MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 10,233
- 22,316
Wakuu leo nikiwa natafakari mambo mbalimbali ya maisha nikakumbuka maisha ya shule y msingi. Zilikuwa nyakati za furaha ila pia nikahuzunika nilipowakumbuka classmates waliokuwa vizuri sana kitaaluma ila hawakubahatika kusonga mbele na kidato cha kwanza. Zilikuwa nyakati mbaya sana kwa uhaba wa shule za sekondari.
Ni nyakati ambazo kwenye darasa la wanafunzi 100 wanachaguliwa wanafunzi chini ya 10 kuendelea na elimu ya sekondari. Ninaweza sema kwa wakati ule nchi ilikuwa maskini sana hadi raia. Ni wazazi wachache walioweza kumudu gharama za private schools.
Binafsi niliambiwa na mzazi ukifeli utaenda gereji. Siku ya kutangazwa Matokeo ya mtihani wa darasa la saba ilikuwa ni siku adhimu sana iliyoteka hisia za wananchi wote. Hiyo siku kwa wengi ilikuwa kama siku ya hukumu. Jina lako lisipoonekana ubaoni basi inahesabika UMEFELI kitu ambacho kilikuwa kibaya mno. Hakukuwa na mambo ya Internet. Matokeo yalikuwa yanabandikwa kwenye ofisi za halmashauri na CCM. Yaani kuna watakaocheka na kulia.
Nakumbuka hiyo siku matokeo ya mtihani yametoka ya mwaka 1999 tulienda ofisi za manispaa Arusha tukiwa na classmates wengine kibao.
Tumefika tu nikawa wa kwanza kuona jina langu nimechaguliwa kwenda shule flani maarufu hapa nchini. Baadhi ya marafiki nao walikuwa wamechaguliwa ila kuna baadhi hawakuona majina yao. Ikawa furaha kwetu ila huzuni kuu kwa baadhi. Nakumbuka wakati tunarudi nyumbani tulipofika maeneo ya B.O.T ikabidi turudi tena manispaa kucheki upya majina baada ya wenzetu waliokuwa hawajachaguliwa kudhani hawakuangalia vizuri. Ilikuwa kimbembe.
Lakini maisha ni kitendawili. Wale marafiki zetu ambao hawakuchaguliwa kuna baadhi walijiingiza kwenye mambo ya utalii na wana makampuni yao huku wakipiga noti ndefu hatari.
Kuna wengine walipata bahati kwenda private schools na sasa hivi baadhi ni ma-Dr huko UDSM na vyuo vingine. Karibu group langu lote liko vizuri.
Shukrani kwa serikali ya CCM kuleta shule za kata zinazotoa fursa kwa vijana wote kupambania ndoto zao.
Zingekuwepo miaka ile kuna watu wengi sana wangefika mbali kielimu.