Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,194
- 4,114
Baada ya kuripotiwa kwa taarifa ya walimu wa shule ya msingi Nyansalala iliyopo kata ya Bukondo Halmashauri ya wilaya ya Geita kufanya kazi wakiwa wamekaa chini kwa madai ya kunyang’anywa madawati waliyokuwa wanatumia kama mbadala wa meza na viti Mkuu wa wa wilaya ya Geita Cornel Magembe amefika shuleni hapo na kusema kuwa changamoto iliyokuwepo tayari imetatuliwa na Shule hiyo imepokea viti Nane na meza nane kwaajili ya walimu wa Shule hiyo.
Akizungumza na Kurasa Mkuu wa wilaya ya Geita Cornel Magembe amesema kilichotokea kati ya mkuu wa shule na Afisa mtendaji wa kijiji ni kutoelewana lakini tayari shule hiyo imepokea viti na meza kwaajili ya matumizi ya walimu wa shule hiyo.
“Changamoto iliyotokea nikutoelewana tu siku hiyo iliaminika kuwa viti vilivyokuwa vimetengenezwa kwaajili ya walimu vilikuwa ndo vinaletwa wakati viti vile vinakuja kutoka kwa fundi walimu nao wakaelekezwa kwamba watoe zile meza walizokuwa wanatumia ili wapeleke kwa wanafunzi kwasababu wanafunzi walikuwa na upungufu wa madawati kwaiyo mpaka sasa tunavyozungumza viti na meza vililetwa siku hiyo na walimu wapo wanavitumia” -CORNEL MAGEMBE-Mkuu wa wilaya ya Geita.