Wajue Zitto, Slaa na Mbowe na tofauti zao

JERRY

JF-Expert Member
Feb 18, 2009
630
502
Naomba ni mu-acknowledge mwandishi wa Makala hii ya tar. 27 Nov-03 Dec. E.Kamwaga wa Raia Mwema


ZITTO

Hoja ya Buzwagi ndiyo ilioanza kumuinua mwanasiasa huyu kijana.Julai 2007 Mbunge huyu wa Kigoma Kaskazini alihoji sababu za aliyekuwa waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi,Kwenda kusaini mkataba mpya wa Mgodi wa Buzwagi ktk kipindi ambacho Taifa lilikuwa likifanyamapitio ya sheria zake.

Hoja hii ilizua mjadala mkali ambao Ulidakwa na Taifa zima.Tangu hapo Zitto akawa ameingia kwenye nyoyo za watanzania na
Hoja zake nyingi zikawaZinafuatiliwa kwa makini na watanzania.

Zitto pia ameibuka na masualaMbalimbali ambayo yameibuaMijadala mingi kitaifa.Mf. alikwendaKinyume na chama chake baada ya kukubali kuingia kwenye Tume ya Madini iliyoteuliwa na Mh.Kikwete na ambayo imeleta mabadiliko makubwa ktk sekta ya madini hapa nchini.

Yeye ndiye mtoa hoja ya kusaka mali na fedha zilizofichwa nje ya nchi, mtoa hoja ya kutokuwa na imani na serikali iliyosababisha kufanyika kwa mabadiliko ktk baraza la mawaziri na sasa anashiriki sana ktk kutafuta haki kwa nchi masikini kwenye masuala ya ukwepaji kodi wa makampuni makubwa.


Mgogoro wake mkubwa kabisa kisiasa na chama chake ulikuja mwaka 2009 wkt alipotangaza nia ya kutaka kuwania uenyekiti wa chama hicho dhidi ya Mh.Mbowe.
Wakosoaji wake wanasema kosa la kwanza la Zitto kisiasa lilikuwa ni kuwania uenyekiti na Mbowe ambaye ni mtu aliyemlea ndani ya chama.Uamuzi huo wa Zitto umemletea madhara kwa sababu umempotezea marafiki ambao walifukuzwa kwa kumuunga mkono lkn pia kupoteza sapoti ya Mbowe.Hii ni kasoro ya kutokuwa na Subira.

Katika miaka ya nyuma ,Zitto angeweza kufanya chochote na asihofu kwa vile alijua Mbowe angemtetea.Kama angeweza kusubiri kidogo pengine hadi wkt huu, huenda Zitto angeweza kupata uenyekiti pasipo kutumia nguvu nyingi.

Pia Tofauti na wanasiasa wengi wa upinzani hapa nchini, Zitto ana mahusiano ya karibu na baadhi ya viongozi wa juu wa ccm, serikali na vyombo vya dola na hivyo amekuwa mwathirika wa mara kwa mara wa tuhuma za kutumiwa na taaasisi hizo. Hata hivyo, kwa jicho lingine , hii pia inaweza kuelezwa kama mojawapo ya nguvu za mwanasiasa huyu.


DK SLAA
Huyu ni miongoni mwa wabunge waliongia bungeni ktk uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995 akipitia jimbo la kwao karatu.Hakuwa maarufu sana kwenye miaka ya 1990 na watetezi wake wanasema utawala wa kiimla wa aliyekuwa Spika wa Bunge , Pius Msekwa ulichangia zaidi hali hiyo.
Umaarufu wa Dk Slaa ulianza kutokea siku moja ya sept.15 2007 ktk viwanja vya Mwembeyanga, vilivyopo Temeke DSM pale alipotangaza iliyokuja kufahamika sana kama "Orodha ya Mafisadi".
Habari hiyo ilipata sapoti kubwa kutoka vyombo vya habari kwani kwa mara ya kwanza ktk historia ya siasa za Tanzania,vyama vya upinzani vilitaja hadharani majina ya watu wanaotajwa kuwa vinara wa rushwa hapa nchini.

