Wakili CHADEMA kesi ya Igunga, Peter Kibatala atoa tamko juu ya hali ya wateja wake

Huyu Mungu tunayemtumikia aipe ujasiri Mahakama kuwa na ujasiri wa kufanya maamuzi.
Tunawashukuru Mawakili wetu Peter Kibatala na Prof. Abdallah Safari, tunaomba muendelee na moyo huo mpaka haki ipatikane!

Tulianza na Mungu, Tunaendelea kuwa na Mungu, na Tutamaliza na Mungu ndugu zangu mjipe moyo tutashinda!

Mahakamani sheria tu,miujiza ya mungu ni gerezani kama ameshindwa kutoka basi hana mungu
 
Lakini nauliza ninyi mnaowatetea hawa ikibainika walimwagia tesha tindikali itakuwaje?acheni mahakama itekeleze wajibu wake maana tesha hajajimwagia tindikali,tusikose utu na huruma kwa wenzetu kissa siasa,Chadema mnasumbuliwa na ugonjwa wakuona haki ni kwa wanachadema tuu,sio sahihi hata kidogo

WW vipi tena, mahakama hajailalamikiwa hapa, Kinacho lalamikiwa ni Serikali ya CCM kulitumia jeshi la polisi vibaya dhidi ya wapinzani wao, kwa kuwabambikizia kesi za ugaidi ili tu wasipate hata dhamana." Childish political tactics"
 
Lakini nauliza ninyi mnaowatetea hawa ikibainika walimwagia tesha tindikali itakuwaje?acheni mahakama itekeleze wajibu wake maana tesha hajajimwagia tindikali,tusikose utu na huruma kwa wenzetu kissa siasa,Chadema mnasumbuliwa na ugonjwa wakuona haki ni kwa wanachadema tuu,sio sahihi hata kidogo
Kumsafirisha mtu kwa siri,ukimnyima hata haki ya kula ndio kazi ya polisi?polisi wangekuwa na nia njema ya kutoa haki kwa aliemwagiwa tindikali,wangetenda haki pia kwa watuhumiwa..jeshi la polisi linatumia ubongo uliooza unaotoa funza...wa mwigulu nchemba na wenzake....HAKUNA UTAWALA DHALIMU,KANDIMIZI, WAUWAJI AMBAO WAMEWAHI KUISHINDA NGUVU YA UMMA...watatumia risasi na dola kunyanyasa wananchi lakini mwisho wa siku dhoruba kali ya nguvu ya umma itawasambaratisha....
 
Naamini Mungu yupo upande wa CDM na daima atawapigania.

Kumbukeni wakati CUF ikiwa kweli chama cha upinzani walipata misukosuko mingi sana hadi walipofunga ndoa bubu ili kupunguzwa kasi.

Nawataka sasa mjue kuwa ukombozi si rahisi kama wengi wanavyodhani na fahamuni pia kuwa kila mtawala hapendi kutoka madarakani akicheka ....

KAZENI BUTI MAKAMANDA.....................
 
Kama Mwigulu amethubutu kudai kuwa CDM wamejitupia bomu, basi CCM watashindwaje kujimwagia tindikali?

Maneno ya siasa yanaishia majukwaani,kilewo alijua kuwa na wakili kutamsaidia asibanwe sasa amesema yaliyotokea,yanayotokea na yatakayotokea kama alijimwagia mwambie wakili aweke maelezo aliyokili kilewo
 
Kwa wakili Kibatala na Prof. Safari; Mungu awape afya njema na ujasiri kutetea haki za wanyonge, awape rehema zake kuu mzidi kuwatetea wanaoshitakiwa na serikali hii dhalimu.

