Wale mlioomba kazi ya Sensa ya Watu na Mmakazi naamini wote mlisoma kitabu cha Ngoswe

Tanzania Nchi Yetu Sote

JF-Expert Member
Mar 12, 2017
505
854
WALE MLIOOMBA KAZI YA SENSA YA WATU NA MAKAZI NAAMINI WOTE MLISOMA KITABU CHA
NGOSWE "Penzi kitovu cha uzembe" TUNAKUMBUSHANA. HATA MIMI NIMEOMBAπŸ˜πŸ˜πŸ™ˆ
πŸ‘‡πŸ½πŸ‘‡πŸ½πŸ‘‡πŸ½πŸ‘‡πŸ½πŸ‘‡πŸ½
MITOMINGI; nadhani sasa mgeni amekwisha kumaliza kula hebu nenda kaondoe vyombo

MAMA_MAZOEA; Basi fanya haraka (Mazoea anatoka, anaenda kwa Ngoswe alipo).

MAZOEA; Hodi! Hodi!

NGOSWE; Karibu

MAZOEA; (Akiingia). Ahsante. Nimekuja kuchukua vyombo.

NGOSWE; Vyombo! Kaa basi mbona unasimama kama vile hakuna viti.

MAZOEA; Nimeambiwa nifanye haraka.

NGOSWE; Mmm! Haya ngoja ninawe basi (Ngoswe ananawa kwa taratibu jicho likiwa usoni mwa Mazoea ambaye anatazama kando). Hivo mzima wee?

MAZOEA; Bee?

NGOSWE; Salama?

MAZOEA; Salama tu.

NGOSWE; Sasa ndio umekataa kukaa?

MAZOEA; (Ajidai hakusikia) Si umekwisha maliza?

NGOSWE; Bado kidogo.

MAZOEA; Basi nitakuja chukua baadaye. (Ataka kutoka)

NGOSWE; Basi nenda navyo. (Mazoea anarudi kuinama kuvichukua. (Ngoswe kwa sauti ndogo). Hivyo waitwa nani?

MAZOEA; Mie?

NGOSWE; Ndio wewe hapo kisura.

MAZOEA; (anatabasamu huku akiondoka). Mazoea!i

Simulizi ni tamu ila tulishaambiwa ya Ngoswe tumuachie Ngoswe ! ! !

πŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎ
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom