Waliosikia kutukanwa Batilda washinda kesi bila alietukanwa kushitaki - imetokea Tanganyika

Kuntakint

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
1,767
1,525
Hivi Lema kahukumiwa kwa kumtukana nani?. Aliyetukanwa hakushitaki, na hata mahakamani hakufika ila waliosikia wameshinda kesi. Walioshitaki ni wasikilizaji, hawa wasikilizaji wanaenda mahakamani bila evidence yoyote zaidi ya midomo yao. Yani sijawahi kuona ila imetokea Tanganyika. Na wanasema mahakama zina haki na usawa. Katika ushahidi ilitakiwa walioshitaki kuwa walisikia lema akitukana watoe ushaidi wa Tape yani maneno yaliyorekodiwa yakisikika lema akitamka ivyo au video iliyorekodiwa ikimwonyesha na kusikika maneno. Hapa ndio lema angepatikana na hatia. Kwasababu kwa upande wa lema napo kuna watetezi wake wanaosema kuwa lema hakutukana. sasa iweje hakimu awe upande mmoja?, ina maana kawaonea huu upande wa mashaidi wa lema ambao nao ushaidi wao ulikuwa ni mdomo. Kilichotakiwa hapa upande unaodai kusikia matusi watoe tape/video kuihakikishia mahakama ushaidi wao. Kwakweli kwa kesi ya lema hata kwa hakimu alieanza kazi juzi asingemhukumu lema, angetupilia mbali. Kwasababu upande wa walalamikaji ushaidi wao hakutosheleza. Tuko kwenye karne ya sayansi na technologia mikutano yote kuna tv, kuna wenye simu, video kamera na hata Phillips ndie yenyewe sauti safi sauti kubwa. Washtaki walitakiwa wawe na ushaidi wa kisasa kama ivyo. Sio kuibuka tu kuwa nilimsikia lema akitukana na Jaji anasema sawa mfungeni huyu. Wote wenye kesi na watetezi walikuwa sawa upande huu wanasema hakusema, upande mwingine wanasema alisema, kupata upande unaosema ukweli iliitajika tape ya maneno na video ya picha ikiambatana anayoyasema mshtakiwa (lema). Kwa namna hii serikali,ya Tanganyika kweli hakuna Majaji kama wapo basi wameongwa na watawala. Hivyo katika nchi hii haki haitapatikana mpaka siku katiba mpya itakapopatikana na kupata chama makini wa kuisimamia. Kwani sio kwamba sheria hazipo sheria zipo lakini zimechukuliwa na watawala wa chama cha mafisi. Majaji, Mahakimu wamekubali kuidhalilisha taaluma yao kwa ajili ya tamaa yao ya kuishi au kuganga njaa ya siku moja huku wananchi wakiteseka, na kulalamika kutokana na hukumu zao zisizofuata haki. Lakini nasema yana mwisho hata ipite miaka mingapi, haki itapatikana na ninawaonea huruma hao Majaji, Mahakimu wanaaopindisha sheria kwani, wapo akina lema waliozaliwa leo na wenye umri wa kujua ni nini kinafanyika leo. Hivyo usije ukaona/kusikia huyo Jaji/hakimu akifia jela kwa makosa aliyoyatenda miaka 20 nyuma. Mungu yupo yeye ndio muamuzi wa yote.
 
Mungu yupo! Haki zetu zinaporwa na hawa wala roho za watu, ulevi wa madaraka ni mbaya kuliko ulevi wa pombe
 
• MAWAKILI WATEMA CHECHE

Na Mwandishi wetu

MAWAKILI wawili wa mjini hapa, wamedai kuwa hukumu iliyomua ubunge Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, ilikuwa na dosari nyingi za kisheria na kwamba imetoa doa katika mhimili huo wa dola.


Wakili Method Kimomogoro aliyemtetea Lema katika kesi hiyo, amezidi kutema cheche safari hii, akidai kuwa hukumu iliyotolewa na Jaji Rwakibarila haikuzingatia hoja muhimu zaidi ya 30 alizoainisha kwenye hati yake ya majumuisho.

Amesema kuwa jaji katika hali ya kushangaza alitumia ushahidi wa wadai na mashahidi waliothibitika kuwa viongozi na wanachama wa CCM huku akipuuza ushahidi wa upande wa utetezi kwa hoja kuwa mashahidi walikuwa viongozi na wanachama wa CHADEMA ambao walikuwa na maslahi katika kesi hiyo.


Alisema kuwa hoja nyingine muhimu ambayo Jaji Rwakibarila hakuizungumzia wala kutolea uamuzi ni ile ya wadai kushindwa kutoa ushahidi mwingine zaidi ya ule wa kusikia ambapo awali walidai wangeleta mahakamani hapo nakala za CD zinazomwonyesha Lema akihutubia na kutoa maneno ya kashfa, udhalilishaji na ubaguzi kidini, lakini hawakuzileta wala hawakutoa sababu za kushindwa kufanya hivyo.


