Madame S
JF-Expert Member
- Mar 4, 2015
- 17,172
- 34,311
Nawasalimia
Kuna jambo leo limeniumiza mno moyo na kichwa changu kwa mawazo
Kisa kipo hivi
Leo kwetu huku ni mvua tangu jana usiku, kulipokucha nilimwandaa mwanangu kwenda shule, sio mbali na eneo tunaloishi. Baada ya kuona muda unaenda mtoto harudi ndio nikakumbuka mvua imesababisha nikajiandaa kumfuata hapo shuleni kwao, nilipofika nikakuta wapo maskini na mwalimu wao wanasubiri wazazi waje wawachukue, nikakuta ugomvi mtoto mmoja ambae namjua amemuuma kwa meno mwenzie huku akililia chupa ya maji ya mwanangu. Ni kama mwalimu wao amezizoea vurugu hivo alikuwa ametulia tuli kitini anachat
Nilipoingia na kuukuta ugomvi ule nikaamulia kwa kuwapokonya ile chupa, mtoto alieumwa na mwenzie akawa analia, tukasalimiana na mwalimu pale nikawa nambembeleza mtoto anayelia akinionesha alipoumwa nikamuuliza nani kakuuma akanionesha moyo wangu ulipasuka kwa woga na presha yule mtoto wazazi wake hawako vizuri kiafya namaanisha ni waathirika na inasemekana na mtoto wao huyo pia ameukwaa.
Nilichokifanya nikamuita mwalimu pembeni, nikamuuliza unaijua hali halisi ya huyu mtoto? mwalimu akakataa, nikamuuliza alivyoletwa huyu mtoto mliambiwa chohote kuhusu afya yake pia akakataa ikabidi nimueleze hali halisi.
Walimu mnaofundisha hizi shule za awali jamani muwe makini, tunajua mnachoka na vurugu za hao kina junior na dada zao ila muwe macho masaa yote nimeogopa nawaza ingekuwa mwanangu ameumwa vile japo sijaona kama kamchubua lakini tahadhari ni bora zaidi ingekuaje? na wazazi ni bora ukamuita mwalimu pembeni ukamueleza hali yako ajue namna ya kuishi na huyo mtoto na kuwasaidia wenzie, hiki kitu leo kimenifikirisha sana nimejaribu kuwaza ni shule ngapi watoto wa hivi wapo, alichonambia mwalimu pia ni wazazi hatuwi wazi
Tusaidiane kuwa wazi na kulinda wengine, watoto wana michezo chungu nzima hujui bahati mbaya itatokea upande gani