Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kushiriki kusimikwa Askofu Arusha

Naomba wakati wa kupokea ekaristi nitajie ni nani kati ya viongozi hao atapokea. Nakumbuka wakati wa kumzika Askofu Mayala wa kwanz akupokea Ekaristi alikuwa Benjamin Mkapa, akifuatiwa na Andrew Chenge.
We jamaa una kumbukumbu kali sana
 
Mkuu wamekwenda na magwanda yao?
Wakivaa magwanda ndo wanakua wakuu wa ulinzi na usalama sio?
Inamaana siku ukiomuona Sirro kavaa kiraia utakataa kwamba sio yeye?

Hapa tunazungumzia mamlaka yao na tukio wanalohudhuria, kuna mahusiano gani? Mbona hatukuwahi kuona tukio la namna hii huko nyuma?
 
Sio kweli kwamba wote ni wakatoliki.
.Kwa mfano Juma Malewa ni muislam kanisani anafata nini?
Bora akina Mabeyo na Sirro wanaweza kusingizia kwamba wanasali
Kusimkwa kwa askofu tatizo m nadhani ni swala dogo,jaribu kupitia zama za kikwete alivyokua anaudhulia kwenye kusimikwa maaskofu ,na ujaribu kuangalia waliokua wanaalikwa
 
Wakivaa magwanda ndo wanakua wakuu wa ulinzi na usalama sio?
Inamaana siku ukiomuona Sirro kavaa kiraia utakataa kwamba sio yeye?

Hapa tunazungumzia mamlaka yao na tukio wanalohudhuria, kuna mahusiano gani? Mbona hatukuwahi kuona tukio la namna hii huko nyuma?

Mkuu nimeuliza tu kama wako in full military gear au la. Mimi mwenyewe nimepata ukakasi juu ya hili jambo. Miaka yangu inayokaribia nusu karne sijawahi kuona wakuu wa vyombo vya usalama kwenye zinduzi za maaskofu!
 
Wakuu wote wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini yaani Mkuu wa Majeshi, IGP na Mkurugenzi mkuu wa Idara ya usalama wa Taifa na Magereza kushiriki kusimikwa kwa Askofu mpya Massawe wa kanisa katoliki Jimbo la Arusha ni sawa sawa au kwasababu wako na msafara wa Mh Rais huko Arusha.

Sijawahi kuliona hili katika kuwasimika maaskofu hapa nchini kwa kuhusisha wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama. Labda kama kuna reference ambayo siijui.

Majeshi yetu hayana dini.
Kwan wao hawaruhusiw kwenda Kansan? Wameenda kama waumin wengne
 
Waende wakaongeze sadaka maana JPM amedai siku hizi zimepungua sana baada ya kuwadhibiti mafisadi, ndo maana maaskofu wanapandwa hasira wakimuona Magu.
 
Wakuu wote wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini yaani Mkuu wa Majeshi, IGP na Mkurugenzi mkuu wa Idara ya usalama wa Taifa na Magereza kushiriki kusimikwa kwa Askofu mpya Massawe wa kanisa katoliki Jimbo la Arusha ni sawa sawa au kwasababu wako na msafara wa Mh Rais huko Arusha.

Sijawahi kuliona hili katika kuwasimika maaskofu hapa nchini kwa kuhusisha wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama. Labda kama kuna reference ambayo siijui.

Majeshi yetu hayana dini.
yapo mengi ambayo huyu bwana mkubwa anakosea watu wanasema wanaambiwa nyumbiz ati wanapinga kila kitu! ukweli ni kwamba raisi anapenda kuabudiwa na kutisha watu wake
 
Vitu vingine sioni hata sababu ya kusema sema hapa.kila mnachojiskia kuongea mnaongea tu ilihali unajua wazi jana Rais alikua na shughuli hapo mjini.unategemea walinzi wake na nchi kwa ujumla watamuacha peke yake?watu wengine bwana..ni hasara tu
 
Ulishawahi kuwapa mialiko hao wakuu wa vyombo vya ulinzi wakakataa kuja ulipokuwa unapewa uaskofu? Au wewe ndio ulikua unaandika barua za mialiko?
 
Wakuu wote wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini yaani Mkuu wa Majeshi, IGP na Mkurugenzi mkuu wa Idara ya usalama wa Taifa na Magereza kushiriki kusimikwa kwa Askofu mpya Massawe wa kanisa katoliki Jimbo la Arusha ni sawa sawa au kwasababu wako na msafara wa Mh Rais huko Arusha.

Sijawahi kuliona hili katika kuwasimika maaskofu hapa nchini kwa kuhusisha wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama. Labda kama kuna reference ambayo siijui.

Majeshi yetu hayana dini.
Utakuta wamerazimisha kuudhuria
 
Back
Top Bottom