WOTE TUMWOMBE MUNGU,
"Mungu wa rehema, wewe wajua yalio ndani ya mioyo yetu, kama kuna mtu anafaidika na haya , tafadhali usiache hili lipite, ulituumba tukuabudu, tukutumikie na mwisho tufike kwako mbinguni.Sasa mungu tenda tafdhali. "

Wewe tafuta laana ya mungu,badala ya kumuomba mungu amsaidie yule aliyeumizwa na kuteseka na maumivu ya tindikali unawaombea waovu wanaotesa binadamu wenzao kwa kuwamwagia tindikali,hivi ww kweli una mungu una mungu ww
 
Hiyo lana unayoiomba tayari inawatesa sana,mateso mliyomsababishia kijana wa igunga ni makali sana,hebu jaribuni hiyo tindikali kwa slaa au mbowe ili wawasimulie watakavyo jisikia

Laana isiyo na sababu haimpati mtu!! Ndio maana mmetega mitego mingi sana kwa viongozi wa chadema hakuna uliofanikiwa!! Madhambi mliyotenda na yale yaliyotendwa na baba zenu kama nawewe ni mmoja wao ndio yanayowamaliza sasa!!
 
kwanini watoroshe mtuhumiwa bila kiwataarifu mawakili zake? kwani hili linahitaji phd kujua? ni mwendelezo wa ajenda ya c.c.m ya kuwabana wapinzani ili waonekane ni magaidi ili kufutwe kwani wameshindwa kupambana na chadema kwa sera
 
Lakini nauliza ninyi mnaowatetea hawa ikibainika walimwagia tesha tindikali itakuwaje?acheni mahakama itekeleze wajibu wake maana tesha hajajimwagia tindikali,tusikose utu na huruma kwa wenzetu kissa siasa,Chadema mnasumbuliwa na ugonjwa wakuona haki ni kwa wanachadema tuu,sio sahihi hata kidogo

Tuko nyuma yao kwa maamuzi yoyote ya Mahakama! GUILTY OR INNOCENT we are behind you henry Kileo na wapiganaji wengine ulionao huko!
 
Last edited by a moderator:
laana isiyo na sababu haimpati mtu!! Ndio maana mmetega mitego mingi sana kwa viongozi wa chadema hakuna uliofanikiwa!! Madhambi mliyotenda na yale yaliyotendwa na baba zenu kama nawewe ni mmoja wao ndio yanayowamaliza sasa!!

yes. Mithali 26:2
 
Halafu mara nyingi utamuona rais wetu Kikwete anashangaa pale watu wa haki za binadamu wanampomtuhumu kuwa kuna uvunjifu wa haki za binadamu unaofanywa na serikali yake, eti wanamuonea! Hana macho/masikio ya kuona na kuelewa mambo kama haya yanayofanywa na jeshi la polisi? Mtuhumiwa anaishi mazingira haya tena mtu aliyeenda mwenyewe kituo cha polisi? Time will tell and ICC will decide!

Hata kama ameenda mwenyewe yy ni mtuhumiwa lazima ahojiwe ikibidi apitie ktk hatua muhimu ili atoe maelezo yaliyo sahihi istoshe yy ametajwa na wale waliokamatwa awali sasa unataka polisi wambebe ili iweje amehojiwa kulingana na maelezo aliyotoa mwenyewe,alidai atakula chakula kitakacholetwa na mkewe sasa ulitaka polisi wamsafilishe mkewe hadi tabora akampelekee chakula,hilo jukumu la chadema wao ndio wana maslai na kilewo
 
kingukitano hayo polisi wafanyao ni maagizo ya c.c.m ili kutafuta njia ya kudhoofisha chadema baada ya kuona inaungwa mkono bado na watu pamoja na kupewa propaganda nyingi. c.c.m sasa haiwezi siasa za jukwaani na demokrasia.walimshitaki lwakatare mwigulu aliapa mbinguni na duniani. ya igunga ni mwendelezo wa yaleyale. c.c.m inawafanya polisi wasiaminike kwani sasa hawafanyi kazi kwa kufuata sheria bali ni kufuata maelekezo ya c.c.m ili kudibiti wapinzani hasa chadema. wananchi wanajua kila kitu hata baadhi ya wanachama wa c.c.m wa chini hawapendi siasa hizi na zinawaudhi. tulianza na mungu tutamaliza na mungu
 
Mwigulu Nchemba anaelewa mbinu alizotumia kuwapanga vijana waliomwagia tindikali Musa Tesha. Na alifanya hivyo kuwadhuru watu ili ionekane ni chadema.
Mkuu tukiweka ushabiki pembeni, na ukitaka kujua kuwa Mwigulu Nchemba na CCM wanapanga mikakati mibovu, hata majuzi walipanga mkakati wa kuwaleta Wahuni kutoka Mwanza wenye mapanga, ambao wanakuwa wamejivalia magwanda ya chadema kuja kufanya vurugu kwenye uchaguzi wa Arusha.
Pamoja na yote hayo CHADEMA ipo imara, na watanzania wanaelewa hilo, wanafahamu ccm wamekuwa magaidi!