Habari hiyo ilikuwa muhimu sana kipindi hicho kwani CDM ilikuwa imeanza kujenga hoja kama chama kuhusu upotevu wa mabilioni ya shilingi ktk iliyokuwa akaunti ya madeni ya nje (EPA) ya Benki kuu ya TZ.

Ktk Bunge lililopita chini ya Spika Samuel Sitta, Slaa alijipambanua kama mmoja wa wapinga ufisadi na nafasi yake kama M/kiti wa kamati ya ya Bunge ya Hesabu za serikali za mitaa,ilimpa fursa ya kuibua ufisadi ktk maeneo mbalimbali hapa nchini.


Akiwa mgombea Urasis ktk uchaguzi wa 2010 Dk Slaa alikuwa kivutio kwa wengi kutokana na tabia yake ya kupenda kuzungumza kwa kutumia takwimu.
Wapo wanaoamini CDM kilipata wabunge wengi kuliko wkt mwingine wowote tangu kianzishwe kutokana na mvuto na ufuasi aliokuwa nao mgombea huyo.

Kutokuwepo kwake ndani ya Bunge kunaelezwa kama kumeondoa eneo lake moja muhimu la kujieleza na hivyo kuonekana kudhoofisha umaarufu wake.

Wakosoaji wa Slaa wanaeleza kwamba amekuwa na tatizo la kutotaka kushaurika na pia mara nyingi si mtu wa kuonekana kwenye matukio makubwa ambayo huwa yanawasaidia wanasiasa kuonekana.
Mfano unaotolewa mara kwa mara ni kukosekana kwake hivi karibuni ktk tukio la kuaga mwili wa marehemu Dk.Sengondo Mvungi lililofanyika jijini DSM – tukio lililohudhuriwa na watu wengine maarufu kutokana na umaarufu wa marehemu.

Kwamba kama hana hoja ya kuzungumza , ni rahisi sana kwa Slaa kupotea kwenye jamii kwa vile si mtu anayependa kuijchanganya.Tabia hii ,wanasema,watu wanaomfahamu kwa karibu,pengine inatokana zaidi na malezi yake ya kilei aliyoyapata wkt akiwa padre wa kanisa katoliki.
Wanasiasa mahiri hutafuta njia za kuonekana mara kwa mara ili wasipotee.Rais Kikwete anaweza asiwe na habari kubwa ya kufanya lkn anaweza kuonekana akiwa msibani,mpirani,mkutanoni, na au safarini.Ni sanaa ambayo Dk.Slaa ameshindwa kuimanya

MBOWE

CDM hii inayoonekana leo ina mkono wa Mbowe ktk eneo zaidi ya moja.Ktk wkt wake, CDM imepata mafanikio makibwa ambayo wengine hawayakuwazia wkt alipopewa madaraka.
Mbowe alipokea uenyekiti wa CDM wkt chama kikiwa na wabunge wasiozidi watano na kikiwa ana kila dalili za uchovu.

Ingawa Baba wa Taifa ,Mwalimu Nyerere . tayari alikuwa ameonyesha kuvutiwa na sera za CDM , lkn kilionekana nichma cha wastaafu , wasiotaka ugomvi na serikali na wasio na shida .Matajiri.Yote yakabadilishwa na Mbowe.
Kubwa kuliko yote ambalo Mbowe amelifanya kwa CDM ni namna alivyoweza kuwaamini vijana na kuwapa majukumu mazito.
Huwezi kutaja vijana kama Zitto,Mnyika,John Mrema, H.Mdee, Kafulira na Muhonga Said Ruhwanya pasipo kutaja mchango wa Mbowe ktk kuwa-groom kiuongozi.
Hata kama vijana hawa wana akili za kutosha vichwani mwao,walihitaji fursa kuweza kuonyesha umahiri na ni Mbowe pekee,miongoni mwa viongozi wa vyama vya siasa nchini, ndiye aliyeweza kucheza kamari na vijana na amevuna matunda ya uamuzi wake huo.

