Waitara ahamasisha wananchi kuigomea serikali Wilayani Tarime

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566


Waitara akihutubia mkutano wa hadhara Wilayani Tarime ameonekana akizungumza kwa jazba huku akiwaeleza Wanachi mambo mbalimbali. Akiwa katika mkutano huo Waitara alisema:

"Muda wa kubembelezana sasa umeisha, siku ile mliniona nalia nilikuwa natoa sumu. Siku ile ningekuwa hapa leo tungekuwa tunazungumza historia nyingine.


Kama kuna mtu amekuja hapa kuandika umbea apeleke, niwaambie tafuta daftari kubwa sana kwa sababu safari ya harakati imeshaanza, yaani hapa shughuli bado. Kwanza tutatafutana mmoja mmoja tupimane uzalendo.

Kwa wale wenye simu ya kurekodi naona na polisi yupo ongeza mabomu na risasi, tupo hapa. Nataka niwaambie hawa watu wanaotulazimisha twende wanakotaka wanafikiri sisi ni waoga? Hawajui sisi wengine ni mili tu inatembea? Walishatuzika siku nyingi.


Wametuchokonoa, mkutano unaofuata mwingine tutafanya katikati ya Bwerege, tutatangaziana mwezi mzima, hakuna mwenyeji atabaki ndani. Aliyepo Tarime Mjini, Dar es Salaam au Kanda ya Ziwa tutawaita Bwerege wote waje. Wakitaka watuue wote tuanze kiazi upya ndiyo wachukue maeneo yetu hapa, naomba muanze kupigiana simu."

====

Mbunge wa Tarime Vijijini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwita Waitara ametangaza kutounga mkono uwekaji wa bikoni (vigingi) unaotekelezwa na Serikali katika vijiji vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti upande wa jimbo hilo.

Akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kegonga katani Nyanungu, jana Aprili 3, 2023 baada ya kutembelea maeneo yaliyowekwa bikoni, Mbunge Waitara alidai mpango huo ni haramu na kuwataka wananchi kuendelea kuyatumia kwa kilimo.

“Yale mashamba ya watu, wananchi waendelee kulima kama kawaida. Zile bikoni siyo halali ni ‘fake’… wanatulazimisha kwenda wanakotaka,” Waitara ambaye amewahi kuhudumu kama Naibu Waziri kwenye wizara mbalimbali katika Serikali ya Awamu ya Tano na Sita aliwambia wananchi hao.

Alisisitiza kutounga mkono uwekaji wa bikoni hizo akidai wanavijiji husika hawakushirikishwa katika maridhiano ya kutekeleza mpango huo.

Naye Diwani wa Kata ya Nyanungu kwa tiketi ya CCM pia, Tiboche Richard akizungumza awali katika mkutano huo, alipinga uwekaji wa bikoni hizo akitoa sababu kama hizo za Mbunge Waitara.

Diwani Tiboche akizungumza mkutanoni Tiboche alikwenda mbali zaidi na kusema udiwani wake hauna maana na kwamba chama chake kikitaka atauachia. “Ndugu zangu mimi niliwambia, narudi tena kusema leo kwenye mkutano huu, udiwani wangu hauna maana yoyote, kama ni udiwani wauchukue,” alisema.

Msimamo huo wa Mbunge Waitara na Diwani Tiboche unatofautiana na viongozi wao chama tawala ngazi ya wilaya na mkoa, ambao wanaunga mkono uwekeji wa vigingi hivyo ili kupata suluhu ya mgogoro uliopo.

Hivi karibuni, Katibu wa CCM Wilaya ya Tarime, Valentine Maganga aliwataka wananchi wa Kata ya Nyanungu kuendelea kuwa watulivu kipindi hiki cha uwekaji wa vigingi vya mpaka wa vijiji vyao na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, huku akiwatia moyo kuwa Serikali ya chama hicho tawala iko makini kuhakisha maslahi yao yanazingatiwa.

Akizindua uwekaji wa vigingi hivyo Machi 27, 2023, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Meja Jenerali Suleiman Mzee alitoa onyo kwa wanasiasa wanaochonganisha Wananchi na Serikali ili kukwamisha shughuli hiyo. “Nawaonya… msijione mko juu ya sheria,” alisisitiza.

Serikali inatekeleza mpango wa kuweka bikoni ili kutatua mgogoro wa muda mrefu wa kugombea mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na vijiji vinavyopakana nayo upande wa Wilaya ya Tarime, vikiwemo Kegonga na Nyandage vya katani Nyanungu.

Taarifa zaidi kutoka serikalini zinasema uwekaji wa vigingi hivyo ni utekelezaji wa maamuzi ya Baraza la Mawaziri kutokana na ushauri wa Kamati ya Mawaziri Wanane wa Kisekta iliyoundwa na Serikali kukusanya maoni ya ufumbuzi wa migogoro ya ardhi kati ya wananchi na Hifadhi za Taifa nchini, ikiwemo Serengeti.

