Wakongwe: Uliangalia wapi Fainali ya Kombe la Dunia 1994 kati ya Brazil VS Italia

privity

Senior Member
Feb 6, 2020
172
603
Wakongwe habari!
Nimepata kumbukumbu za Fainali za Kombe la Dunia mwaka 1994, wakati huo nilikuwa nipo shule ya Msingi.
Mechi za mashindano haya nilizingalia Jet Club (ilikuwa ndani ya eneo la Uwanja wa ndege wa Julius Nyerere International Airport wakati ule ulijulikana kama Uwanja wa ndege wa Dar es Salaam - Dar es Salaam International Airport.
Watu wengi waliokuwa wakiishi Kipawa na Kiwalani hapa ndio eneo la kwenda kuangalia mpira hasa kwa wale ambao walikuwa na ndugu ama marafiki wanaofanya kazi uwanja wa ndege.
Miaka ile uwanja wa ndege haukuwa na uzio wa ukuta kama ilivyo sasa.
Fainali ilipigwa Rose Bowl, katika jiji la Pasadena, California
Mechi ilichezwa kwa dakika 120 mpaka kwenye mikwaju ya penati. Brazil ikishinda kwa 3 na Italia kupata penati 2

Uliangalia mechi ya fainali ukiwa wapi?
 
Nilikuwa naangalia kwa kupiga chabo kwa jirani yetu, mtaa wa Kitomondo B. Enzi hizo nikiwa nasoma pale shule ya msingi Wailes.

Nawakumbuka sana Romario na Bebeto (Brazil), Roberto Baggio (Italia), Claudio Canigia, David Ginola, Omam Biyiki wa Cameroon, Rashid Yekini wa Nigeria, na mastaa wengine kibao.
 
Nlikua vidudu ( siku hizi vinaitwa nursery) naenda shule kunywa uji huku nna daftari dogo lililogawanyishwa kati yakapatikana mawili, vivyo hivyo na penseli inavunjwa mara mbili. Nikitoka shule ni kombolela mwanzo mwisho.

Mengine yote sijui.
 
Wakongwe habari!
Nimepata kumbukumbu za Fainali za Kombe la Dunia mwaka 1994, wakati huo nilikuwa nipo shule ya Msingi.
Mechi za mashindano haya nilizingalia Jet Club (ilikuwa ndani ya eneo la Uwanja wa ndege wa Julius Nyerere International Airport wakati ule ulijulikana kama Uwanja wa ndege wa Dar es Salaam - Dar es Salaam International Airport.
Watu wengi waliokuwa wakiishi Kipawa na Kiwalani hapa ndio eneo la kwenda kuangalia mpira hasa kwa wale ambao walikuwa na ndugu ama marafiki wanaofanya kazi uwanja wa ndege.
Miaka ile uwanja wa ndege haukuwa na uzio wa ukuta kama ilivyo sasa.
Fainali ilipigwa Rose Bowl, katika jiji la Pasadena, California
Mechi ilichezwa kwa dakika 120 mpaka kwenye mikwaju ya penati. Brazil ikishinda kwa 3 na Italia kupata penati 2

Uliangalia mechi ya fainali ukiwa wapi?
Butiama Hotel Shinyanga.
 
Ikifika saa 2½ usiku unalala Hadi saa 8:00. Mechi inaanza 8½ usiku.
 
Uwanja wa Sabasaba Kilwa Rd pale ndani kulikuwa na TV kibao kwenye mabaa ITV ikionyesha na Roberto Baggio akakosa penalty.
 
Nlikua vidudu ( siku hizi vinaitwa nursery) naenda shule kunywa uji huku nna daftari dogo lililogawanyishwa kati yakapatikana mawili, vivyo hivyo na penseli inavunjwa mara mbili. Nikitoka shule ni kombolela mwanzo mwisho.

Mengine yote sijui.

Wewe utakuwa na umri sawa na Last born wetu, yeye ndio alikuwa anakwenda chekechea miaka hiyo. Alikuwa anapenda sana zile pipi za kijiti (actually ni sukari ilikaangwa). Hakukuwa na hizi Big Boom wala Ivory chocolate. Sisi wakubwa tulikuwa tunatumia pipi za Toffee au Pipi kifua.
 
Tulikua tunaziita gulbit sijui ni sawa make maneno ya enzi hizo bana kuna mahali tulizoea kupaita olofea nmekuja kuwa mzee ndo najua kumbe ilikua welfare 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom