Waliobahatika Viwanja vya Geza Ulole

Inakera sana, tena unaweza kukuta toto lenyewe hata kazi halina na halijui kusoma wala kuandika, linatambaa lakini kwa kuwa ni toto la rais basi linakuwa li-rais la watendaji wenye elimu lakini waoga. Pole sana mkuu
 
baada ya uhuru wa sudan kusini taifa lililobaki duniani ni tanganyika.
pole kaka tukipata uhuru kila kitu kitakuwa swaafi.
 
Kwa vile Tanzania inaongozwa na Utawala wa Sheria, basi nyie mliokosa viwanja mna haki kamili ya kukata Ruffaaa na kujua ni kigezo gani kilitumika katika kugawa viwanja hivyo.

Na msiporidhika na hapo mna haki kamili ya kwenda mahakamani na kusimamisha zoezi lenyewe mpaka suala lenu litakapopatiwa ufumbuzi.

Pole sana ila tumia haki yako kisheria na kikatiba


Kwani ni lazima sana uandike hata kama ni upuuzi?
 
Kwanza hivyo viwanja mkipewa mtajenga na maneno? waachieni wenye uwezo wa kujenga.
 
Hivi hawa kina Mwandosya na Mama Ghasia, zile nyumba walizouziwa OysterBay haziwatoshi? Viwanja vyao vya Mbezi Beach bado haviwatoshi? Khalfani Kiwete baba ake si anawajengea mahekalu kule Msoga? Kwa kweli inasikitisha... Kweli hata Yesu Kristo alisema mwenye nacho uongezwa...
 
Mshrika pole sana, haya ndio mafunzo, tunakwenda wapi......?????. anyway usikate tamaa
 
Na wewe ndio umetumia akili hapo.......acheni ushabiki wa kijinga...hakuna topic zingine zaidi ya kusema watu bila mpango, ooo watoto wa wakubwa mara wanaccm, yote hii ni wivu....

Inawezekana na wewe ni mmojawapo....
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Na wewe ndio umetumia akili hapo.......acheni ushabiki wa kijinga...hakuna topic zingine zaidi ya kusema watu bila mpango, ooo watoto wa wakubwa mara wanaccm, yote hii ni wivu....
Natamani ningepata bahati ya kuona sura yako, nione unafananaje!. Sio binadamu wa kawaida wewe.
 
Uliowataja sioni hata mmoja aliyebahatika! Kwa mbaaaaaaali labda ingekuwa wao hao wanagombania kiwanja kimoja na mmoja wao kupata ningekubali kuwa AMEBAHATIKA.
 
matajiri na wenye vyeo ndio watu wenye bahati zaidi Tanzania. Lazima tuharibu dhana hii kwa vitendo!
 
Bora mkoa wangu una ukame,njaa,vumbi,hauna madini, udongo umechoka hili linanipa uhakika kuwa nitabaki na kiardhi changu hata kama kidogo
 
Kaka pole sana,tuzidi kumbambana kwa ajiri ya kuwatoa madarakani hawa CCM mana watoto wao ndiyo huwa wanafaidi, mali za wananchi maskini watanzania.
 
Back
Top Bottom