Wakati Mamilioni ya kuzipa Simba, Yanga na Taifa Stars zikiwepo, Shule ya Msingi Mchira Rorya Mkoani Mara Walimu na Wanafunzi wanakaa Chini

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,694
109,133
Hata hivyo GENTAMYCINE sishangai sana kwani Mshauri Mkuu wa Chalinze kamdanganya Mtu kuwa ili apendwe ajikite sana na Vilabu vya Simba na Yanga (vyenye Mashabiki wengi na wenye Ushawishi Kisiasa kama Wakikupenda) huku pia ahakikishe anaifanikisha Taifa Stars ili ikifanya vyema Sifa nyingi apewe Yeye na wala si Karia na TFF yake na Wachezaji na Benchi zima la Ufundi ambao ndiyo Wapembana.

Taarifa:

Wakazi wa Kijiji cha Mchira Wilayani Rorya Mkoani Mara wamemuomba Rais awape msaada wa Madawati na Uimarishwaji wa Majengo kwani hali ni mbaya Shuleni (Shule ya Mchira) ambapo Walimu na Wanafunzi wanakaa Chini Sakafuni kusahihisha na kusoma.

Chanzo: Kipindi cha Matukio cha RFA Asubuhi hii.

Hata hivyo Mbunge wa Jimbo hilo Bwana Jaffari Wambura amejitutumua Kuifichia Aibu Serikali kwa kutoa Fedha kidogo za kusaidia mambo machache ila bado hazijatosha.

Na GENTAMYCINE namalizia kwa Kuwakumbusheni tu kuwa hata Jana Usiku Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa kwa Maagizo ya Mama (Rais) kaenda kutupa tena Fedha kama Zawadi kwa Washindi wa Michuano isiyo rasmi kwa mujibu wa FIFA na CAF ya Ndondo (Uhuni na Usela) Cup pale Clouds Media Group (CMG) na kutoa Cash Shilingi Milioni 92 huku Wapokea Fedha hizo Wakilazimishwa kuimba Wimbo usemao..... Mama hana Mbambamba akiahidi anatoa.

Kwa nilivyomsikia Mmoja wa Mwalimu wa hiyo Shule ya Msingi ya Mchira ni kwamba kiasi cha Pesa kinachotakiwa ili Walimu na Wanafunzi wao wasikae tena chini (sakafuni) pamoja na Ukarabati wa Majengo ni kama Shilingi Milioni 50 hadi 60 tu ila kila Wakiomba Wanaambiwa Wasubirie ila Fedha za Kuwapa Simba, Yanga na Taifa Stars tumeambiwa na Rais wa nchi kuwa zipo muda wote na zitaendelea tu kuwepo.

Kazi ipo!
 
Back
Top Bottom