Wakongwe: Uliangalia wapi Fainali ya Kombe la Dunia 1994 kati ya Brazil VS Italia

Niliangalia kwenye Kibanda-Umiza kwa Binamu yangu Deo Matengelele Visiga Kibaha. Kulikuwa na Mzee anakuja na tv na antena yake na kuonyesha mpira pale kupitia ITV.

Mashindano yale kiujumla yalikuwa bora hata kwa Cameroon ya mkongwe wa miaka 42 Roger Milla. Kulikuwa na bingwa wa kufunga magoli ya kichwa...mtu mweusi mmoja wa Sweden akiitwa Darlin.

Vya kale ni dhahabu kwakweli...
Mwamba kweli kweli Dan Martin Nataniel Dahlin huyu aliiwezesha Sweden kushika nafasi ya tatu kwenye World Cup ya 1994.

Alikuwa fundi kweli kweli.
 
Umenikumbusha. ITV zamani walikuwa wanaonyesha ligi ya Uingereza. Bure kabisa. Enzi Arsenal ikiwa na wachezaji kama kina Overmass, Tony Adams, etc...
Hata NBA pia
Ukitaka kuona marudio ublnasubiri tamasha la michezo j2 mchana
 
Hata NBA pia
Ukitaka kuona marudio ublnasubiri tamasha la michezo j2 mchana
Game za NBA zilikuwa zinaonyeshwa mchana, miaka ile Chicago Bulls na Milwaukee wapo moto sana na wale wengine Clippers.

Maisha yalikuwa tofauti sana.
 
nilikuwa mpakani, tv inayo kamata ilikuwa tv rwanda na burundi hizi itv, channel 10 na nyingine za kibongo nimekuja zifahamu baada ya kuhama mpakani
ukamshuhudia Zidane LIVE bila chenga. hapo mimi ndio kwanza hata Uso sijui kunawa
 
Wakongwe habari!
Nimepata kumbukumbu za Fainali za Kombe la Dunia mwaka 1994, wakati huo nilikuwa nipo shule ya Msingi.
Mechi za mashindano haya nilizingalia Jet Club (ilikuwa ndani ya eneo la Uwanja wa ndege wa Julius Nyerere International Airport wakati ule ulijulikana kama Uwanja wa ndege wa Dar es Salaam - Dar es Salaam International Airport.
Watu wengi waliokuwa wakiishi Kipawa na Kiwalani hapa ndio eneo la kwenda kuangalia mpira hasa kwa wale ambao walikuwa na ndugu ama marafiki wanaofanya kazi uwanja wa ndege.
Miaka ile uwanja wa ndege haukuwa na uzio wa ukuta kama ilivyo sasa.
Fainali ilipigwa Rose Bowl, katika jiji la Pasadena, California
Mechi ilichezwa kwa dakika 120 mpaka kwenye mikwaju ya penati. Brazil ikishinda kwa 3 na Italia kupata penati 2


Uliangalia mechi ya fainali ukiwa wapi?
Kombe LA KWANZA kabisa LA Dunia KUWAHI KURUSHWA na local TV channel ITV. KABLA ya HAPO ni WATU WA Masaki tu waliokuwa wnanagalia Kombe LA dunia KUPITIA Satellite dishes
Nilikuwa Manzese Tip Top
 
Zamani mpira ulikuwa unachezwa haswa, yaani ilikuwa ni full maufundi, full burudani na wachezaji wazuri walikuwepo wengi sana ila mashabiki wengi tulikuwa hatuna access ya kupata burudani hiyo, wengi tulifuatilia mechi kupitia redio tu.

Miaka hii ambayo ndio Kuna access kubwa ya kuona mechi yoyote unayoitaka, mpira mzuri mzuri nao umekuwa adimu, timu nyingi zinacheza utopolo mtupu na wachezaji mafundi wenye vipaji asilia nao wameadimika.... !!

Binafsi Huwa nina enjoy sana, kuangalia mechi za zamani hasa za world cup kuanzia 1980s mpaka 2002 hapo. Hizi mechi ndio Huwa zinakula bando langu nikiingia YouTube.
 
ukamshuhudia Zidane LIVE bila chenga. hapo mimi ndio kwanza hata Uso sijui kunawa
Ufaransa haikuwepo kwenye World Cup ya 1994; kwenye mechi za kufuza kwa maajabu akachapwa na Bulgaria na Israel.
 
Back
Top Bottom