Kwa sasa CDM , pengine ndio chama kinachoweza kijivunia kama tumaini la vijana wengi hapa nchini ambao wanaamini watapata fursa endapo tu watajiunga au kujihusisha na chama hicho.
Ni wanasiasa wachache sana hapa nchini wenye uwezo wa wa kushindana naye pindi anapopanda kuzungumza na wananchi.

Ni Mbowe huyuhuyu ambaye utaratibu wake wa kutumia Helikopta wkt wa kampeni za uchaguzi umebadili kabisa namna ya ufanyaji wa kampeni. Sasa karibu vyama vyote vimeona umuhimu wa kutumia chombo hicho ktk kampeni zake.

Pia CDM, ni chama pekee nchini ambacho kina ubunifu wake wa mavazi na hili pia linahusishwa naye kwa vile limetokea chini ya utawala wake.

Hata hivyo wakosoaji wa Mbowe wanataja kasoro zake kubwa mbili.Mosi ni ile ya kutokuwa na uwezo wa kuibua hoja binafsi zitakazomtambulisha yeye binafsi.Wakati Slaa anaweza kuijgamba na EPA na orodha ya Mafisadi, huku Zitto akijitapa kwa Buzwagi na Mabilioni ya Uswisi,M/kiti huyu hadi sasa hana hoja ya binafsi anayoweza kuisimamia kwamba ni yake.
Hivyo anaonekana kama ni mwanasiasa wa matukio.

Kasoro ya pili imetajwa kuwa ni tabia yake ya kuhofia upinzani kutoka ndani ya chama chake au jimboni.Wakosoaji wake wanasema hata tofauti zake na Zitto zimesababishwa zaidi na kilichotokea 2009 kuliko kitu kingine chochote.

Watetezi wake wanasema tabia hii huenda inatokana na ukweli anatoka ktk familia (bora)ya kitajiri na hivyo ubongo wake umetengenezewa dhana ya kumiliki na ndiyo maana si rahisi kwake kuvumilia upinzani
 
mwandishi alikuwa anamuegemeo na mtu katika hao aliowataja.
hata hivyo kwa uchache huu wa wasifu alioutoa kwa wote haitoshi kuwajua watu hao kiundani.
 
mwandishi ajafunguka inavyo takiwa kwa mfano ujasiri wa Mbowe ni mkubwa kuliko mwanasiasa mwingine hapa tz
 
Mbowe ukimpa muda wa kumsikiliza hata dakika 5 tu lazima atakushawishi ukubaliane naye, huyu jamaa ni noma!!
 
Tumekusoma mkuu ,hii ni kwamtindo mwingine ila kwa maana ile ile .....kumbe jamaa yuko seriously eeenh...
 
mwandishi ajafunguka inavyo takiwa kwa mfano ujasiri wa Mbowe ni mkubwa kuliko mwanasiasa mwingine hapa tz

kweli
kabisa kuwa mwenyekiti wa chama, procurement officer wa chama na loan officer and cashier mfanowe hakuna


sifia tu watu ufe maskini
 
Mi wiki ijayo nitatoa makala inayohusu maisha na harakati za kisiasa za Kamanda @Nyakurungu.

Stay tuned...
 
Nianze kwa kuzungumzia mapungufu ya hawa watu wawili dk slaa na zitto kabwe ili jamii ielewe nani alianguka wapi na na wapi alianguka nani

DK SLAA

Kiukweli dhahama inayomkuta Zitto hivi karibuni ni baraka za dokta slaa. Dokta alilijua hili mapema na alikuwa na jukumu la kumuita Zitto na kumuweka chini kisha kumuonya kwa mienendo yake na kumrudisha kwenye mstari ulionyooka. Ilikikuwa ni busara kwa dk kama sehemu ya balaza la wazee kumshauri Zitto bila kuchoka kama kijana wake juu ya mwenendo wake
Ila alichokifanya dokta ni kushirikiana na viongozi wenzake wa juu wa chama kumtenga na kumuona kama msaliti badala ya kumshauri.Dokta ameutumia mwenendo huu wa Zitto kama fimbo ya kumchapia Zitto kwa maslai yake binafsi ya kuondoa ushidani wa mtu yeyote dhidi yake na huku akiuficha ukweli huu kwa naneno ya kukijenga chama dhidi ya wasaliti

