The Khoisan
JF-Expert Member
- Jun 5, 2007
- 15,394
- 12,978
Hivi kazi ya wakuu wa mikoa ni nini??
Maswali yanayonijia
1. Hivi gharama za kuwahamisha wote hao ni kiasi gani??? (Pesa za mlala hoi)
Machibya from Mara to Morogoro na Kalembo ametoka Moro kwenda Tanga
Mimi nilidhani wale vilaza wote wanapigwa chini kumbe ni mchezo ule wa ku-recycle!! Yetu macho
Namjua huyo mama in personal ni mchemfu haswa....hafai hata kuwa mwenyekiti wa kitongoji....
Uteuzi huo inaelekea kabisa unalenga kutafuta kura mwaka 2010. Waliobadilishwa mikoa wanatakiwa kuwa karibu na majimbo watakayogombea ili waweze kushinda ifikapo 2010. Lakini pia, ili waweze kumsaidia Rais kupata kura za kutosha.
- Lukuvi, alikosea mahesabu tu na kum-support Sumaye kwa siri kwenye urais, otherwise ni Lowassa to the teeth, na Muungwana hajawahi kumsamehe hii ni njia tu ya kumtolea nje next!
- Na kama unaelewa vizuri huu upanguzi ni kupunguza nguvu za Lowassa tu na 2010, ukiwa Dodoma unakuwa na nguvu ya ajabu sana kuliko Dar as far as uchaguzi is concerned, tuweni makini na uchambuzi wa siasa za taifa letu.
FMES
Mr. zero
Gharama ni kama ifuatavyo:
Subsistence Allowance Mr & Mrs X 80,000.00 X 14dys= 2,240,000.00
+ watoto 4 X 40,000.00 X 14dys= 2,240,000.00
- Disturbance Allowance 823,000
- Kusafirisha mizigo = 2,000,000/=
- Night Allowance kwenda kuripoti na kurudi kufunga mizigo kwa Mhe. 80,000.00 X 14
Days= 1,120,000.00
Posho ya dereva Dereva 45,000.00 X 14= 630,000.00
Wastani wa Mafuta kwa anayetoka Ruvuma kwenda Kilimanjaro Lita 540 X 1,500.00 kwa lita = 810,000.00
Gharama ya kusafirisha gari binafsi kama unalo 700,000.00
JUMLA KUU= 10,563,000.00 kwa Familia moja. Hapa wamehamishwa 11 zidisha mara 11 utapata 116,193,000.00
Hapo hujaletewa risiti za kuokoteza na gharama za kubadili samani za nguvu na magodoro ya nyumba ya Mhe. maana kila takachokuta atakiita kichafu. Nilisahau gharama za ukarabati wa nyumba hizo. Ni lazima zipakwe rangi au kubomoa kuta ili zifiti mahitaji ya Mkuu. Piga hesabu.Kwa wastani gharama ya ukarabati itakuwa ni Tshs. ngapi. Obviously haipungui 50,000,000.00 ukizidisha mara 11 utapata = 550,000,000.00. Mzee kazi ipo. Kwa mawazo yangu tija haipatikani kwa kuhamisha watu tu. Kama umeshindwa umeshindwa huwezi kuuja na jipya. Nimepata pia kutoka mtonyaji wangu wa unyalu kuwa Kandoro kapigwa Mwanza ili kumzuia kuanza kampeni mapema za kugombea Jimbo la Kalenga.Kama ambavyo mpiga debe wake Bw. Elaston Mbwilo alivohamishiwa Mtwara.
Ninavyojua mimi jimbo la Kalenga linaenda CHADEMA wamejipanga vizuri sana kule mgombea wao anauzika kirahisi sana, ndo maana Kandoro alianza kupeleka mabati na kujipendekeza huko....habari ndo hiyo!