Kimomogoro alisema hoja nyingine ambayo haikufanyiwa kazi ni ile aliyoieleza mahakamani kuwa ni ushahidi wa kimazingira ulioonyesha kuwa Lema asingeweza kutoa maneno kuonyesha kuwa wanawake hawana uwezo wa kuongoza kwa sababu kwenye timu yake ya kampeni alikuwa akiongozana na wagombea udiwani wanawake ambao aliwanadi na kuwaombea kura.


Aidha CHADEMA ilisimamisha wagombea udiwani wanawake watatu kwenye kata za jimbo la Arusha Mjini na mgombea ubunge mwanamke katika jimbo la Longido ambalo wenyeji wake ni Wamaasai.


Kimomogoro alisema kuwa hoja nyingine ni ile ya CCM na mgombea wake Dk. Burian aliyedaiwa kukashfiwa kutolalamika kwenye kamati ya maadili ya jimbo licha ya kupewa fursa hiyo kisheria.


“Jaji aliacha hoja nyingi bila kuzishughulikia na kuzitolea uamuzi ndiyo maana aliweza kusoma na kumaliza hukumu yake ndani ya saa moja licha ya ukweli kwamba mimi niliwasilisha majumuisho ya kurasa 60, mawakili wa walalamikaji walileta majumuisho yenye kurasa 30 pamoja na maelezo ya mashahidi walikuwa 18 na hoja za mawakili wa serikali ambazo kama angepitia zote ninaamini angetumia muda mrefu zaidi kutoa hukumu yake,” alieleza wakili Kimomogoro.


Hata hivyo wakili huyo alisema kuwa atakuwa kwenye nafasi nzuri ya kuzungumzia suala hilo wiki ijayo baada ya kupata nakala ya hukumu ambayo inachapishwa kabla ya kujiandaa kukata rufaa.


Alisema kuwa kutokana na kuwa na nakala ya mwenendo ya kesi waliyokuwa wakipewa kila wiki anaweza kuandaa na kuwasilisha rufaa yake mwisho wa mwezi huu na kulingana na taratibu za kimahakama zilivyo kwa sasa mpaka mwezi Juni maamuzi yatakuwa yamepatikana.


Kwa upande wake Mkuu wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Kanda ya Arusha, Shilinde Ngalula, alisema Jaji huyo alitoa uamuzi ambao umeacha shaka kubwa, ikiwa una dhamira ya kweli ya kimahakama au ina mikono ya watu kama inavyolalamikiwa.


Aliongeza kuwa kwa mujibu wa sheria, Jaji hupaswa kutoa hukumu kwa kusema makosa aliyomtia nayo hatiani mshtakiwa sanjari na kutamka adhabu hivyo kama atakuwa ametumia kifungu 114 cha sheria ya uchaguzi.


Kifungu hicho kinahusu “Illegal Practice” ambacho kinaangukia kwenye makosa yanayohusiana na vitendo vya rushwa kwa wapiga kura, watendaji wa serikali na watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), hivyo alipaswa kutamka wazi kuwa Lema hatagombea ubunge kwa kipindi cha miaka mitano.


“Hukumu ndiyo inayotamka adhabu; huwezi kuhukumiwa halafu uende kwenye vifungu vya sheria kuanza kuangalia nimetiwa hatiani adhabu yangu inakuwaje, mahakama ndiyo yenye jukumu hilo la kutamka vifungu vya adhabu na si kutamka kutengua matokeo ya uchaguzi na kuacha kutamka vifungu vya kanuni ya adhabu,” alisisitiza mwanasheria huyo.


Hoja nyingine ambayo inalalamikiwa katika uamuzi huo ni juu ya Lema kutiwa hatiani kwa kosa la kumkashfu aliyekuwa mgombea wa CCM, Dk. Batilda Burian, akidai kuwa suala la kashfa hufikishwa mahakamani na yule aliyekashfiwa na si vinginevyo na lithibitike.


“Kesi za kashfa huwa hazirithiwi ndiyo sababu endapo anayedaiwa kukashfiwa akifariki basi na kesi hiyo huishia hapo,” alifafanua.


“Kama Lema alitamka maneno hayo na kudhihirika kweli kuwa yalikuwa ya kashfa basi, shauri la kukashfiwa lingefunguliwa na Dk. Burian mwenyewe aliyekashfiwa na si mtu mwingine,” alisema.


Wakili huyo alisema kuwa kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi, makosa yote mawili yanaangukia kwenye kifungu cha 108 (II)(a) ambayo humruhusu aliyevuliwa ubunge kugombea kwenye uchaguzi mdogo utakaoitishwa.


Naye, wakili wa wadai kwenye shauri hilo Modest Akida, aliliambia gazeti hili kwa njia ya simu kuwa Jaji Rwakibarila alitumia kifungu cha 114 kumtia hatiani Lema lakini hakutamka sheria ya kanuni ya adhabu anayopaswa kuitumikia baada ya kutiwa hatiani.


Jaji Rwakibarila alimtia Lema kwa kudaiwa kutoa kauli kuwa Dk. Burian si mwaminifu kwenye ndoa yake kwani alikuwa na mtoto aliyezaa nje ya ndoa yake na kwamba alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Edward Lowassa.