Tulianza na Mungu na Tunamaliza na Mungu

Umeripoti wapi kama hao watu kutoka mwanza hawahusiani na chadema
 
Last edited by a moderator:
kwani kama hawa wanahusika kwanini polisi wanamtorosha mtuhumiwa bila taarifa kwa wakili wala familia? ujue kwamba wanatafuta mazingira ili wamfunge bila utetezu wa wanasheria
 
Dah mimi nachukia sana watekelezaj wa sheria za taifa ili pekee duniani. Nasema pekee dunian kwa kuwa ni taifa tajiri sana lenye watu masikini sana. Ivi Dpp akisha enta nolle prosequi kwa makosa yale yale na watu wale wale inawezekanaje watu wale wale warud mahakaman kwa makosa yale yale?hata kama sheria imeletwa nyingine.
 
Umeripoti wapi kama hao watu kutoka mwanza hawahusiani na chadema

Kwakuwa Polisi ni taasisi ya ccm, CHADEMA walichokifanya ni kuripoti kwa umma, na ushahidi upo lazima CCM na wapumbavu wake wote waumbuke safari hii!
 
Lakini nauliza ninyi mnaowatetea hawa ikibainika walimwagia tesha tindikali itakuwaje?acheni mahakama itekeleze wajibu wake maana tesha hajajimwagia tindikali,tusikose utu na huruma kwa wenzetu kissa siasa,Chadema mnasumbuliwa na ugonjwa wakuona haki ni kwa wanachadema tuu,sio sahihi hata kidogo

Swala sio amefanya kosa au hajafanya kosa swala ni JE wanapewa haki zao kama wadhaniwa maana jinsi polisi wanavyowafanya ni kama wameshatiwa hatiani na mahakama nawe pia usiwaaangalie kama chadema waangalie na wao kama binadamu wanao shukiwa je ikitokea hawana hatia ya ugaidi ? fikiri nje ya box ndugu
 
Tusome gazeti la mawio toleo la leo tarehe 27 june 2013 kuna unyama ambao wamefanyiwa hao vijana wanaodhaniwa kummwagia tindikali bwana tesha.
Mnyika ameeleza vizur sana na kiukweli ni mambo mabaya sana kufanyiwa binadamu,mungu atawalaani sana wote ambao wapo nyuma utesaji huu..
 
RE: HENRY JOHN KILEO.

BAADA YA SINTOFAHAMU KUHUSU KILICHOMSIBU HASA HENRY JOHN KILEO, NA BAADA YA MAJIBU YA JESHI LA POLICE KUHUSU JUHUDI ZA JOYCE KIRIA KILEWO KUFAHAMISHWA ALIKO MUMEWE HENRY JOHN KILEWO, NA BAADA YA MASWALI MENGI KWANGU KAMA WAKILI WA KILEWO NA KIRIA, NIMEONA YAFAA NITOE MAELEZO HAYA KWA KIREFU.

Henry John Kileo alipiwa simu na Maafisa wa Police Makao Makuu mnamo Tarehe 17/6/2013, wakimuarifu kwamba wanataka kufanya mahojiano naye.Hawakusema ni kuhusu nini.mara moja Kilewo akawasiliana nami kama wakili wa familia yao na Joyce Kiria,nami nikawasiliana na maafisa hao kuwaarifu kwamba kwa kuwa nina majukumu kadhaa ya kkimahakama, na kwa kuwa Kilewo yuko nje ya mkoa,basi ninaahidi kama wakili kuhakikisha ninamepeleka binafsi Kilewo Makao Makuu Police mnamo Ijumaa ya tarehe 21/6/2013.

