Wakuu nimechanganyikiwa - daktari yupi yuko sahihi?

Mara ya mwisho, niliingia ktk period 8 july, 2013, mwezi uliofuata sikuona siku zangu.

last menstrual cycle yako kama ilikuwa tarehe 8 July 2013 hesabu zinaniambia delivery date itakuwa tarehe 15 April 2014. Kuwa mvumilivu mama ingawa kunatokea mabadiliko kidogo kutokana na mabadiliko ya siku katika mwezi. E.g mwenzi mfupi na mrefu.
 
Kama tarehe 8 ndio ilikuwa
siku ya kwanza, kwa kalenda ya google inasema due date ni 14th April
2014. Ila muone daktari kwa ushauru zaidi, sie madaktari kanjanja tusije
tukakuingiza chaka. Na ndio maana nikasema, isingekuwa issue ya planned
tarehe, ungesubiri mpaka uone dalili za mauza uza ndio
ujisogeze...

Asante Dina!
 
Last edited by a moderator:
Wote wapo sahihi kulingana namna ulivyowaeleza. Calculation ya edd huwa inavary sana na hata walioiweka walisema its not obsolete! Wanawake wengi ukiwauliza siku zao za mwisho kwenda mwezini huwa wanataja tarehe ambayo alitegemea kuona na hakuona. Hui inasogeza mwezi mmoja mbele zaidi ya yule atakayetaja exact date ambayo alianza siku zake za mwisho kabisa. Daktari au nurse asopouliza kwa umakini zaidi anajikuta ameandika tarehe ambazo sio! By the way hongera kwa kufika mpaka wiki hizo.
 
Mara ya mwisho, niliingia ktk period 8 july, 2013, mwezi uliofuata sikuona siku zangu.

Kwa tarehe hiyo mpaka sasa una 39 weeks and 3 days. That means siku yoyote unaweza kuanza uchungu. Inakubidi kuwa makini uchungu ukikuanza maana huyo daktari wako wa hicho kijiji hana mawazo ya kwamba uko term. Usicheze mbali na hospitali.
 
Kama tarehe 8 ndio ilikuwa siku ya kwanza, kwa kalenda ya google inasema due date ni 14th April 2014. Ila muone daktari kwa ushauru zaidi, sie madaktari kanjanja tusije tukakuingiza chaka. Na ndio maana nikasema, isingekuwa issue ya planned tarehe, ungesubiri mpaka uone dalili za mauza uza ndio ujisogeze...

Huyu anaonekana hawajajipanga na huyo mume wake. Mambo ya kubadirisha daktari siku za mwisho kabisa yamepitwa na wakati. Mtu aliyemakini atataka awe na daktari mmoja kipindi chote cha ujauzito mpaka atakapojifungua. Hii inarahisisha ufuatiliaji was mimba na maendeleo ya mama.
 
Dah....kweli tuwaheshima na kuwapenda mama zetu. Watoto wanne wote mama amerisk maisha yake na kukubali kisu. Hivi georgina george wataalamu wote wameridhika kwamba kamwe hutaweza kujifungua kwa njia ya kawaida? hebu mkabidhi mwenye enzi mungu kwa huyu kwani yeye kila jambo linawezekana. Wana JF wenzangu hebu tumuombee huyu mama kwenye sala zetu mungu ampe uwezo wa kujifungua kwa njia ya kawaida na salama. Kisu mara nne sio masihara
 
Last edited by a moderator:
Hongera kwa hatua uliyofikia. Kwa tarehe ya mwisho ulipoona hedhi uliyoitoa yaani tar8 July 2013, daktari wa kwanza yupo sahihi ijapokuwa kunaweza kuwa na variation ya siku chache. Lakini kwa ushauri wangu fanya maandalizi yote muhimu mapema na nenda clinic iliyo karibu mara unapoona kuna mabadiliko ya aina yoyote ile. Mungu akutangulie katika hili.
 
Mwenzangu...halafu kuishia na kuambiwa discrepancy ya mwezi mzima! Mbaya zaidi kama mwishoni ameishia kwenye huduma zisizo na uhakika sana....na jinsi issue za uzazi zisivyo lelemama.
 
Hiyo sala ifanye peke yako aise. Ingekuwa ni mimba ya pili ningekusaidia. Scar mara tatu aafu tuanze kumjaribu Mungu? Mimi namuombea ampate mtoto wake na yeye wakiwa wazima.

But, wonders never end!! Don't wait for wonders
 
Last edited by a moderator:
Mwenzangu...halafu kuishia na kuambiwa discrepancy ya mwezi mzima! Mbaya zaidi kama mwishoni ameishia kwenye huduma zisizo na uhakika sana....na jinsi issue za uzazi zisivyo lelemama.

Smart woman akishajijua ni mjamzito tu yuko tayari kutumia gharama yoyote ile ili mradi safari ya yeye na kijacho iwe salama. Mwenzenu kaamua kurudi kwa mama yake.
 
Huyu anaonekana hawajajipanga na huyo mume wake. Mambo ya kubadirisha daktari siku za mwisho kabisa yamepitwa na wakati. Mtu aliyemakini atataka awe na daktari mmoja kipindi chote cha ujauzito mpaka atakapojifungua. Hii inarahisisha ufuatiliaji was mimba na maendeleo ya mama.

