Barabara ya mtaani kwako ina hali gani? Tuma picha au video fupi hapa

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,115
Malalamiko ya ubovu ya barabara yamekuwepo muda mrefu na yanazidi kuongezeka kila siku hasa wakati huu wa maeneo mengi nchini kuwa katika kipindi cha masika.

Kutokana na changamoto hiyo wananchi wanakumbwa na adha kubwa wanapotumia barabara ili kutoka eneo moja kweda lingine kufanikisha shughuli zao za maisha, kero ya ubovu wa barabara umesababisha bei za bidhaa kupanda na nauli za vyombo vya usafiri baadhi kupandishwa bei.

Hali ya ubovu wa barabara unachangia kwa kiasi kikubwa kukwamisha shughuli za kiuchumi na kurudisha nyuma juhudi za wananchi kujikwamua na umasikini, barabara zinapokuwa mbuvu shughuli nyingi hukwama au kufanyika kwa tabu na kasi ndogo ivyo kulipa hasara taifa.

Je, mtaani kwako kuna marekebisho yamefanyika baada ya barabara kuharibika? Tuma tuione.

1707449760654.jpeg
K

Baadhi ya barabara ambazo zimelalamikiwa
 
Back
Top Bottom