Abunwasi
JF-Expert Member
- Jun 25, 2009
- 5,486
- 3,468
Observation zangu kuhusu hilo ni kuwaWana-jf sina uhakika kama hili lilishawahi kuzungumzwa hapa au la. Lakini nimeona si vibaya tukalijadili na kuchangia mawazo. Ndugu yangu mmoja hakumaliza wikiendi yake vizuri jana. Kisa ni kuwa mke wake amechachamaa anataka house girl aondoke haraka. Kwa maelezo ya huyo ndugu yangu ni kuwa jumamosi ya juzi binti wa kazi aliomba ruhusa kwa mother house kwenda kusuka nywele tangu alipoondoka saa 4 asubuhi akarudi saa 11 jioni. Mother house alipomuuliza binti kulikoni kachelewa vile akadai kuwa msusi alikuwa na kazi nyingi na wateja wa kusuka walikuwa wengi so alilazimika kusubiri. Mother house hataki anasema binti ameshakuwa na kiburi so akiondoka anarudi muda anaotaka. Jamaa amejaribu kumsihi mkewe amsamehe huyo binti kwa kuwa kwanza hana uhakika wa kupata h/girl mwingine kwa haraka na ukizingatia wana watoto wadogo wa kati ya miaka 5 na 2. Mother house amepamba moto kwa nini jamaa anapinga binti kuondolewa au yeye ndio anayempa kiburi may be kashamuonja so kanogewa hataki aondoke. Kwa kweli jamaa kila akifikiria busara ya kumfukuza binti ukizingatia yeye na mkewe wote ni wafanyakazi haelewei kilichompata mkewe. Na kibaya zaidi mother house kampigia simu mpaka mama yake mzazi ( mama wa mother house) kuwa yeye muda wowote atarudi kwao kwa kuwa jamaa anapinga binti wa kazi kuondolewa kwa kuwa eti huenda anampenda sana h/girl kuliko kusikiliza ushauri wa mkewe. Ndani ya nyumba hakuna amani kisa msichana wa kazi.. Jamani hii vipi? FL, Nyamayao, Pretty na wadada/wamama wengine ndivyo mlivyo au??
1. Kina mama wengi hasa wanaojiweza kwa kisingizio cha uchovu wa kazi humuachia kazi karibu zote nyumbani na wanasahau kuwa hawa ma house maid ni binadamu na wanahitaji kupumzika na kusocialize hivyo kazi zao karibu wengi ni masaa 18 kwa siku
2. Kina mama humuachia hata shughuli za chumbani.
3. Mara nyingi kwenye ndoa hasa kwa zile zimedumu muda na mama akiwa na uwezo basi hufanya/husema mambo ambayo yanamhusu mume ambayo ni negative mbele ya house girl
Tatizo linakuja unapo appreciate [hata kama hakuna mahusiano ya kimapenzi] na kumsifu au kumtetea mbele ya mama kasheshe huanza [mama hutambua inadequacy yake lakini hapendi kukubali]. Wakati mwingine kina mama bila kujua wanawafanya waume zao watembee na hawa wasaidizi [mwanamume ingawa tuna musuli lakini ni viume dhaifu sana].
Siku moja kwa utani niliwahi kumuuliza memsap 'sasa huyu mfanyakazi ananipikia, ananifulia,anatandika kitanda ninacho lala, anatunza watoto pamoja na nyumba Sasa wewe mpenz unafanya nini??? jee huoni kuwa huyu house girl ananitunza kuliko inavyopasa?? Eeh bwana majibu aliyonipa hayafai kuyaeleza hapa na huyo mfanyakazi aliachishwa kazi baada ya muda tuu Lakini uzuri ni kwamba ingawa ilikuwa utani lakini aliichukulia kama wake up call na hivi sasa ingawa tuna mfanyakazi lakini naye anachacharika hapo nyumbani kiasi kwamba week ends inabidi nimsaidie baadhi ya shughuli.