Mkuu Nyalotsi, kadi ya clinic inaonyesha history yote ya attendance yangu pamoja na vipimo vya Utra-Sound, sioni kama kuna tatizo sana.
 
Last edited by a moderator:
Salaam Zenu Wakuu!

Mimi ni mama wa watoto watatu, wote wa kike. Watoto wote hao nilijifungua kwa njia ya operation. Wakati wa mimba ya kwanza niliambiwa na Daktari kuwa siwezi kujifungua kwa njia ya kawaida hivyo nilifanyiwa Emergency Caesarian ili kunusuru maisha yangu pamoja na mtoto. Mimba mbili zilizofuata nilifanyiwa a Planned Caesarian. Pamoja na watoto wote watatu kuzaliwa kabla ya muda (premature), thank Lord, watoto wote wamekua vizuri wakiwa na afya njema.
First born yuko Kidato cha 2 mwaka huu, wa pili Class 5 na watatu yuko Chekechea.

Mwaka jana (2013) mimi & my husband tuliamua kutupa karata zetu za mwisho, japo mwenzangu mwanzoni alikataa akishauri kuwa watoto watatu wanatosha regardless of being the same gender. Nilitumia busara sana kumshauri mwenzangu kuhusu kutengeneza mtoto mwingine wa nne na wa mwisho. Lengo langu likiwa at least kubahatisha a baby boy, Lord knows!

Mnamo Aug, 2013 sikuona siku zangu, obviously nilijua kitu kimenasa!
Nisiwachoshe sana; in short lipo tatizo linalonipa wasi wasi ambalo ndilo lengo kuu la kuleta hapa jamvini thread hii.

Nimekuwa niki hudhuria clinic mara kwa mara na pia Daktari alifanya calculations zake na kunijulisha kuwa tarehe yangu ya kufanyiwa OP itakuwa 15.04.2014.
Nilipotimiza wiki ya 34 ya ujauzito wangu, niliamua kufunga safari na kwenda kwa mama yangu mzazi ili nipewe uangalizi wa karibu. Nilipofika kwa mama mzazi, baada ya siku mbili au tatu hivi nikwenda clinic (hospitali nyingine) pia Daktari wa pale naye alifanya calculations zake akitumia kadi ya clinic niliyokwenda nayo toka hospitali ya mwanzo. Huyu Daktari wa pili aliniambia kuwa nitafanyiwa OP tarehe 11.05.2014! Nilimwambia kuwa ni tarehe 15.04.2014, Daktari huyu alikataa na kuniambia kuwa yeye yuko sahihi na kwamba yule wa kwanza alikosea hesabu.

Tatizo langu: Binafsi hii variation ya siku takriban 27 kati ya hesabu za hawa madaktari wawili inanichanganya sana wakuu! Naogopa risk zitakazojitokeza endapo huyu Daktari wa pili atakuwa amekosea hesabu zake.

NINAOMBA USHAURI WENU WANA JF PAMOJA NA MADAKTARI WALIOPO HAPA JF.

Kwa hiyo ndo umekuja nishitaki humu siyo eeeh,,,Sasa nakusubir hyo cku ya OP ndo utanielewa mii nan
 
Hongera kwa hatua uliyofikia. Kwa tarehe ya mwisho ulipoona hedhi uliyoitoa yaani tar8 July 2013, daktari wa kwanza yupo sahihi ijapokuwa kunaweza kuwa na variation ya siku chache. Lakini kwa ushauri wangu fanya maandalizi yote muhimu mapema na nenda clinic iliyo karibu mara unapoona kuna mabadiliko ya aina yoyote ile. Mungu akutangulie katika hili.

Ameeen!
 
Kwa tarehe hiyo mpaka sasa una 39 weeks and 3 days. That means siku yoyote unaweza kuanza uchungu. Inakubidi kuwa makini uchungu ukikuanza maana huyo daktari wako wa hicho kijiji hana mawazo ya kwamba uko term. Usicheze mbali na hospitali.

Duuuh, mbona roho inaanza kudunda! Wiki nzima sipati usingizi hasa kuanzia saa 8 usiku hadi saa 10 alfajiri.
 
Mkuu Nyalotsi, kadi ya clinic inaonyesha history yote ya attendance yangu pamoja na vipimo vya Utra-Sound, sioni kama kuna tatizo sana.

Sisemei kuhusu hiyo tarehe na ultrasound. Discrepancy kati ya watu wawili imekuchanganya wewe wakati ungekuwa na yule uliyeanza naye usingepatwa na hali hii.
 
Last edited by a moderator:
Mara ya mwisho, niliingia ktk period 8 july, 2013, mwezi uliofuata sikuona siku zangu.

Kwa kurejea tarehe ulizotaja, mimba ulipata kwenye tarehe 22/07/2013, mimba yako sasa ina umri wa wiki 38 na tarehe tarajiwa ya kujifungua ni 14/04/2014, na inaweza kufikia hadi tarehe 28/04; hongera sana, nani kama mama?. Hesabu hii inategemea kwamba mzunguko wako wa hedhio ni wa kawaida, yaani siku 28. Kuhusu hao madakitari wawili, wewe rejea ushauri wa Mheshimiwa Rais wetu: Akili ya kuambiwa, changanya na yako!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom