Elections 2010 Walio hudhulia Kikao cha Siri Mwanza hawahapa,, Mmoja hajasema kitu

well hii barua sawa lakini naitilia shaka kwa upande fulani, itakuwaje iandikwe wazi namna hiyo wakati inajulikana ni siri kubwa? sitaki kuamini kuwa tunao viongozi bogus namna hii hata kutenda kosa wanakosea tena!

Kwanza hao walio mix matokeo na wewe tutasemaje??ina maana hawana akili vizuri??Na wenyewe ni ma bogus pamoja na huyo aliyeandika mhii barua..unajuwa mkuu mambo yakizidi kuwa mengi lazima uchanganyikiwa na ndio hivyo ilivyokuwa!!
 
Hawa atu tuwashikirie hivihivi kwasababu watafikiri sisi Watanzania ni wajinga kama jana alivyo kuwa anajieleza,,
Inabidi tufikie hatua Tukubali kuwa Katiba yetu na sheria Zentu tulizo ziweka hapa nchini zinatakiwa zifanyiwe marekebisho makubwa kwa ustawi wa Tanzania Yetu,, hii itasaidia Sana kwenye maendeleo yetu sisi Watanzania na Selikali yetu,, naona hata Fedha yetu itapanda kwani Sababu za kupanda ki uchumi zipo,, Nia pia Zipo,, miundo mbinu imebanwa na chances za kimaendeleo zimefungwa na sheria na Katiba ya nchi
 
wale wazee wa kikao cha siri huko mjini mwanza kwaajiri ya kuweka mazingira mazuri ya ccm kushinda wameongea na watanzania,, kilamtu alikuwa akijiumauma na kusingizia publicity, ,hivi hawa watu wakienda kule usiku haiwezekani kurudi usiku bila watanzania kujua? Hii ndo maana ya kikao cha siri..

Mr. Gachuma anasema hakuwepo lakini hajasema alikuwa wapi, na kwenye barua yupo iliyosainiwa na mwanza municipal council director mr. Wilson kabwe,,
ridhwani anasema ahukwepo akitoa sababu nyingi zisizo aminika
rostam azizi anasema alikuwa south afrika,, akiwadanganya wananchi kuwa yeye ni mtu wa safari wakati kipindi hicho kilikuwa cha lala salama kwenye kampeni,, na kwenye barua nayeye yupo
lakini katika |woote walioongea kikwete hajaongea kwasababu anaona aibu ile barua inaonesha kila kitu...

Watanzania hatudanganyiki kwasababu kilicho andikwa mule ndicho kilicho fanyika lakini mulishindwa tu kufauli missio yao kwasababu watanzania wameamua kubadilika sasa
kikwete ndugu yangu muonee huruma amechoka maana nasikia jana amekesha akicheza kiduku kusherehekea uchakachuaji.
 
well hii barua sawa lakini naitilia shaka kwa upande fulani, itakuwaje iandikwe wazi namna hiyo wakati inajulikana ni siri kubwa? sitaki kuamini kuwa tunao viongozi bogus namna hii hata kutenda kosa wanakosea tena!
.

Kwani unawaona wahaini hao kuwa ni watu makini? Mipango yao mingi ya wizi wa kura itajulikana na kuanikwa hadharani na hapo ndipo utajua kuwa nchi yetu inaongozwa na watu wasio makini na ambao ni kama Watawala wa Roma ambao walipoambiwa kuwa utawala wao unaanguka badala ya kunyanyuka na kuchukua hatua wengi wao walipuuza kauli hizo na kujitumbukiza kwenye anasa na matanuzi ya ajabu. Pale watumwa na watumishi wao wa ndani walipowafukuza kwenye makao yao hawakuamini kuwa himaya yao ilikuwa imekwisha anguka.

Vivyo hivyo ndivyo itakuwa kwa CCM kwani muda mfupi ujao itaanguka kutokana na kuongozwa na watu wanaopuuza historia na wanaodhani kuwa kwa kuendelea kuwapuuza Watanzania huku wakitumia nguvu ya dola wataendelea kuwa madarakani. Nawaonea huruma sana kwani mwisho wao huu karibu na ukifika wengi wao watakuwa ni wapangaji wa kudumu wa Ukonga, Segerea, na sehemu kama hizo huku "mali zao" zote walizozichuma na kulimbikza hata kwa majina bandia au jamaa zitakuwa mali za Watanzania. Yote wanayoyafanya hivi sasa yanapalilia wao kufikia huko. Heri yao watakaotubu na kujiunga na upande wa haki, ukweli na uzalendo.
 