Hata hivyo hadi Ijumaa Machi 31, 2023, kazi ya uwekaji wa vigingi vya mpaka wa vijiji vya katani Nyanungu na Hifadhi ya Serengeti iliripotiwa kuendeleea kwa amani, huku baadhi ya Wananchi wa maeneo hayo wakijitokeza kutoa ushirikiano. Kazi hiyo ya kuweka vigingi inatekelezwa na wataalamu wa Serikali kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.


Kwanini haya yanatokea?
Inadaiwa kwamba kuna mgogoro wa ardhi katika sehemu ya Hifadhi ya Serengeti, Wananchi wanaamini hawajashirikishwa na wanaona ardhi yao inachukuliwa kibabe.

Hivyo, Mbunge Waitara yupo upande wa Wananchi, RC yupo upande wa mamlaka wanaogawa hiyo ardhi.

Aidha, inadaiwa pia kuna mgawanyiko wa viongozi wa CCM ndani kwa ndani kutokana na kuelekea uchaguzi ujao, Polisi nao wapo upande wa Mkuu wa Mkoa.
Pia soma:

 
Kwisha ndugu yangu Mwita, Angalia plan B, hilo jimbo anapewa Heche. FM na wasaigon ndio walivyokubaliana, Kuna majimbo FM anapewa ili vijana wake wasife njaa.

Mwita ulikuwa Waziri, Mbunge kwa 10yrs + kipindi ya CDM kama hujamake jamaa yangu sijui itakuaje, maana nina wasiwasi hata ubunge ukiisha jamaa wanakuweka kapuni.
 
Kwisha ndugu yangu Mwita, Angalia plan B, hilo jimbo anapewa Heche. FM na wasaigon ndio walivyokubaliana, Kuna majimbo FM anapewa ili vijana wake wasife njaa.

Mwita ulikuwa Waziri, Mbunge kwa 10yrs + kipindi ya CDM kama hujamake jamaa yangu sijui itakuaje, maana nina wasiwasi hata ubunge ukiisha jamaa wanakuweka kapuni.
Wasaigon noma ndio wanaendesha nchi hii
 
Aisee lakini maovu lazima yafichuliwe ebu cheki watu wametafuna mabilion mama kaongea tu hakuna hatua zilizochukuliwa zaidi ya kuwaambia wezi hawatozikwa na fedha.
 
UKiwa MJINGA utashughulishwa na wanasiasa wa aina hii, kwa mwelevu akiangalia matumbo yao tu yanatosha kuandika kurasa mia moja za habari zao.

Any way, anaangaikia riziki yake.
 
Nipo mkoani Mara nimepewa dokezo na mtu wa uhakika kwamba kuna vita inaendelea huko Tarime kijijini cha Mrito kata ya Kemambo.

Sababu kubwa ikiwa ni migogoro ya ardhi huku mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tarime akiwa na upande wake
Hizi taarifa umezipata wapi mkuu. Siku nyingine chunguza chanzo cha taarifa kwanza.
 
Nilichosikia ni KWAMBA Kuna mgawanyiko mkubwa ndani ya Chama kile kila mmoja anavuta kamba kwake na kutafuta kuungwa Mkono kundi moja linapotosha na jingine linajenga.

Wananchi watakuja kujua baadaye kwamba wanatumika vibaya Kwa maslahi binafsi ya walafi.

Hivi inaingia akilini kusema lazima damu imwagike au ningekuwepo historia ingeandikwa au mgogoro huu upo kabla sijazaliwa hivyo unataka uendelee kuwepo! Unawaambia machief wawalaani waliojipatia ajira kuchimba na kubeba vifaa vya UJENZI!

Niliwahi kupita maeneo hayo kwakweli Kuna kila haja ya Serikali kuwekeza kuwaelimisha Wananchi wa maeneo hayo Kwa mpango maalumu wanapata viongozi ambao hawana Nia ya kuwakomboa Wananchi badala yake ni kuwahamasisha kufanya Vita ambayo mwisho wake wanajua watashindwa na kukimbilia Kenya viongozi ambao haiwezi hata kupinga ukatili wa Kukeketa watoto na kuwanyima soko la kuoelewa kwakuwa wanavuruga utamu wa mabinti Wetu wakiwa wakubwa.

Viongozi ambao bado wanafikra za kuchunga badala ya kufuga. Ukiona Kuna mgogoro basi usiamini kwamba wewe ndiyo mwenye haki lazima mgogoro utatuliwe ili maisha yaendelee ukileta maslahi binafsi Kwa gharama ya damu ya mwanadamu ni dhambi na huwezi kufanikiwa.

Kwasasa kuelewa ni ngumu lakini 2025 nimekaa paleeee nawaangalia majibu mtayaona.
 
Back
Top Bottom