Hata hivyo Ngalula alisema kuwa kama ni kweli kwenye hukumu hiyo kuna mkanganyiko unaoongelewa unaweza kuondolewa kwa Jaji Rwakibarila kuipitia (review ) na kuifanyia marekebisho au kwa Jaji Mkuu au Mahakama ya Rufaa nchini kuipitia na kuifanyia marekebisho (Revision) ili kuondoa mkanganyiko huo.


CHADEMA kutoa msimamo leo Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, leo anatarajiwa kutoa msimamo wa chama kama kitachukua uamuzi wa kukata rufaa kupinga hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha iliyomvua ubunge Lema au la.


Mwenyekiti wa CHADEMA wilayani Arusha, Ephata Nanyaro, alisema kuwa msimamo huo utatolewa kwenye mkutano wa hadhara utakaofanyika katika viwanja vya NMC.

 
Judiciary Weakness can prove a biggest calamities in our nation if the new constitution will not make a change and separate the 3 power of JUDICIARY; PARLIAMENT and PRESIDENT have to separate them and at least give a limitation that no one among them is above the rule of law, and we the people we will follow constituency to attain our freedom, independence and rights to follow our religious rights.
 
Mahakimu na majaji wa Tanzania wanahongeka kwa bei cheeee, tena wanaiogopa sana na wanaitikia sana kila lisemwalo na CCM, kiasi kwamba wanasahau kabisa ethics za uanasheria
 
Inatakiwa majaji na mahakimu Tanzania walaani kabisa Jaji kama huyu ambae ameidhalilisha sana taaluma yao. Taaluma hata ya ualimu ilianza kushushwa hadhi kwa kuendekeza kuingiza vihiyo katika fani, hata Sheria sasa imeingiliwa. Wanasheria chukueni hatua haraka mlinde taaluma yenu.
 
Mimi sijui wala sifahamu mengi kuhusu tasnia ya Sheria ila kwa haya niliyoyasoma hapo juu ni dhahiri kabisa lengo la hukumu ya Jaji ni kumuondoa au kumvua Lema uongozi na sio kumuhukumu kwa kosa alilofanya.
 
Wakuu hukumu ile imejaa mawaa mengi sana na jukumu la wapenda haki wote kuilaani sana.
 
Jaji mkuu Chande ili alinde heshima ya mahakama chini ya uongozi wake hana budi kuingillia kati na kufanya review ya hukumu hii ya Lema non-partisanly kama alivyoingilia uamuzi wa mahakama ulipotoa arrest warrant kukamatwa Askofu Mokiwa kwa kumsimika Askofu huko huko Arusha!!
 
Narudia kusema tena kunamambo yanatokea Tanzania tu na si kwinine dunia hihi
 
Hii ndio athari ya majaji ambao rais amekuwa akiwateua ovyo ovyo bila kujali viwango vyao eti kwa lengo la kuongeza idadi ya majaji nchini!
 
Hata mahakama imeingiliwa na wakata nyasi kama ualimu? Hii Tanzania ni nchi ya kipekee Duniani kwa mambo mengi mojawapo ni hili.
 
Mimi sijasomea sheria na kwa staili hii siipendi tena tasinia hiyo,ina maana hukumu imetolewa ili watu tuilaani tu au kisheria twaweza kuchukua hatua?Hainiingii akilini mtu aliewekwa kusimamia haki anaipindisha kiuwazi kiasi kwamba hata sisi tusiojua sheria tunaona kabisa kama katoa hukumu kwa shinikizo au kaahidiwa ulaji jamani?Na mashaka yangu yalizidi pale Ikulu ilipojibu malalamiko ya Lema haraka mno kiasi kwamba nina kuwa na wasiwasi kwamba walijua atalalamika coz hukumu walikuwa nayo tayari,sidhani kama nitakuwa nimekosea sana kuwaza kuwa hukumu ilitoka kwingine na jaji Rwakibarila alipewa tu kuisoma na sidhani kama alipata muda wa kuipitia coz angengundua mapungufu mengi na asingekubari kudhalilisha taaluma yake ki hivyo.....Hii ndio Tanzania yetu inayotembea gizani bila taa...
 
iko siku mambo ya aina hii yataleta hatari kubwa katika nchi hii, polisi wala jeshi hawataweza kuzuia. nafikiri wenzetu kenya wanaheshimiana baada ya ile vurugu kule kwao.
 
Siku ya mwisho kutakuwa ni kilio na kusaga meno, na ni vigumu matajiri kuuona ufalme wa Mbinguni kuliko Ngamia kupenya kwenye tundu la sindano!
 
Tanzania zaidi ya uijuavyo!

Inabidi hili ajabu liingizwe kwenye guiness book of records!
 
Majaji hapa nchini wanatakiwa kufanya kazi zao kwa kuzingatia miiko ya taaluma zao na si vinginevyo. Hukumu juu ya kesi ya Lema imeacha sintofahamu na uvulivuli mwingi miongoni mwa wananchi wengi wapenda haki.
 
Back
Top Bottom