Lavit
JF-Expert Member
- May 16, 2011
- 13,157
- 27,167
Ni kama tunapambana kurudi nyuma, habari kamili hii hapa!
#HABARI Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na kikosi kazi maalum cha kuzuia na kupambana na matumizi ya makosa ya kimtandao limewakamata Claudian Makaranga (28) mkazi Kawe na Hongliang Yang (35) Mchina, mkazi wa Kigamboni, kwa tuhuma za kuingiza vifaa vya mawasiliano ya intaneti nchini bila kufuata utaratibu wa kisheria vyenye jina la STARLINK KIT/DEVICE.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda maalum SACP Jumanne Muliro anasema Watuhumiwa hao wamekuwa wakijitangaza kuuza vifaa na kutoa huduma ya internet nchini kupitia mtandao ya kijamii wa Instagram kwa akaunti yenye jina la STARLINK.
Baadhi ya vifaa vilivyoingizwa nchini imebanika vilishauzwa na kutumika katika baadhi ya maeneo ya Dar es Salaam kitendo ambacho ni kosa na kinyume na sheria kwani havijaidhinishwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
#EastAfricaRadio