Wakongwe, Athumani Juma Chama na Zamoyoni Mogella ...

PAGAN

JF-Expert Member
Aug 19, 2014
11,230
17,813
20229277_1597609976939251_6956923369637906127_n.jpg
 
Mkuu hiyo inanikumbusha miaka ile 1982-1986. Asubuhi ya siku ya mechi ya simba na yanga Gazeti la Uhuru (gazeti pekee la kila siku wakati huo) liliandika hivi "Ni nani atakayemdhibiti Zamoyoni Mogela leo?" Jioni ya siku hiyo Athumani juma "chama" au jogoo na golikipa wake mtata himisi kinye walipata wakati mgumu kumdhibiti Mogella aliyekuwa tishio sana anapoingia kwenye 18 ya adui. Chama alimchezea rafu ambayo ilimpasua kichwa mogela na hivyo alimaliza mchezo huo akiwa na bandeji kichwani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sifa kubwa ya Chama Jogoo ilikuwa ni Ubabe na Utemi ambapo Wachezaji wengi waliokuwa wakikutana nae au kukabana nae wengi wao kwa kujihami na kumuogopa walikuwa kila mara wakimuamkia Shikamoo Kaka Chama na Chama alikuwa hawajibu vile vile huku akiwakaba kiroho mbaya / ng'adu kwa ng'adu. Sifa kubwa ya Zamoyoni Mogella a.k.a Morgan a.k.a Golden Boy ni kuweza kufunga Magoli ya ajabu ajabu na ambayo hukuyatarajia na alikuwa haogopi msitu wa Mabeki katili kama Rafiki yake Chama Jogoo na ndiyo wawili hawa walipokutana mbungi / mchezo ulikuwa mtamu na Watu walikuwa wakienda Uwanjani kuwatizama wao tu.

Mpira ulikuwa zamani bhana siyo siku hizi tuna Wapuuzi kama akina Ibrahim Ajib. Huyu Ajib angenikuta enzi zangu nasimama half back four yangu au nacheza dimba la juu la Kukaba angenitambua kwani ningemtengua sana nyongo na angekula mno Vipepsi vyangu. Mtoto mnafiki mno huyo na mechi ya Ngao ya Jamii kuna Mtu tutampa Kazi maalum ya kuvivunjilia mbali vimiguu vyake ili asicheze tena msimu mzima na tukimkosakosa hapo tunamuendea mlingotini Pemba kummaliza kabisa Kiutamaduni na Kimila ili asiweze tena kucheza mpira.

Unyama Unyama tu!
 
Mnayowaza kwa Ajibu,pia tunawaza kuyafanya kwa Niyonzima

Narudi kijijini
 
Naomba kurekebisha kidogo mkuu... Chama hakumpasua kichwa Mogella. Ile ishu ilikuwa hivi... Mogella alianguka akiwa pale chini beki mwingine wa Yanga, Yussuf Ismael 'Bana' akiwa naviatu vyenye six-meno alitaka kumkanyaga usoni Chama akamsukuma Bana na vile viatu vikamchana Mogella kichwani. Ila Athuman Juma Chama hakumchezea rafu iliyompasua kichwa Mogella. Take It From Me.
 
Wenzao wakina Zidane sasa hivi ni makocha, wao ujuzi wanaunywea kahawa na kashata tu.
 
Kipindi hicho ndipo ulipoibuka msemo Chama na mogela yaani kama mtu anakufutilia sana unasema mbona unanikaba kama chama na mogela jina lingine aliitwa DHL
 
Mnayowaza kwa Ajibu,pia tunawaza kuyafanya kwa Niyonzima

Narudi kijijini

Basi kama ni hivyo mwaka huu mpira hautachezeka. Huyo Mtoto Ajib katudharau sana wana Simba SC hivyo hatuna namna nyingine zaidi ya kumtengua au kumtengeneza kwa Babu.

Nabaki mjini.
 
Sifa kubwa ya Chama Jogoo ilikuwa ni Ubabe na Utemi ambapo Wachezaji wengi waliokuwa wakikutana nae au kukabana nae wengi wao kwa kujihami na kumuogopa walikuwa kila mara wakimuamkia Shikamoo Kaka Chama na Chama alikuwa hawajibu vile vile huku akiwakaba kiroho mbaya / ng'adu kwa ng'adu. Sifa kubwa ya Zamoyoni Mogella a.k.a Morgan a.k.a Golden Boy ni kuweza kufunga Magoli ya ajabu ajabu na ambayo hukuyatarajia na alikuwa haogopi msitu wa Mabeki katili kama Rafiki yake Chama Jogoo na ndiyo wawili hawa walipokutana mbungi / mchezo ulikuwa mtamu na Watu walikuwa wakienda Uwanjani kuwatizama wao tu.

Mpira ulikuwa zamani bhana siyo siku hizi tuna Wapuuzi kama akina Ibrahim Ajib. Huyu Ajib angenikuta enzi zangu nasimama half back four yangu au nacheza dimba la juu la Kukaba angenitambua kwani ningemtengua sana nyongo na angekula mno Vipepsi vyangu. Mtoto mnafiki mno huyo na mechi ya Ngao ya Jamii kuna Mtu tutampa Kazi maalum ya kuvivunjilia mbali vimiguu vyake ili asicheze tena msimu mzima na tukimkosakosa hapo tunamuendea mlingotini Pemba kummaliza kabisa Kiutamaduni na Kimila ili asiweze tena kucheza mpira.

Unyama Unyama tu!
Naona mada ndani ya mada!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba kurekebisha kidogo mkuu... Chama hakumpasua kichwa Mogella. Ile ishu ilikuwa hivi... Mogella alianguka akiwa pale chini beki mwingine wa Yanga, Yussuf Ismael 'Bana' akiwa naviatu vyenye six-meno alitaka kumkanyaga usoni Chama akamsukuma Bana na vile viatu vikamchana Mogella kichwani. Ila Athuman Juma Chama hakumchezea rafu iliyompasua kichwa Mogella. Take It From Me.
Shukrani kwa kuweka sawa hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom