Seif al Islam
JF-Expert Member
- Nov 14, 2011
- 2,156
- 638
WAKRISTO wa dhehebu la Katoliki nchini wametakiwa kuisoma kwa makini Katiba inayopendekezwa kabla ya kupiga kura ya maoni ili kufanya chaguo sahihi.
Hayo yalisemwa juzi na Paroko wa Parokia ya Bikira Maria Mama wa Huruma (BMMH) Mbezi Tangibovu jijini Dar es Salaam, Andrew Mwakibindu wakati akiongoza ibada ya pili kanisani hapo.
Katiba mahubiri yake, paroko huyo aliwaasa waamini wa dhehebu hilo popote walipo kuacha kusikiliza maneno ya wengine kuhusu katiba inayopendekezwa watumie muda wao kusoma ili wapigie kura kitu wanachokielewa.
"Nawashauri kuisoma sana katiba inayopendekezwa msisikilize kelele za watu mwende mkachague kitu mnchokielewa… ya Mungu mpeni Mungu na yaliyo ya Kaisari mpeni Kaisari.
"Msiache kuisoma katiba inayopendekezwa kwa sababu ile ni mali ya watanzania wote bila kujali chama cha mtu wala dini yake," alisisitiza paroko Mwakibindu na kuwataka kuliombea amani taifa hili.
Aliwataka waamini hao kutii sheria za nchi ikiwemo kulipa kodi na kutimiza wajibu wao katika kanisa wa kulipa zaka, fungu la 10 na kumrejeshea Mungu sadaka iliyonona ili wapokee baraka za Mungu.
Chanzo:Tanzania Daima