ZITTO KABWE

Ni kijana aliyepambanua kama mzalendo ila kiukweli ana mapungufu ambayo siyo sehemu ya uzalendo kama mwanasiasa.Hali ya kuwaona wenzio hawafai na kujiona wewe ni bora kuliko wenzio ni udhaifu mkubwa.Kama unaona uongozi haufai kwanini usiwe wazi na kuyaweka haya hadharani na wao wakajua au kwanini usikae na kuongea na viongozi wa chama juu ya udhaifu wao na wapi wajilekebishe hii ni tabia ya ubinafsi na upenda sifa kwa maslai binafsi na tabia hizi hupelekea mtu kuwa na tamaa ya madaraka

VIONGOZI WENGINE NDANI YA CHAMA HASA WABUNGE

Ni fedheha kwa kiongozi wa chama au mbunge kujipendekeza kwa viongozi wa juu wa chama na kuongea maneno ambayo wao viongozi wa juu wa chama wanapenda kuyasikia na yanawafurahisha au kuwatetea ili mradi tu na wewe wakufikirie au au wakutafutie nafasi furani.Kumbuka kuwa unauza utu wako kwa maslai yako binafsi ila jua ya kwamba na wao wanakupa nafasi hiyo kwa maslai yao binafsi ili wakutumie
Watu tunaamini kwenye siasa za kusema na kutenda.Lakini naona sisi wapinzani tumeegemea kwenye kusema bila hata ya kutenda mfano mzuri ni majimboni mwetu tumefanya nini.Tupo radhi tukitetee chama kuliko nchi tuko tayari kumtetea mwanachama kuliko mwananchi hata kama udhaifu umeonekana. Ikumbukwe kuwa wanachama pekee hawawezi kukipa ushindi chama ila wananchi wanauwezo wakukipa ushindi chama kwa kwani wanachama sehemu ndogo ya wananchi

WITO WANGU
hakuna msafi ndani ya chama ndo maana huyu yupo kundi hili na yule yupo kundi lile cha muhimu ni kwamba
Viongozi wasijisahau na kujifanya wao ni miungu watu wanaojua kila kitu huku wakutumia fedha za wanachama kuwadharau hao hao wanachama waliowapa dhamana ya kuwaongoza na kutumia sera za umaskini wa watanzania kuficha udhaifu wao. Tuwe wazalendo wa kweli kwa kusimamia sera ya kusema na kutenda
 
Chadema ni sawa na mbuyu mkubwa unaoliwa na mchwa ndani kwa ndani, siku ukianguka ndio watu watajua ubovu wake
 
Hivi Dr. Ashindane na Zitto ili iweje? Hivi unafikiri Dr. Anamiaka mingapi imebaki kwenye uongozi wa kisiasa au hata umri wa kuishi hadi aamue kupambana na mwanaye Zitto?

Tuwe wa kweli Zitto angevumilia miaka 5 au 10 ijayo na kuendelea kuwa karibu na hawa wazee angepungua nini? By the way kwa vijana walioko Chadema sasa hivi kuna wa kupambana na Zitto miaka 5 au 10 ijayo?

Ukweli ni kuwa Zitto ametumika kudhoofisha mapambani sikuzote tangu alipo ingia kwenye kamati ya Buzwagi.

Na hakika usaliti huu hauto muacha utamtafuna Daima milele.
 
Homa ya uchaguzi ndani ya chama. Mbowe anamuogopa zitto kwenye uenyekiti, slaa anamuogopa zitto kwenye urais kwa hiyo slaa na mbowe wameungana kumpiga adui yao zito
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom