A
Anonymous
Guest
Kinachoendelea Shule ya Sekondari Mpanda Day, Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi ni kinyume cha Sheria, Serikali imetangaza elimu bure kidato cha kwanza mpaka cha nne, lakini Wanafunzi wa kidato cha tatu wanalazimishwa kulipa pesa ya tuition ili waweze kufundishwa maada zote za kidato cha nne kipindi cha likizo.
Wanafunzi ambao hawatalipa hawapati haki ya kufundishwa hizo mada hata baada ya shule itakapofunguliwa kwa maana baada ya likizo ya Desemba.
Naomba Afisa Elimu atusaidie hili kwani Wazazi tunaumia kwa kinachoendelea, Watoto wanakosa Haki ya Msingi na pia ni wajibu wa Walimu kufundisha Wanafunzi.
Kinachoendelea Wanafunzi wameambiwa watoe pesa ya tuition ili wafundishwe kipindi cha likizo ya Desemba, ambaye hatatoa imekula kwake, maana mwezi wa kwanza hawatarudia kufundisha mada za Kidato cha Nne katika vipindi vya darasani.
Tunaomba Serikali itusaidie kwenye hili, kwani ikitokea mzazi una changamoto ya kifedha Desemba hii inamaanisha mwanao naye atayumba kielimu.