Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kushiriki kusimikwa Askofu Arusha

BAKWATA ilianza kwa mtindo huu. Mbeleni kuna kataasisi kamoja tu ndio katakuwa rasmi wengine wataitwa majina mengi yenye kudhalilisha utu.
 
Biblia inasema kanisa linawahitaji zaidi wabaya kuliko wema. Kama unaamini Rais, igp na mkuu wa jeshi ni wabaya basi hapo kanisani ndipo wanapotakiwa kuwa.

sijui lawama zako za nini tena?
Yesu alisema nyumba yangu si mahali pa wanyang'anyi
 
Nilipata kuuliza humu,ni kwanini Amiri jeshi mkuu wetu anapokuwa sehemu wakuu wakuu kibao wanakuwa nyuma yake?

Hapo kakosekana wa mjengoni,Jaji msomi Prof na Mkubwa wa kazi tu.
 
Kimsingi Rais alialikwa kwenye hii sherehe na hata kitendo cha Rais kutumia wiki nzima kwa ziara ya uzinduzi-zinduzi huko Arusha ilikuwa ni opprtunity tu maana kanisa lilishamualika zamani.

Swali ni kwamba hao IGP, CDF na Usalama wamevaa kiraia au kijeshi?
 
Naomba wakati wa kupokea ekaristi nitajie ni nani kati ya viongozi hao atapokea. Nakumbuka wakati wa kumzika Askofu Mayala wa kwanz akupokea Ekaristi alikuwa Benjamin Mkapa, akifuatiwa na Andrew Chenge.
 
Wakuu wote wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini yaani Mkuu wa Majeshi,IGP,Mkurugenzi mkuu wa Idara ya usalama wa Taifa na Magereza kushiriki kusimikwa kwa Askofu mpya Massawe wa kanisa katoliki Jimbo la Arusha ni sawa sawa au kwasababu wako na msafara wa Mh Rais huko Arusha.

Sijawahi kuliona hili katika kuwasimika maaskofu hapa nchini kwa kuhusisha wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama.Labda kama kuna reference ambayo siijui.

Majeshi yetu hayana dini.
Elezea tatizo unaloliona au kisa hujawahi kuwaona?? Ni vingapi inaviona kwa mara ya kwanza ila haupati taharuki yoyote??
Nachoona hapa kama kawaida, umetanguliza siasa mbele kuliko common sense, kitu ambacho ni ishara mbaya sana kwa mtu anayetegemewa na familia yake.
 
Elezea tatizo unaloliona au kisa hujawahi kuwaona?? Ni vingapi inaviona kwa mara ya kwanza ila haupati taharuki yoyote??
Nachoona hapa kama kawaida, umetanguliza siasa mbele kuliko common sense, kitu ambacho ni ishara mbaya sana kwa mtu anayetegemewa na familia yake.
soma vizuri mada.toka lini kanisa likawapa wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama mwaliko wa kusimikwa Askofu....toa mfano
 
Mbona Tatum mara nyingi unahoji UWEPO wa Wakuu wote wa vyombo vya ULINZI NA USALAMA kwenye shughuli zinazomhusu Rais?? Wanakukera nini? au UNA AJENDA gani inayokufanya uone kuwepo kwao ni KIKWAZO KWAKO?
 
Wanachunga yasijetokea yale ya Olasiti ya kurushwa Bomu kanisani na kusababisha vifo na vilema
 
Back
Top Bottom