Me nadhani kuna haja ya kuundwa tume huru ya kuchunguza uchaguzi ulikuwa na mapungufu gani na watu walichangia kuwepo kwa vurugu na kuwakosesha imani wapiga kura waliokuwa wakisubili matoke yatangazwe na yakachukua muda usiokubalika machoni pa wengi hata waangalizi walilisema hilo.

Hivyo basi NEC ikubali tu kuwa ilikuwa na mapungufu tena mengi na ndio yaliyo sababisha wananchi kutokuwa na imani na matokeo yanayotajwa mpaka sasa, na hilo swala la kuchelewesha matokeo kutangazwa kweli ndio lililo wafanya wananchi kujiuliza na kupoteza uvumilivu wa kusubili na kushinikiza matokeo yatangazwe kwa vurugu na kwa kuaaa kwenye malango ya manispaaa mikoani na wilayani usiku kucha

mkuu watakula hela zetu tu kwa kuunda tume,
 
Kama Dr. Slaa anaitumia barua hii kama msingi wake wa malalamiko, hapo ameshashindwa na ikienda mahakamani hii barua itamwumbua sana.

Huhitaji hata kuwa na akili kubwa kujua hiyo barua ni fake. Na ikienda mahakamani itachambuliwa kama njugu.

Ubaya wa mahakama, wakigundua umetoa barua fake, madai yako mengine yote hata yale ya maana yanatupwa.

Hili la barua hii pamoja na lile la kontaina lenye kura fake huenda Slaa alitegeshewa makusudi na wajanja ili waanze kuthibitisha ni muongo na mropokaji.

Kibaya mwandishi ametaja na sehemu walipokutana. Mtu mmoja au wawili wakiwa na alibi kuonyesha isingeliwezekana wawe Mwanza wakati huo, madai yote yanaporomoka hapo hapo.

Nilipoanza kuisoma hiyo barua tu nikwa nasema come on people.

Yaani watu wafanye kikao cha siri halafu waweke ushahidi wote kwenye barua kama vile wanataka barua ije kuwashtaki baadaye. Complete with the quorum, undeciphered and unequivocally self incriminating. We all know CCM people are not too smart, but they are not this fatally dumb either.

What kind of fool would do that ?
 
Wadau sasa Kabwe ataongea alikuwa wapi mana kwake yeye ni Mwanza wenzake wanasema walikua south , kwenye kampeni na maeneo mengine ila kwa nini wajitetee kama wanaona Dr.Slaa anawaongopea waende mahakamani ivi kwa kutumia mass media wanafikiri tunaweza kuwaelewa kwa watu wenye akili timamu hatuwezi kamwe.

Mzee Gomezi
 
Kikwete bado haja zungumza naona anatuma tu watu wake wamzungumzie,, na inamaanisha alikuwepi kwenye kikao hicho hawawengine s wanaona wakikaa kimya watakuwa wameumbuka?

kwa mfano ridhwani alionekana kabisaaaa akiingia,, Kikwete:tape: kuhusu mkutano wa siri
 
mkuu uliyemchambua Rithwaani ugreat thinker nimekukubali, ila swali la pili kwa nini iwe mwanza tu na majimbo hayo mawili na si kwingine, ndugu sensa nisaidie ktk hili tafadhali

Naomba nikujibu Ferds swali lako kuwa 'kwanini Mwanza tu'?
Ni kuwa hayo maagizo yalitolewa nchi nzima manake maagizo yake yametendeka nchi nzima. Kinachoonekana hapa Mkurugenzi wa MZA alifanya kosa kupeleka mawasiliano kwa njia ya barua. Inawezekana zipo sehemu zingine lakini zilfanyika kwa usiri mkubwa na walichukua tahadhari kubwa kuwasiliana kwa njia zingine kama simu au kukutana nao direct wahusika.

Anayesema eti barua haina hata refference Simuelewi. Unategemea barua hizi za kihalifu ziwe na kila kipengele? Hiyo ni kama barua isiyokuwa rasmi lakini ujumbe unafika.

Inawezekana hata kuwa si wote waliotajwa walikuwa MZA lakini wote wana dhima moja ya kuhakikisha mkwere anashinda kwa njia yoyote hivo kwa kuwa dhima ndo hiyo ili kutilia uzito wakatajwa watu wazito kwenye chama ili ujumbe uzingatiwe kwa uzito mkubwa.
Kwa kiasi kikubwa ni kuwa kikao kilikuwepo na waliotajwa walikuwepo ila pia inawezekana si wote ila wametumika kusisitiza umuhimu wa barua hiyo na kwa kuwa Kabwe alijua huo ndo mpango wao hakuwa na wasiwasi kuwaandika hata kama hawapo.
 
jamani hii kali japo si salama, hayo maagizo ya hiyo barua naona yote ya mekamilika, hakuna hata moja ambalo ccm hawakulitekeleza, na kali zaidi ni hilo la kuchelewesha matokea, mmmmmmh, ccm hawafai kabisaaaaaaaaa

Cha kushangaza Hayo maagizo yooote yaliyo kwenye barua yametekelezeka lakini hawakufaulu mission yao... sasa nyinyi munakana nini au mumetumwa nini?
 
