Walimu watangaza mgomo nchi nzima

John W. Mlacha

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
3,504
1,341
Walimu watangaza mgomo nchi nzima
Send to a friend
Thursday, 01 December 2011 20:42
0digg

mukoba-gratian-top.jpg
Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam jana , kuhusu mgomo wa walimu nchi nzima utakaoanza mwezi Januari kama Serikali haitatimiza makubaliano yaliyofikiwa ya kuwalipa madai yao. Picha na Venance Nestory

Raymond Kaminyoge
CHAMA Cha Walimu Tanzania (CWT), kimetangaza mgomo wa walimu nchi nzima kuanzia Januari mwakani ikiwa ni hatua ya kuishinikiza Serikali iwalipe walimu deni la malimbikizo ya stahili zao mbalimbali, linalofikia Sh49.6 bilioni.

Hatua hiyo imekuja baada ya Serikali kushindwa kutimiza ahadi yake ya kuanza kuwalipa walimu fedha hizo tangu Novemba mwaka huu. Rais wa CWT, Gratian Mukoba alisema jana jijini Dar es Salaam alipozungumza na wandishi wa habari kuwa Serikali iliahidi kuwalipa walimu Novemba hadi Desemba mwaka huu ili kumaliza deni hilo.

“Natangaza kuwa shule zitakapofunguliwa mwezi Januari 2012, sisi walimu tutaendelea kuwa likizo mpaka kero zetu zitakapotatuliwa,” alisema Mukoba. Alisema tangu Juni mwaka huu, CWT na Serikali wamekuwa na vikao kadhaa kuhusu madai hayo na ikafikia uamuzi wa kuwalipa walimu katika kipindi cha miezi miwili ambayo ni Novemba na Desemba mwaka huu.

“Kumbe Serikali haikuwa na nia ya kweli kutaka kutulipa, waliona tunaweza kugoma katika kipindi cha mitihani ya taifa wakatudanganya,” alisema. Alisema kwa kuwa Serikali haina nia ya dhati katika kulipa madai hayo, wameamua kufikia uamuzi wa kutoendelea kufundisha.

Mukoba alisema wakati mishahara na posho za wabunge zikizidi kuongezeka, walimu wanashindwa kulipwa madai yao ya msingi. “Tunawaomba wazazi watuunge mkono katika mgomo huu ili watoto wenu wapate elimu sahihi,” alisema Mukoba. Kwa mujibu wa Mukoba, madai hayo yanayowahusu zaidi ya walimu 3,000 ni ya kuanzia mwaka 2008.

Alisema kero nyingine inayowafanya walimu wagome ni waraka kandamizi uliotolewa na Serikali mwaka 2007 unaowashusha vyeo walimu wanaojiendeleza kielimu. “Serikali ilikubali kuufuta waraka huo baada ya kuridhika kwamba ulikuwa unawakandamiza walimu, lakini hadi sasa unaendelea kutumika, haujafutwa,” alisema. Mukoba alisema waraka huo umelenga kuwakatisha tamaa walimu ili wasijiendeleze kielimu.

Aidha, Mukoba alisema walimu wanakaa kwa muda mrefu bila kupandishwa vyeo ingawa wanastahili kulingana na sifa zao. “Walimu tumekosa nini, kwa nini kilio chetu hakisikiki na Serikali? Iweje tunadanganywa kila siku? Sasa ni lazima tuchukue hatua,” alisema Mukoba. Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawamba hakupatikana jana kuzungumzia tishio hilo la mgomo baada ya simu yake ya mkononi kutopatikana kabisa.
 
Tabaka kubla linalonyonywa huku fisi wachache pale mjengoni dodoma wakijilipa mabilioni
 
Viongozi wa chama cha walimu ni wanafiki wakubwa.Hamna uwezo kufanya maamuzi magumu.serikali hii legelege inayomlipa mbunge kwa siku sawa na mshahara wa mwalimu graduate wa mwezi1.kumbukeni kuwa hata kama hayo mabilioni yatalipwa bado ni kazi bure.mfano hapa mwanza jiji walimu zaidi ya 1,000 waliopanda madaraja mwaka mmoja na nusu uliopita bado hawajarekebishiwa mishahara.Hii ina maana kuwa ktk zoezi hili hawatalipwa malimbikizo yao kwa kua mishahara yao haijarekebishwa.Hii ni kwamba leo selikali km watalipa bil 40,watakuta kesho wanadaiwa bil100. Ni ajabu kwa raisi wa nchi kulidanganya Taifa kuwa kuwa suala la malimbikizo kwa watumishi wa umma halitatokea tena.kwa upungufu wa mishahara walimu wanalazimika kukopa kny mabenki si kw lengo la kujenga bali kufidia mapungufu ya mshahara.kibaya zaidi ili upate mkopo ni lazima uhonge 50,000 tabia hii iko ktk tawi la Nmb kenyata usipotoa utazungushwa zaidi ya miezi 2 kwani kwa hp Mza unaruhusiwa kukopa nmb tu
 
anatafuta hela ya kula tu huyu
sheria za kuanzisha mgomo anazijua je amezifuata au anatafuta kujitangaza
CWT siwaamni ndiyo maana Kigoma walitaka kujitoa
 
naona anataka kupata umashuhuri kwani amesikia madai yao yanashughulikiwa ndio anapiga kelele za mgomo, huyu ni kibaraka wa serikali nadhani imefika wakati walimu waanze kimfukuza kwenye cheo hiki, anaendesha chama cha walimu kama CCM
 
Teachers diserves no pay as a price for their irresponsibity, as they don't teach sons a lesson that there is no hope in green and yellow...

Shikaaaamoooooo! Mwalimu

Natania tu Sir
 
Hawana uwezo wa kugoma hawa....wanatishia kujamba wakati wana tumbo la kuhara. Hw comes umwambie mwl wa primary school mwenye div 4 ya point 28 agome ataenda wapi? Afadhali wenye diploma na degrees wanaweza coz wanaweza kwnda private bt wao ni wachache hawataweza kuongoza mgomo....so i ts better wakae kimya!
 
hawa nao, kila siku mgomo mgomo, muda ukifika utasikia ooooooooh, tumeahirisha. Mimi nadhan njai nzuri ya mgomo ni kutofundisha tu badala ya kutoingia darasani kwani matokeo ya njia hii ndo serikali itatia akili
 
....so i ts better wakae kimya!

Mi nadhani wafundishe topic za ahera, itasaidia serikali kuamka pindi idadi ya watakaofeli iongezeke kushinda ya mwaka juzi. Hili litasaidia kuitia akili serikali adabu.
 
ndo take home ya mwalimu, askari polisi, magereza, na idara nyingine kibao kama malipo ya kazi yao ya mwezi mzima
Halafu watu wanapowatetea kitu chenye maslahi kwao(POLISI),wanawapiga mabomu na maji ya kuwasha.Mi Polisi ya Tanzania MIPUUZI sana.
 
Back
Top Bottom