Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,446
- 7,822
Kamanda Murilo leo ametangaza kukamata watu wawili, mtanzania na mchina kwa kuingiza vifaa na kutangaza kutoa huduma ya internet ya starlink. Polisi wamesema wameuza vifaa hivyo bila kuidhinishwa na TCRA.
Naona kama mitandao yetu wanaipiga pini starlink by fire, by force 😅 Kwanini Serikali wasimalize mchakato kama wananchi ndio wanahitaji.
=========
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na kikosi kazi maalum cha kuzuia na kupambana na matumizi ya makosa ya kimtandao limewakamata Claudian Makaranga (28) mkazi Kawe na Hongliang Yang (35) Mchina, mkazi wa Kigamboni, kwa tuhuma za kuingiza vifaa vya mawasiliano ya intaneti nchini bila kufuata utaratibu wa kisheria vyenye jina la STARLINK KIT/DEVICE.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda maalum SACP Jumanne Muliro anasema Watuhumiwa hao wamekuwa wakijitangaza kuuza vifaa na kutoa huduma ya internet nchini kupitia mtandao ya kijamii wa Instagram kwa akaunti yenye jina la STARLINK.
Baadhi ya vifaa vilivyoingizwa nchini imebanika vilishauzwa na kutumika katika baadhi ya maeneo ya Dar es Salaam kitendo ambacho ni kosa na kinyume na sheria kwani havijaidhinishwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
EATV