Wale wazee wa kikao cha siri huko mjini mwanza kwaajiri ya kuweka mazingira mazuri ya CCM kushinda wameongea na watanzania,, kilamtu alikuwa akijiumauma na kusingizia publicity, ,hivi hawa watu wakienda kule usiku haiwezekani kurudi usiku bila Watanzania kujua? hii ndo maana ya kikao cha siri..

Mr. Gachuma anasema hakuwepo lakini hajasema alikuwa wapi, na kwenye barua yupo iliyosainiwa na Mwanza municipal Council Director Mr. Wilson Kabwe,,
Ridhwani anasema ahukwepo akitoa sababu nyingi zisizo aminika
Rostam Azizi anasema alikuwa South Afrika,, akiwadanganya wananchi kuwa yeye ni mtu wa Safari wakati kipindi hicho kilikuwa cha lala salama kwenye kampeni,, na kwenye Barua nayeye yupo
Lakini katika |Woote walioongea Kikwete hajaongea kwasababu anaona aibu ile barua inaonesha kila kitu...

Watanzania hatudanganyiki kwasababu kilicho andikwa mule ndicho kilicho fanyika lakini mulishindwa tu kufauli missio yao kwasababu watanzania wameamua kubadilika sasa

KAma kigezo ni ile barua, ww unashindwa kuitengeneza ile barua? Tujaribu kupanua mawazo. Ule si ushahidi tosha.
 
.

Kwani unawaona wahaini hao kuwa ni watu makini? Mipango yao mingi ya wizi wa kura itajulikana na kuanikwa hadharani na hapo ndipo utajua kuwa nchi yetu inaongozwa na watu wasio makini na ambao ni kama Watawala wa Roma ambao walipoambiwa kuwa utawala wao unaanguka badala ya kunyanyuka na kuchukua hatua wengi wao walipuuza kauli hizo na kujitumbukiza kwenye anasa na matanuzi ya ajabu. Pale watumwa na watumishi wao wa ndani walipowafukuza kwenye makao yao hawakuamini kuwa himaya yao ilikuwa imekwisha anguka.

Vivyo hivyo ndivyo itakuwa kwa CCM kwani muda mfupi ujao itaanguka kutokana na kuongozwa na watu wanaopuuza historia na wanaodhani kuwa kwa kuendelea kuwapuuza Watanzania huku wakitumia nguvu ya dola wataendelea kuwa madarakani. Nawaonea huruma sana kwani mwisho wao huu karibu na ukifika wengi wao watakuwa ni wapangaji wa kudumu wa Ukonga, Segerea, na sehemu kama hizo huku "mali zao" zote walizozichuma na kulimbikza hata kwa majina bandia au jamaa zitakuwa mali za Watanzania. Yote wanayoyafanya hivi sasa yanapalilia wao kufikia huko. Heri yao watakaotubu na kujiunga na upande wa haki, ukweli na uzalendo.

Naamini Dr Slaa hawezi kufanya kosa, kuitumia hiyo barua kama kielelezo. Hizo ni mbinu chafu tu.
 
Najua hii haina uhusiano na maudhui nzuri na muhimu hii hapa, lakini nitaisema kwa vile mimi ni mkereketwa wa hii lugha yetu Kiswahili. Mzee Silver 25 neno ni kuhudhuRia na siyo Lia. Nadhani umefika wakati sasa wa kuwa tough na lugha otherwise hakuna mtu atayekuja Tanzania kujifunza Kiswahili chetu kibovu. Inakuwaje tunapozungumza Kiingereza hatu 'confuse' baina ya R na L, lakini tunafanya hivyo katika Kiswahili? Kweli Mtazania anaweza kusema 'vely lale' (very rare)?!!!!!!
 
Watanzania wameshachoka na CCM ila wanalazimisha tu,, na siku tukiamua kufanya mabadiliko ya lazima.. patachimbia hapa bongo..
 
Mmmh jamani mpaka mnanitisha kweli jf inanipa elimu ambayo ckuipata hii nchi inakokwenda damu lazma imwagke kwel slaa akurupuki
 
Mmmh jamani mpaka mnanitisha kweli jf inanipa elimu ambayo ckuipata hii nchi inakokwenda damu lazma imwagke kwel slaa akurupuki
 
Back
Top Bottom