Walimu waliokataa kuunga mkono wenzao katika mgomo hawa hapa!

Olesambai

Member
Jul 31, 2012
39
4
Katika utafiti nilioufanya kuanzia Julai 31 hadi sasa nimegundua makundi matatu ya walimu waliokataa kuunga mkono mgomo na sababu zao. KUNDI la kwanza ni la walimu walioajiriwa Februari 2012. Hawa wanaogopa kugoma kwa sababu wengi wao bado hawana uzoefu na bado si wanachama wa CWT. KUNDI la pili ni la wale wanaokaribia kustaafu. Hawa wanahofia kupoteza mafao ya kustaafu(pension) endapo serikali itawafukuza waliogoma. KUNDI la tatu ni la wale wanaopandishwa vyeo kiholela. Hawa wanatafuta kupanda madaraja hivyo mishahara ya kuongezeka.
 
Ni sawa kuna kundi lingine la baadhi yao kwenda shuleni wakifikiri kuwa watachaguliwa kwenye sensa. Hata hivyo hapa shuleni kwangu walimu wanaokaribia kustafu wamekuwa wajasiri sana kwa vile tu wanajitambua. Kuna mwalimu jirani yangu amebakiza mwaka mmoja tu lakini hana mpango wa kurudi nyuma katika mgomo huu. yuko tayari kufukuzwa, hata hivyo walimu wanapaswa kufahamu mgomo upo kisheria hafukuzwi mtu nchi hii ni watanzania wote. Walimu acha kutishiwa nyau. someni angalau kidogo sheria inayosimamia migomo.

Hata wanaoenda kusaini na kurudi nyumbani ni wasaliti kama wasaliti wengine, maafisa elimu wakamateni hao ndo wanafiki unasaini nini wakati hufundishi. SHAME ON THEM!
 
Naunga mkono hoja yako ya kwamba makundi hayo matatu ni wasaliti tu. Hawana mpango wala nini kwani haki stahiki zikipatikana wao hawatahusika? Waache mambo ya kujipendekeza!
 
Ni halali waalimu walio kataa kuunga mkono mgomo. Kila njiwa huruka kwa bawa lake mwenyewe. tusifuate mkumbo. wengine kesho wanahamia ofisi nyingine!! shauri yao wanao goma.
 
mgomo wa walimu haupimwi kwa kwenda au kutokwena kazini pekee. mgomo unaanzia rohoni na kisha katika akili hatimaye inakuwa kama imani. cha msingi ni kuongea na walimu vizuri na kwapa hali halisi si maneno ya hovyo hovyo ubabe na vitisho. teaching is really not a mechanical work like digging or sweeping, it is a work that is deep rooteted inside somebody: more psychological, philosophical and to some extent religious. ni sawa na yaya ukimpuuza naye atampuuza mwanao naye mtoto aweza kukua kiajabuajabu kama yaya anapuuzwa. walimu wamegubikwa na umasikini mkubwa na dharau miongoni mwa watumishi wa umma. mtu huingia kazi hii kama last solution. THE FUNDAMETAL QUESTION MUST BE " KWA NINI WALIMU HAWANA HADHI SASA NA NJIA GANI INAWEZA KUTUMIWA KUREJESHA HADHI YA UALIMU?" MTU ANAYEPENDA TAIFA HILI NI LAZIMA AJUE KUWA UALIMU NI MUHIMU SANA KUSHAPE TAIFA LA SASA NA LA KESHO!
 
Ni halali waalimu walio kataa kuunga mkono mgomo. Kila njiwa huruka kwa bawa lake mwenyewe. tusifuate mkumbo. wengine kesho wanahamia ofisi nyingine!! shauri yao wanao goma.

Inaonesha wewe ni mmoja wa hao wasaliti... Jitambue!
 
Ni halali waalimu walio kataa kuunga mkono mgomo. Kila njiwa huruka kwa bawa lake mwenyewe. tusifuate mkumbo. wengine kesho wanahamia ofisi nyingine!! shauri yao wanao goma.
Asee wewe unaonekana kutumia kichwa chako kufuga nywele tu, emancipate your self from mental slavery
 
Hakuna wa kuwakomboa walimu zaidi ya walimu wenyewe. But politician bana wanaharibu kabisa tasinia hii ya ualimu.
 
Wengine hamjui walimu wanapata mishahara kiwango kipi.jamani ni aibu.mke wangu mshahara wote ni nauli tu kwa mwezi.kaamua akae nyumbani hata akifukuzwa sawa tu.tujadili kwa kuangalia uhalisia.
 
Mkuu umesahau wake za wakuu wa wilaya.
Hili ni kundi kubwa tu la wake wa viongozi wa serikali mkoani na wilayani. Mfano Mkuu wa Mkoa/Wilaya, Afisa tawala Mkoa/Wilaya, Maafisa Elimu/Kilimo/Biashara wa Mikoa/Wilaya na wateule wengine. Hili kundi linaathiri hata walimu wengine kwenye hizo shule na ninadhani huwa hawana madai ya muda mrefu maana waume zao huwashughulikia kwa kutumia madaraka yao.
 
Dawa ya migomo ni kushusha mishahara ya wabunge kwa asilimia 55 ,hili linawezekana ikiwa kutaitishwa mgomo wa Nchi nzima , mbunge kulipwa milioni 15 kwa mwezi sio mchezo,wakati mwalimu mshahara wake kwa mbinde !atakubali nani ? Wacha wabunge waongezewe mishahara ili wafundishe mashule.
 
Ilo kundi la kwanza---- hapana nduguyangu! Tena hao ndio vichaa nusu kwa sasa na mimi mmoja wao.
 
Back
Top Bottom