Walimu watangaza mgomo nchi nzima

Vitisho vya nini, si mlete vitendo tuvione. Mnapiga mkwara kwa sababu mnajua hamuwezi kugoma.
 
Pamoja na kwamba nyumbu ni wengi sana mbugani, ni miujiza nyumbu hao kuungana kupambana na Simba!
 
Teh teh! walimu hawa naowafahamu ndo wagome? Teh teh! Muda ukifika mara utasikia "mi za kwangu nimelipwa kwa hiyo sina haja ya kugoma",wengine utasikia "mi nimebakiza miaka mitano kustaafu kwa hiyo sina haja ya kugoma,mwingine ni UPE kwa hiyo anaona kama ni fadhira kuwa na hiyo kazi.WALIMU WA TANZANIA KUGOMA HAIWEZEKANI!!!!
 
Walimu watangaza mgomo nchi nzima Send to a friend
Thursday, 01 December 2011 20:42
0diggsdigg

Raymond Kaminyoge
CHAMA Cha Walimu Tanzania (CWT), kimetangaza mgomo wa walimu nchi nzima kuanzia Januari mwakani ikiwa ni hatua ya kuishinikiza Serikali iwalipe walimu deni la malimbikizo ya stahili zao mbalimbali, linalofikia Sh49.6 bilioni.

Hatua hiyo imekuja baada ya Serikali kushindwa kutimiza ahadi yake ya kuanza kuwalipa walimu fedha hizo tangu Novemba mwaka huu. Rais wa CWT, Gratian Mukoba alisema jana jijini Dar es Salaam alipozungumza na wandishi wa habari kuwa Serikali iliahidi kuwalipa walimu Novemba hadi Desemba mwaka huu ili kumaliza deni hilo.

“Natangaza kuwa shule zitakapofunguliwa mwezi Januari 2012, sisi walimu tutaendelea kuwa likizo mpaka kero zetu zitakapotatuliwa,” alisema Mukoba. Alisema tangu Juni mwaka huu, CWT na Serikali wamekuwa na vikao kadhaa kuhusu madai hayo na ikafikia uamuzi wa kuwalipa walimu katika kipindi cha miezi miwili ambayo ni Novemba na Desemba mwaka huu.

“Kumbe Serikali haikuwa na nia ya kweli kutaka kutulipa, waliona tunaweza kugoma katika kipindi cha mitihani ya taifa wakatudanganya,” alisema. Alisema kwa kuwa Serikali haina nia ya dhati katika kulipa madai hayo, wameamua kufikia uamuzi wa kutoendelea kufundisha.

Mukoba alisema wakati mishahara na posho za wabunge zikizidi kuongezeka, walimu wanashindwa kulipwa madai yao ya msingi. “Tunawaomba wazazi watuunge mkono katika mgomo huu ili watoto wenu wapate elimu sahihi,” alisema Mukoba. Kwa mujibu wa Mukoba, madai hayo yanayowahusu zaidi ya walimu 3,000 ni ya kuanzia mwaka 2008.

Alisema kero nyingine inayowafanya walimu wagome ni waraka kandamizi uliotolewa na Serikali mwaka 2007 unaowashusha vyeo walimu wanaojiendeleza kielimu. “Serikali ilikubali kuufuta waraka huo baada ya kuridhika kwamba ulikuwa unawakandamiza walimu, lakini hadi sasa unaendelea kutumika, haujafutwa,” alisema. Mukoba alisema waraka huo umelenga kuwakatisha tamaa walimu ili wasijiendeleze kielimu.

Aidha, Mukoba alisema walimu wanakaa kwa muda mrefu bila kupandishwa vyeo ingawa wanastahili kulingana na sifa zao. “Walimu tumekosa nini, kwa nini kilio chetu hakisikiki na Serikali? Iweje tunadanganywa kila siku? Sasa ni lazima tuchukue hatua,” alisema Mukoba. Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawamba hakupatikana jana kuzungumzia tishio hilo la mgomo baada ya simu yake ya mkononi kutopatikana kabisa.
 
Hao walimu bure kabisa. Hizo porojo tumezisikia mara alfu lela ulela. Sit back and get your beer.
 
si mnavuna mlichopanda?. Nyie ndio mnaoshiriki kuiba kura zetu ili kuwaweka mafisadi madarakani sasa mnalalama nini? Mlipopanda bangi mlitegemea kuvuna mchicha?
hii nimeipenda kwa maana walimu hasa wa kike huwa wanakiherehere sana kushabikia chama tawala eti wakidai kinaongozwa na hendisome boy. Sasa kama mnataka ukombozi wa kweli achaneni na tabia yenu ya kuchakachua kura zetu na kuifanya ccm kushinda. Saa ya ukombozi ni sasa.
 
Waende zao waoga wakubwa hao, yaani wananiboa kwli kla sku hadth ile ile, wana ngvu kubwa likn waoga kma nini, wanaweza kbsa kua wa kwanza kfnya mapndzi kwnye nch hii na ss 2fuate, wakaendlee kshka chaki tu huko, mtu mzma unaogoopa
 
Wamezoeleka kwa haya matangazo yao ya kila mara with no effects,always they are not serious
 
Wacheni kuwadharau walimu nyie au ww na kiproffesional chako 'jina tu 'unaona wengine hawafai.hata kama walim ni maköndoo ila msiwanyanyase waalimu! ndio maana Taifa hili haliendelei maana mnadharau haki za watu wenye kima cha chini au wanyonge hiyo ni LAANA KWA TAIFA ambao mchango wao ni mkubwa kwa Taifa.SHAME ON ANY JF MEMBER ambaye anawadharau walim! i respect teachers!
 
mukoba mnafiki tu anataka aitwe kwenye meza ya makubaliano akomae wampe cha juu asitishe mgomo. HAKUNA MGOMO KWA WALIMU,
 
Back
Top Bottom