Wakazi wa Ubungo wampongeza Rais Kikwete kujenga barabara maeneo yao

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
46,973
32,372
Wanabodi,

Wakazi wa Ubungo pamoja na wakazi wa Jiji la Dar es Salam wamempongeza Rais Kikwete kwa kitendo chake kujenga barabara za Ubungo kupambana kupunguza foleni.

Serikali imetenga Sh10.5 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa barabara hizo ili kupunguza msongamano wa magari barabara hizo ni pamoja na Mbezi Luis kupitia Goba mpaka Tanki Bovu, Mbezi kwa Yusuph, Msakuzi-Mpiji Magohe, Tegeta Bunju.

Nyingine ni Mbezi Malambamawili-Kinyerezi, Kimara-Mavurunza, Bonyokwa, Ubungo Maziwa-External, Kimara-Kilungule, Makoka, Makaburini, Kimara-Matosa, Mbezi, Ubungo-Msewe, Chuo Kikuu.

Wakazi hao wanasubiri usafari wa treni yenye uwezo wa kubeba abiria walioketi na kusimama wasiopungua 1,000 kila safari, hizo treni zitakuwa na vituo sita Buguruni, Tabata, Matumbi, Mabibo, Ubungo Maziwa.
 
Hebu elezea vizuri hiyo habari yako manake mie navyoelewa hayo maeneo yote yalikuwa na barabara toka enzi za serikali ya awamu ya kwanza sasa wanampongeza kwa kujenga nini?
 
Daaaah! Habari imekusanywa na ritz mwenyewe baada ya kuwahoji wana ccm wa ubungo!

Big up ritz
 
Ritz kumbe haya ni majukumu ya Kikwete? sasa na sisi ambao majimbo yetu hatujapata miradi hii lawama tumpe nani JK au Mbunge wetu? naomba kuuliza tu mkuu wangu.
 
Last edited by a moderator:
atakuwa aliwaita wawakilishi waende ikulu ili wakampongeze.si ndiyo hivyo ritz?
 
ni wajibu wa serikali yake kuboresha huduma na kuleta maendeleo sasa ulitaka akae hapo magogoni kuuza sura, aligombea kwa ajiri ya kuwatumikia watz, so hakuna jipya na ukizingatia ni hela zetu wananchi zake anajengea na familia yake so he ought to do so
 
Wanabodi,

Wakazi hao wanasubiri usafari wa treni yenye uwezo wa kubeba abiria walioketi na kusimama wasiopungua 1,000 kila safari, hizo treni zitakuwa na vituo sita Buguruni, Tabata, Matumbi, Mabibo, Ubungo Maziwa.......

Mosi. Hizo ni pongezi za wakazi wa ubungo au maoni yako? ni wapi yametolewa source? Pili, Mazuri yote ya serikali huenda kwa kikwete mbona mabaya huwa hayaendi kwake? hutupiwa washauri wake. Cheap popularity wont last forever.
 
Ritz kumbe haya ni majukumu ya Kikwete? sasa na sisi ambao majimbo yetu hatujapata miradi hii lawama tumpe nani JK au Mbunge wetu? naomba kuuliza tu mkuu wangu......

Usiulize sana mkuu wangu. Hali ya maisha ya wananchi imeboreka. Hivi sasa wananchi wa kawaida wamejitahidi mpaka wameweza kujijengea majumba ya ghorofa. Maisha bora kwa kila Mtanzania. Kwanini wasimpongeze Rais wao?

Canon+4+WJC+107.jpg
 
ghorofa la aina hii, kunguni wakileta fujo dawa yake piga tu kiberiti, unaua mpaka mayai. Hakuna haja ya kupoteza gharama ya kununua dawa ya RUNGU wakt thamani ya jengo hailipi.
 
Wanabodi,

Wakazi wa Ubungo pamoja na wakazi wa Jiji la Dar es Salam wamempongeza Rais Kikwete kwa kitendo chake kujenga barabara za Ubungo kupambana kupunguza foleni.

Serikali imetenga Sh10.5 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa barabara hizo ili kupunguza msongamano wa magari barabara hizo ni pamoja na Mbezi Luis kupitia Goba mpaka Tanki Bovu, Mbezi kwa Yusuph, Msakuzi-Mpiji Magohe, Tegeta Bunju.

Nyingine ni Mbezi Malambamawili-Kinyerezi, Kimara-Mavurunza, Bonyokwa, Ubungo Maziwa-External, Kimara-Kilungule, Makoka, Makaburini, Kimara-Matosa, Mbezi, Ubungo-Msewe, Chuo Kikuu.

Wakazi hao wanasubiri usafari wa treni yenye uwezo wa kubeba abiria walioketi na kusimama wasiopungua 1,000 kila safari, hizo treni zitakuwa na vituo sita Buguruni, Tabata, Matumbi, Mabibo, Ubungo Maziwa.
yaani ritz umeona taaabu sana kumsifia mnyika badala yake unamsifia dhaifu wako kikwete, sababu hii taarifa umeicopy ktk gazeti la leo la mwananchi ambapo mnyika amepongeza serikali kwa kutenga kiasi cha 10b kwa ajili ya barabara za pembezoni. fedha hizo zimetengwa kutokana na juhudi za mbunge mnyika kuishinikiza serikali juu ya kutenga fedha fedha hizo. na sasa ataishikiza serikali kutenga 100b ili barabara hizi zitengenezwe kwa kiwango cha lami. na kuhusu suala la treni kuchukua abiria ni kati ya mambo ambayo mnyika alikua anazungumza wakati wa kampeni juu ya serikali kuanzisha route ya treni ndani ya dar kupitia ubungo ili kupunguza foleni dar. lakini haya yote ritz kaona nongwa kweli kumsifu mnyika kwa kazi kubwa ya kuishawishi serikali badala yake anamsifu dhaifu kikwete.
 
kikwete ni mtu mwema sana.wananchi lazima wampongeze kwa kazi nzuri hasa ya kujenga miundombinu ya barabara,vyuo vikuu na kutoa uhuru wa kutoa maoni
 
Sasa wanampongeza wakati ni wajibu wake kutengeneza barabara.. Kumpongeza mtu kitu ni kama vile ulikua hutegemei angefanya sasa ukaona kafanya
 
Sasa wanampongeza wakati ni wajibu wake kutengeneza barabara.. Kumpongeza mtu kitu ni kama vile ulikua hutegemei angefanya sasa ukaona kafanya

tafsiri yako siyo sahihi mkuu.walichofanya wananchi ni sahihi kabisa na ndio uungwana
 
Kwa raslimali zilizopo hap nchini miradi hii ni long overdues hivyo hakuna pongezi hapo
 
Mosi. Hizo ni pongezi za wakazi wa ubungo au maoni yako? ni wapi yametolewa source? Pili, Mazuri yote ya serikali huenda kwa kikwete mbona mabaya huwa hayaendi kwake? hutupiwa washauri wake. Cheap popularity wont last forever.

Ritz kala chaka.
 
Back
Top Bottom