Walimu wanafelisha, madaktari watafanya nini?

Mess

JF-Expert Member
Mar 2, 2009
661
181
Jamani mgomo baridi unaoendelea wa walimu impact zake kila mmoja ameziona kwenye elimu ya Tanzania kwa sasa baada ya serikali kutumia mabavu. Swali langu kama madaktari wataamua kurudi kazini na kuanzisha mgomo baridi matokeo yake yatakuwa nini?

My opinion: tuungane na madaktari ili wakirudi suluhu ya kweli iwe imepatikana watanzania wenzangu.
 
Jibu ni rahisi; mgomo baridi wa madaktari ni watu kutopata huduma inayostahili - hivyo ni vifo!
Serikali inachoangalia ni kufaulu kisiasa kuwarudisha kazini bila ya kuangalia madhara yake.Ni muhimu kwa serikali kuweka mazingira yanayostahili siyo kusema kazi zingine ni za wito hali ya kuwa wao ktk siasa wanajineemesha tu!
Serikali ichukue hatua stahiki kumaliza kero za watumishi wa umma.
 
Jamani mgomo baridi unaoendelea wa walimu impact zake kila mmoja ameziona kwenye elimu ya Tanzania kwa sasa baada ya serikali kutumia mabavu. Swali langu kama madaktari wataamua kurudi kazini na kuanzisha mgomo baridi matokeo yake yatakuwa nini?

My opinion: tuungane na madaktari ili wakirudi suluhu ya kweli iwe imepatikana watanzania wenzangu.

Walimu wanapokuwa na mgomo baridi ni dhahiri hawatafundisha na matokeo yake wanafunzi wengi watashindwa mitihani yao. Hivyo hivyo madaktari wanapoanza mgomo baridi baada ya serikali kutumia nguvu bila akili katika kutatua matatizo yao, tutarajie vifo vingi zaidi kutokea katika hospitali zote za nchi hii. ... Hawatatibu wagonjwa ipasavyo. Watatimiza wajibu wa bosi wao anayewataka wawepo vituo vyao vya kazi lakini wagonjwa hawapewa matibu sitahiki kabisa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Naunga mkono mgomo wa madaktari mpaka serikali ijirekebishe ...
 
Kibaya zaidi ni kwamba, wananchi ambao ndio wateja wakuu wa hospitali zetu(tabaka tawala/wanasiasa wao Indiaaaaaa!) wamekaa tuli, utadhani hawaathiriki na mgomo huu. Tumerogwa? Tumetupiwa majini? Tumelishwa limbwata? Au sie ni wagonjwa wa afya ya akili? Haiwezekani ndugu yako, mkeo, mmeo, mwanao, etc afariki kwa kukosa huduma eti wewe unabaki kulalamika tu! Mh. Pinda anaongea kwa upande mmoja usipo changanya na zakwako utaona Drs wakorofi lakini ukweli ni kuwa Drs wana hoja za msingi isipokuwa zimepelekwa pasipo stahali <mwanasiasa> Chukua hatua stahiki!
 
Back
Top Bottom