Tarehe 21/6/2013 tuliambatana mimi, Kilewo na John Mnyika (MB) mpaka Police Makao Makuu, ambapo Mnyika alituacha na Kilewo;mahojiano yakaanza.Kwa ujumla walimuhoji Kilewo mambo mbalimbali kuhusiana na tukio la kumwagiwa tindikali kijana aitwaye Mussa Tesha katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga mnamo mwaka 2011.Wakati mahijiano hayo yanafanyika,tayari kulikuwa na Case ya jinai ikiendelea huko Igunga, ambapo washtakiwa Wanne (4) ambao ni makada wa Chadema kutoka maeneo mbalimbali nchini walishtakiwa kama mshtakiwa nambari moja mpaka nne.Walishtakiwa kuhusiana na tukio hilo nililolisema, la Mussa Tesha kumwagiwa Tindikali.Walishtakiwa chini ya vifungu vya sheria ya kanuni ya adhabu, (Penal Code, na si ugaidi).

Baada ya mahojiano na Police yaliyomalizika kwa Kileo kuandikisha statement mpaka mnamo saa 11.30 hivi za jioni ya hiyo Tarehe 21/6/2013, Police walimnyima Kilewo dhamana, na wakampeleka remand iliyoko Central Police Station,akalala huko.

Jumamosi ya mnamo tarehe 22/6/2013, mimi wakili, Joyce Kiria na John Mnyika tulifika Central Police station, ambapo OCS wa hiyo Central Police Station alituarifu kwamba amri alizonazo ni kwamba Kilewo haruhusiwi kuonana na mtu yeyote. Kama wakili nilijadiliana masuala ya kisheria na OCS, ikalazimu kuwasiliana na maafisa wa Police Makao Makuu ambao hatimaye waliniruhusu mimi kama wakili kwa mujibu wa sheria kuonana na mteja wangu.

Tukazungumza na kupeana "moyo", nikahakikisha amekula chakula kilicoletwa na mkewe Joyce Kiria (ambaye muda wote alikuwa akimuangalia mumewe kwa mbali tu,kwani mazungumzo yangu na Kilewo yalifanyika faragha).

Mnamo saa 7.30 hivi tuliondoka sote (wakili, Kiria na Mnyika), na kukubaliana kurudi tena Central Police Station Jumapili ya Tarehe 23/6/2013 kumtembelea tena Kilewo, na pia kufahamu mipango hasa ya jeshi la Police kuhusu Kilewo kwani mpaka tunaondoka si wakili wala mkewe Kilewo aliyefahamishwa rasmi kuhusu mipango hiyo.

Nikiwa Nyumbani nilipokea simu toka kwa Joyce Kiria akiniarifu kwamba amefika Central Police Station jioni ya Jumamosi ya tarehe 22/6/2013 na kuarifiwa tu kwa mkato kwamba Henry John Kilewo "ameondoka".

Ukweli kama mke alikuwa amechanganyikiwa, na jukumu la kwanza lilikuwa kumtuliza kisaikoilojia kwani nilifahamu kina Kilewo walikuwa wamepata mtoto muda si mrefu huko nyuma;kwa hiyo hali ya Joyce ilikuwa delicate sana kiafya na kisaikolojia.
Nikapambana kama wakili kwa kutumia uzoefu na contacts (P.R) ili kupata tarifa ya aliko mteja wangu.

Niliariwa tu "off record" na maafisa wa Police kwamba Kilewo amesafrishwa kwa ndege ya Precision kuelekea Tabora kupitia Mwanza chini ya ulinzi wa maafisa Senior wa Police ili kule Tabora afunguliwe Case.Sikuwa na mawasiliano yeyote na mteja wangu, na hizo taarifa "off record" ndo cha pekee tulichokuwa nacho mimi, Joyce Kiria na uongozi wa Chadema kuhusu nini kimemsibu Henry Kileo.

Niliendelea kupambana kupata taarifa rasmi, na hatimaye Jumapili ya Tarehe 23/6/2013 majira ya saa 6 hivi (noon) ndipo nilipopigiwa simu na mmoja wa maafisa waliomsindikiza Kilewo kuelekea huko Tabora kwa utaratibu ule ule wa "off record", na kuniunganisha na Kilewo, ambapo nilizungumza naye kwa kifupi kumjulia hali na kumuhakikishia kwamba tutapigana kwa uwakili wetu wote kwa ajili yake.

