mwanawao
JF-Expert Member
- Aug 18, 2010
- 3,142
- 5,634
Watanzania walio wengi tulitegemea wajumbe walioko katika bunge la katiba ni watu makini na wenye uwezo mkubwa wa kuchambua mambo. Katika hali isiyo ya kawaida jana wakati wa kupiga kura ya kumchagua mwenyeketi kura saba ziliharibika. Huwezi kutegemea watu ambao wanategemewa kuja na katiba ambayo ni msingi wa Taifa hata kupiga kura tu kunawashinda? Je, kujenga hoja ya kutetea maslahi ya Taifa wataweza?
Mara nyingi tunategemea kura kuharibika sehemu ambazo kuna jamii isiyojua kusoma wala kuandika ndo huwa wanafanya madudu ya namna hiyo, na hatuwalaumu kwa sababu uwezo wao hauwaruhusu kufanya mambo juu ya uwezo wao. Ila kwa hawa wanaokula kodi zetu kila siku wakati uwezo wao ni mdogo haikubaliki.
Ni vyema hao waliofanya hayo madudu wajipime kama wanastahili kuendelea kukaa katika bunge hilo. Otherwise kwa hiari yao waondoke tu badala ya kuendelea kula kodi ya Watanzania. Maana hamna sababu ya Taifa kuendelea kuharibu hela kwa watu ambao ni mizigo.