Kama Wananchi hawaijui Katiba hadi Wafundishwe ina maana UKAWA walikula Posho ya Bure Bunge la Katiba 2014?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,147
UKAWA walisusia Bunge la Katiba 2014 wakiwa wameshatia mfukoni kodi za Walalahoi wa nchi

Swali ni: Kama Katiba Mpya haiwezekani hadi Wananchi wote waelimishwe ilikuwaje UKAWA na ile Tume ya Warioba wakalipwa maposho kibao?

Heri Shujaa Magufuli alijisemea Katiba Mpya siyo kipaumbele chake 😁😁

Msema kweli mpenzi wa Mungu!
 
Hebu acha usanii. Na hao wanaodai wananchi wapewe tuisheni ya katiba nao ni conmen watupu!
Hivi,ile katiba ya mwaka 1977 ni wananchi wangapi waliisomea/kupewa tuisheni yake?
 
UKAWA walisusia Bunge la Katiba 2014 wakiwa wameshatia mfukoni kodi za Walalahoi wa nchi

Swali ni: Kama Katiba Mpya haiwezekani hadi Wananchi wote waelimishwe ilikuwaje UKAWA na ile Tume ya Warioba wakalipwa maposho kibao?

Heri Shujaa Magufuli alijisemea Katiba Mpya siyo kipaumbele chake 😁😁

Msema kweli mpenzi wa Mungu!
Hata Maza na MaCCM walikua posho. Tena Maza alikuwa ndiye Naibu Spika.

Hawa watu kila awamu lazima waje na ulaji kwa design tofauti.
 
UKAWA walisusia Bunge la Katiba 2014 wakiwa wameshatia mfukoni kodi za Walalahoi wa nchi

Swali ni: Kama Katiba Mpya haiwezekani hadi Wananchi wote waelimishwe ilikuwaje UKAWA na ile Tume ya Warioba wakalipwa maposho kibao?

Heri Shujaa Magufuli alijisemea Katiba Mpya siyo kipaumbele chake

Msema kweli mpenzi wa Mungu!
Ndugu yetu Baptist, ina maana lile bunge la katiba lilikuwa linaundwa na UKAWA peke yao? Kama siyo hivyo kwann useme UKAWA walikula fedha ya bure? Hao CCM waliobaki ndani ya bunge la katiba, walitunga hiyo katiba mpya?

Haya mawazo ya kishabiki yanaturudisha nyuma sana Kama taifa. Watu tunajitoa ufahamu kwasababu ya ushabiki wa vyama na kujipendekeza ili mkumbukwe kwenye teuzi. Njooni na maoni ya masuruhisho ya changamoto zinazowakabili wananchi, wateuzi wanaweza kuwaona. Hii ya kuwazodoa wapinzani mpate vyeo aliondoka nayo Magufuli, huyu wa Sasa ni tofauti!!
 
Back
Top Bottom