Wajamaika na Jarida la Forbes wampa tano Rais Samia

Billal Saadat

Senior Member
Nov 30, 2022
169
356
Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuagiza Fedha zilizotengwa kwa ajili ya Sherehe za Uhuru Zaidi ya Milioni 900 zipelekwe Ofisi ya Rais TAMISEMI Kujenga Mabweni kwenye Shule za Msingi (8) za Wanafunzi wenye mahitaji Maalumu.

Nchini Jamaica wameitaka Serikali yao kujifunza kupitia Tanzania kwa Rais Samia matumizi ya Pesa zilizotengwa kwa ajili ya gwaride la miaka 60 ya Uhuru wa Jamaica zitumike katika kuboresha baadhi ya miundombinu nchini humo.

Tanya Stephanie muimbaji mashuhuri wa muziki wa Dancehall na Raggae ameitaka Serikali ya Jamaica kufanya jambo Jema kama hilo la kujifunza kutoka kwa Rais Samia.

Kauli ya Tanya imeungwa mkono na mashabiki wanaomfiatilia Tanya kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa kitendo alichokifanya ni cha kiungwana sana na kinafaa kuungwa mkono.

Vivvienie Tanya Stephanie ni moja kati ya Wasanii mashuhuri nchini Jamaica aliyevuma sana miaka 90 kipindi muziki wa Reggae umeshika hatamu Duniani alitoka na kibao chake matata “Yuh Nuh Ready Fi Dis Yet” wale wa Dancehall mnaweza kuwa mnakifahamu zaidi.

Wakati huohuo Jarida Maarufu Duniani Forbes limemjumuisha Rais Samia kuwa miongoni mwa Wanawake wenye nguvu Duniani kwa Mwaka 2022.

Ngoma za Tanya unaweza kuziperuzi kwa wakati wako ukiwa ni msimu wa sikukuu huu.

"Skettle 2004" (2004), Golden Kartel – Tanya Stephens and Cecil, B-side of Sasha's "Run Dung Me"
"Enuff 4 U" (2004), Wall of Sound – TCC Prassay featuring Tanya Stephens
"Dance 4 Me" (2006) – Mark Morrison featuring Tanya Stephens, promo only CD-R
"Child of the Universe" (2007) on Chuck Fenda's album The Living Fire (2007)[26]
"Heart of Stone" (2008), Bass Inna Yu Face – Taddy P. featuring Tanya Stephens
"Want Love" (2012), Kirkledove – with Marcia Griffiths

IMG_0327.jpg

IMG_0329.jpg
 
Hao wajamaica hawajui kitu ishu kubwa IPO kwenye usimamizi wa hizo pesa alizoamrisha zijenge mabweni... Huyu mama anapigwa Tu
 
Hao wajamaica hawajui kitu ishu kubwa IPO kwenye usimamizi wa hizo pesa alizoamrisha zijenge mabweni... Huyu mama anapigwa Tu
Hivi ni dharau ndio inayofanya tuone kuwa huyu rais mwanamke yeye anapotoshwa tu hana anachokijua au hatutaki tu kukubali kuwa anahusika na hayo yanayoendelea?
 
Wameanza kukiri wenyewe bila shuruti kuwa nchi inaongozwa na mbumbumbu
 
Hivi ni dharau ndio inayofanya tuone kuwa huyu rais mwanamke yeye anapotoshwa tu hana anachokijua au hatutaki tu kukubali kuwa anahusika na hayo yanayoendelea?

Haya tunasema ni ubinadamu. Nyie mkiwa manaendelea vizuri hamuwakumbuki wengine wenye uhitaji acha Rais samia afanye kwa moyo wake.
 
Kwamba wajamaika wanaijua hii nchi kuliko sisi!!??
Hakuna kipya hapo hizi zilikuwa ni staili za Magu kukansel sherehe kutumia pesa kwenye maendeleo
 
Back
Top Bottom