Kwa hiyo mpaka muda huo hatukuwa bado na uhakika wa 100% kwamba Kilewo yuko wapi hasa. Kw wale mawakili wenzangu wanafahamu kwamba huwezi tegemea taarifa za kusikilizishwa mteja kwenye simu ambayo hata si ya kwake.Wala huo si ushahidi wa alipo mtu huyo kisheria.

Lakini ikatubidi ku-"assume" kwamba Kilewo yuko/atapelekwa Tabora kushtakiwa.mimi na Prof Abdallah Safari tukaanza maandalizi ya upesi upesi ya safari kuelekea Tabora kwa gari (kwani ndege kuulekea Tabora ni Jumamosi na Jumatatu tu). Tuliondoka kwa gari ya makao makuu ya Chadema Jumapili ya tarehe 23/6/2013, majira ya saa 11.30 hivi za jioni. Tulisafiri usiku kucha, na tulichukuwa "risk" ambazo kwa kawaida tusingechukuwa, ikiwemo kupita katika mapori maarufu kwa utakaji;kilichotusukuma na kutupa moyo ni kwamba Henry John Kilewo yuko mahali ambapo anatuhitaji sana, na hana tumaini lingine bali sisi mawakili wake.

Tukisafiri usuku kucha na kufika Tabora asubuhi ya Jumatatu tarehe 24/6/2013, majira ya saa 2.30 asubuhi;tumechoka hakuna mfano.Tukabadili mavazi upesi upesi na kuvaa suits zetu na kukimbilia mahakama ya Hakimu Mkazi Tabora, ambapo turiarifiwa kuwa wao hawana taarifa zozote za Kilewo. Tukaelekea Makao Makua ya Police Tabora;jibe likawa ni lile.

Maana yake ni kwamba sisi mawakili wa Kilewo, tuko Tabora ambayo ni kubwa has, na hatujui mteja yuko wapi hasa. Nikafanya juhudi zile zile za "off record", na kufahamishwa kwamba Kilewo alishikiliwa Police Station ya Nzega (masaa matatu toka Tabora), na kwamba yuko njiani kuletwa Tabora.Hatukuwa na uhakika bado, ila ilitulazimu kushikilia hako kataarifa kasiko rasmi, na kuendelea na maandalizi ya case.
Majira ya saa 9 hivi za alasiri ya Tarehe 23/6/2013 Kilewo, akiwa chini ya ulinzi mkali sana wa FFU katika Land Cruisers Mbili za Police waliwasili Mahakama ya Hakimu Mkazi Tabora; hajala tangu jana yake.
Alikuwa yeye na wenzake wanne ambao walikuwa wamefutiwa mashtaka kwa hati ya "Nolle Prosequi" huko Igunga, kisha kukamatwa tena mara moja na kusafirishwa kwa ulinzi mkali sana mpaka Tabora.

Ukweli ni kwamba tulivyoonana na Kilewo si mawakili wala KIlewo mwenyewe aliyejizuia kulengwa na machozi;yeye akimshukuru MUNGU kwamba tumepambana na yote mpaka Tabaora kwa ajili yake kwa kasi vile, nasi kwamba hatimaye tumeonana na mteja wetu.

Tukaingia Mahakamani, Kilewo na wenzake wakasomewa mashtaka mawili; moja chini ya sheria ya kuzuia ugaidi kwamba walimteka kwa nia ya ugaidi Mussa Tesha huko Igunga, Tabora na la pili kwamba walimdhuru kwa kumwagia Tindikali.
Makosa ya Ugaidi hayana dhamana.

Mawakili tulipambana na kutoa hoja za kisheria nne (4) dhidi ya uhalali wa mashtaka yenyewe na utaratibu wa kufungua case husika. Tumeoimba mahakama kufuta mashtaka ya ugaidi, au la iamuru kila mshtakiwa arudishwe kushtakiwa mahali alikokamatwa (mfano Kilewo, Dar es Salaam).

Uamuzi wa Mahakama ni tarehe 8/7/2013.

Kabla ya kuondoka Tabora jana, tulipita kumuaga Henry Kilewo na wenzake katika gereza la Uyui. Wote wako na combat zao za chama chao, na wako imara, hasa baada ya kuona mawakili wako imara.

Cha msingi ni kuomba MUNGU aipe mahakama ujasiri.

Peter Kibatala, Advocate.
Duh,,kitambo
 
Back
Top Bottom