Wakazi wa kata ya Tambani wilayani Mkuranga tunataka barabara yenye hadhi

SAMFA

Member
Mar 5, 2023
10
18
Habari wadau.

Kwa niaba ya wananchi wa kata ya Tambani wilaya ya Mkuranga tunapenda kutoa malalamiko yetu kuhusu ubovu wa barabara .

Kata ya Tambani ni kata iliyopo Karibu Mbande kata ya Chamanzi iliyoko Dar. Wakazi wa Tambani asilimia kubwa ya vitu tunachukulia Mbande, karibia huduma zote za shule mpaka hospitali tunafuata Mbande kwa vile ni karibu sana.

Barabara ya tambani ni hatari kwa maisha ya binadamu, magari hayapiti hata bajaji zinapita kwa shida, tunaomba TARURA mtujengee japo gravel road kama hamuwezi kuweka lami.

Halmashauri ya Mkuranga wameisusa hii kata. Mbunge wetu Ulega pambania watu wako wapate barabara Bora achanana na paper work inakupotezea muda.

Halmashauri ya Mkuranga inasua sua sana kwenye miradi ya barabara.
 
Habari nzuri,
Pole, ila heading umeiandika ukiwa na hasira sana.
Pole mkazi.
Nina imani watakusikia wenye mamlaka yao maana wanakatiza katiza humu
 
Wahusika wameshalichukua pendekezo lako..
asanti...

R.I.P Laigwanan comrade ENL
 
Back
Top Bottom