Nguva Jike
JF-Expert Member
- Jan 22, 2018
- 856
- 1,006
Habari za mchana.
Kwa masikitiko makubwa walimu waliohamishwa kwenda katika shule tofauti za wilaya ya Kilindi wameuza vitu vyao vingi Ili wajihamishe wenyewe.
Hali hiyo imejitokeza baada ya jitihada zao za kupewa stahiki zao kushindwa kutekelezwa na mwajiri wao(DED-Kilindi) ambae a pia aliwaahidi kuwapa magari ya halmashauri Ili waweze kuhamisha vitu vyao.
Mpaka kufikia January pamoja na kukumbushia wapewe gari walipewa majibu kuwa mafuta hakuna.Ikumbukwe kuwa walimu wa Parakuyo Kilindi Tanga walihamishwa kutokana na shule hiyo kuwa ya Handeni baada ya mgogoro wa kimipaka kumalizwa.
Walimu hao wamenaswa wakisema Wana msongo wa mawazo huku wengine wakisema wanaidai Halmashauri ya Kilindi madai ya tangu 2016.Inasemekana kuna hatua wanataka kuchukua japo hawakusema ni hatua gani na mpaka Sasa wanaishi madarasani.So sad Kilindi.