Waliosikia kutukanwa Batilda washinda kesi bila alietukanwa kushitaki - imetokea Tanganyika

popote duniani hili linawezekana. Hata wewe unaweza fungua kesi dhidi ya lusinde et al kwa matusi yaliyoporomoshwa majuzi. Tatizo kwenye kesi ya Lema ni hukumu ya kisiasa, basi, ila kisheria inawezekana
 
Mbivu na mbichi ni leo pale NMC grounds km ni mapambano ya kipinga kunyanyaswa yaanze rasmi hata hao viongozi wanahofu kubwa na huko arusha.
 
Askofu Laizer , Amesema Mahakama imetenda haki , Shame on him , Hawezi kupata heshima inaonekana amenunuliwa na mafisadi ,
 
Kutenda haki na hukumu humpendeza Bwana Mungu.Pia asiye haki hutoa rushwa kifuani ili kuzipotosha njia za hukumu.Haya yote ni chukizo kwa mwenyezi Mungu.Tanzania tunakosa baraka hivi hivi kwa ajili ya ubovu wa viongozi wetu.Kusema kweli huyu jaji kakosea sana,kapindisha hukumu.Yule mama Matilda alitakiwa atoe ushahidi mahakamani akiwa na ushahidi wa vielelezo kama recorded CD au au VCD.
 
Hii ni syllabus mpya katika fani ya sheria nchini, haijapata tokea 3rd party tena hana documentary evidence ashinde kesi hii ya 'defamation'. Hivi ingetoke mhusika 'BATILDA' ameaga dunia wakati kesi ikiwa inaendelea jaji angechukua uamuzi gani?. Duh.
 
Ukiwa unafuga mbwa na unajitahidi kumhudumia,siku 1 usiku wa manane ndani ya fensi yako ukarusha mfupa mkubwa nje kupitia dirishani,mbwa wako akainuka kwa mapozi na kuufuata mfupa ule,utambue wazi huyo chapa risasi.Mahakama zetu hazina uhuru wa kuamua mambo ya haki na ya msingi,leo mfuko unaongea.Sasa,uelewe wazi mahakama ni tofauti bunge na pia utawala.Leo mahakama inapeleka viganja kuomba hela,sasa mahakama itathubutu kuibwekea serikali?Mfumo wetu ubadilishwe.Naomba kuwasilisha
 
Inajulikana wazi mahakama zetu haziko huru. Cheki mfano mwingine ile Kesi ya mtikila ya mgombea binafsi.
 
Naomba nitangulize haki kuliko ushabiki wa kisiasa. Ninachoshangaa hapa ni kitu kimoja kikubwa kwenye mfumo wa sheria ya nchi yetu. Kesi ya uchaguzi ni civil case- election petition! Yawezekanaje watu fulani i.e third parties wakaenda mahakamani kufungua kesi inayohusu mtu mwingine kutukanwa ama kudhalilishwa kwenye kampeni ya uchaguzi?
Kwanza, suala la msingi hapa ni LOCUS QUO. Yaani hao wanaolalamika wameathirika kwa kiasi gani na hayo matusi mpaka kushitaki? Kwa maneno mengine wana maslahi gani na hiyo kesi? Vinginevyo hawana haki ya kushtaki! Jamani hivi waweza kwenda kumshitaki mdeni wa rafiki yako ili rafikiyo alipwe na kesi ikawapo kweli? Kama ni hivyo basi sheria zetu zina hitilafu!
Ninachomaanisha ni kwamba third parties waweza kufungua kesi kulalamikia jambo lolote ambalo wao wanaathirika moja kwa moja mfano walizuiwa kupiga kura ilhali wana sifa, kuchakachuliwa matokeo n.k.
Pili, ninapata wasiwasi pia kwenye ushahidi katika kesi hii. Ushahidi wa mdomo unakuwa dhaifu sana kumtia mtu hatiani ukizingatia upande mwingine unakanusha. Pamoja na ukweli kesi itaamuliwa on a balance of probabilities kulitakiwa kuwe na ushahidi mwingine wa kanda za sauti au video. Lakini la mwisho kabisa ni pale aliyetukanwa anapopuuzwa kwenye ushahidi! Kwa maoni yangu naona huyu mtu ni muhimu sana. Je, akikana kutukanwa au kudhalilishwa? Kutakuwa na kesi hapo? Tukiendekeza mashauri ya namna hii tutasababisha mfumo wetu wa sheria uonekane kituko mbele ya jamii na mataifa!
Kwa mtazamo wangu hii kesi ikienda kwenye appeal or review yaweza hukumu kutenguliwa lakini kwa mfumo wa mahakama nchini kesi hii yaweza kuamuliwa kwa muda usiopungua miaka 3!
Naomba kuwasilisha,
 
Hukumu imetoka ikulu hapa jaji kaisoma tu kama asante ya KUPEWA UJAJI. AIBU KWAKE YEYE BINAFSI NA TAALUMA YA SHERIA NCHINI
 
popote duniani hili linawezekana. Hata wewe unaweza fungua kesi dhidi ya lusinde et al kwa matusi yaliyoporomoshwa majuzi. Tatizo kwenye kesi ya Lema ni hukumu ya kisiasa, basi, ila kisheria inawezekana

naomba kujuzwa wale locus stand ya kushtaki wamepata vp?kwa kifungu gan cha sheria na kwa sheria ipi
 
Mpeni wakati mugumu huyo Judge! Nashindwa kuelewa hapo mitaani anapitaje huyu mbumbumbu! Naamini CDM watafanya kweli maana kule kuna mitambo ya sheria zaidi ya majaji wa Baba MwanaAsha!
 
kwa trend hii haki haipaswi kuombwa. kama mbunge amebambikizwa kesi iliyomvua ubunge, je ni wananchi wangapi magerezani wanatumikia kesi halali? Uwezo mdogo na tamaa za viongozi wetu, watalitumbukiza taifa kwenye maafa makubwa. ikiwa Lusinde ambaye ushahid ni ku-tune to redio au tv unapatikana; anadunda tu mtaani kama shujaa wa-ccm. Ikiwa mzazi wa watoto wengi then wengine unawasaidia kuvunja sheria na taratibu (katiba) halafu wengine kuwakemea vikali...utawala bora hauwez kupatikana, aman, upendo vitatoweka tu. So, as to me, kesi hii iwe chachu kwa wananchi kushiriki kikamilifu kwenye mchakato wa katiba maana hii ni input kwetu kwa TZ tunayoitaka. Mungu ibariki Tanzania, Mungu wabariki watetea haki.
 
Huyu Judge amefanya fadhira kwa aliempa hicho cheo,kadhalika najua CDM kuna wataalamu wa Sheria ngoja tusubirie leo NMC Mwenyekiti atasema nn lakn hii nchi haina Demokrasia kabisa na hizi three Organs haziko huru kabisa
 
Back
Top Bottom