DOKEZO KWENU SERIKALI: Adha ya usafiri kwa wakazi wanaotumia barabara ya Kimara - Bonyokwa itakwisha lini?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Mkono Mmoja

JF-Expert Member
Jan 26, 2019
1,932
4,086
Salam

Husikeni na kichwa cha habari hapo juu , Wakazi na watumiaji wa barabara kuu itokayo kimara kuelekea bonyokwa na vitongoji vya karibu kama Baa mpya,Mavurunza,Kwa Mringo na Golani wamekuwa wakisumbuka kwa muda mrefu sasa juu ya kero ya usafiri wa hii barabara.

Kiuhalisia urefu wa barabara kuu ya Kimara - Bonyokwa haizidi kilometa 7 na hivyo vitongoji vingine kuelekea kimara havizidi km 4 ila imekuwa ni kero sana hususani nyakati za usiku kutokana na madereva wa bajaji na gari ndogo aina ya Noah kutoza nauli kutoka 1000 mpaka 2000 kwa kila abiria.

Hii barabara imekuwa ikinadiwa kila leo kuwa ipo kwenye mpango wa serikali wa kuhakikisha kuwa inawekwa lami lakini zimekuwa ni ahadi hewa. Kupanda kwa gharama za usafiri nyakati za usiku na nyakati za mvua imekuwa ni mzigo kwa raia kwa wanaofanya kazi katikati ya jiji hulazimika kutumia zaidi ya shilingi 6000 kwa ajili ya usafiri kila siku.

Wito wangu kwa serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Mheshimiwa Rais Daktari Mama Samia Suluhu Hassani ifanikishe kuitengeneza hii barabara ili kutoa fursa kwa wamiliki wa daladala kuleta mabasi yao ili kuwapunguzia wananchi gharama kubwa za usafiri zinazochangiwa na ubovu wa hii barabara.

Hii ni barabara ya kimkakati inayorahisisha kupunguza msongamano wa magari ktk barabara ya morogoro kwa kutoa wepesi wa watukufika tabata segerea,kinyerezi,buguruni na ukonga pasi na kupitia ubungo.

Kipindi cha uchaguzi kinakaribia na kero kubwa ya wananchi wa kimara ni ubovu wa hii barabara.

Mbunge wa hili jimbo ndio hana habari kabisa kuhusu hii barabara, pia tunakutaka Waziri wa ujenzi kupitia TANROADS muhakikishe hii barabara inawekwa lami.
 
Asante kwa Bandiko Mkuu.

NAAMINI WAKUU WAMEKUSIKIA, TEGEMEA LOLOTE KUANZIA SASA.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
Hii kata ya kimara ilikuwa chini ya upinzani kwa muda wa miaka 10 ikiongozwa na john Mnyika ila ilikuwa haina maendeleo yoyote ,yaani ni kama haipo ndani ya jiji la Dar-es-salaam.

Huduma za Maji zilikuwa hakuna, barabara mbovu na umeme wa kusuasua. Ila baada ya kurejea chini ya CCM wameweza kuondoa adha ya upatikanaji wa Maji.

Kilichobaki ni kero ya barabara. Kipindi cha Mvua ndio hakuna kabisa usafiri hata pikipiki unaweza kukosa kutokana na barabara kuwa mbovu na zenye utelezi mkali. TANROADS tunawataka msimuangushe Rais mama Samia Suluhu.

Kimara ina wakazi wengi mno na ajenda kuu kipindi cha uchaguzi itakuwa sio nyingine zaidi ya hii barabara ya kimara-bonyokwa
 
Dar es salaam ilitakiwa kuwa na ring road inayotoka Tegeta-Madale-Kimara-Bonyokwa-Kinyerezi-Kitunda-Mbagala-Kijichi-Gezaulole.

Ukitoka Tegeta unaenda mpaka airport au mpaka Gezaulole kwa kutumia hii barabara bila kutumia Bagamoyo Rd, Kawawa Rd, Mandela Rd au Nyerere Rd.

Barabara ingepunguza sana msongamano wa magari hapo kati, pia ingesaidia kuufungua mji vizuri vitongoji vya nje vifikiane kirahisi.
 
Kabisa hizi barabara zingekuwa ni chachu ya kuinua maendeleo ya wananchi wa maeneo hayo
 
Back
Top Bottom