtu aliyedhalilishwa kwa matusi lazima yeye ndiye anayetakiwa kushitaki mahakani na aeleze ni namna gani ameathirika na matusi hayo! Na kwa kesi ya kifo ni case tofauti!
 
Lema hakuhukumiwa na Mahakama, bali alihukumiwa na Rwakibarila.
 
Back
Top Bottom