KAMATI ya Siasa ya Shura ya Maimamu jana ilizindua programu ya Elimu ya Uraia yenye lengo la kutekeleza kwa vitendo waraka wake kuhusu uchaguzi mkuu wa mwakani.
Programu hiyo inataja sifa za msingi za chama na mgombea anayepaswa kuchaguliwa, masuala ambayo yalisababisha utata mkubwa baada ya nyaraka hizo za Shura ya Maimamu na Kanisa Katoliki kutolewa.
Mpango huo umo kwenye kitabu cha kurasa 76 na unataka Waislaam kuutekeleza kwa vitendo mwongozo uliozinduliwa na kamati hiyo Agosti 26 mwaka huu.
Programu hiyo ilizinduliwa jana kwenye Msikiti wa Mtoro jijini jijini Dar es Salaam na balozi wa zamani wa Tanzania katika nchi za Ufaransa na Italia, Abbass Sykes. Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo, Sykes alisema: "Nchi hii ni ya Watanzania wote, hakuna chama wala mtu mwenye hati miliki ya kutawala nchi hii."
Alisema kila chama na mtu bila ya kujali rangi, dini, kabila au mahali alipotoka, ana haki ya kuomba uongozi ili mradi awe amegombea nafasi ya uongozi kwa kufuata taratibu na sheria zilizopo.
Sifa za mgombea zinatajwa katika mada nambari tano ya kitabu hicho cha 'Elimu ya Uraia' kikitaja bayana sifa za mgombea anayetakiwa kupigiwa kura na Waislamu. "Awe kiongozi mwadilifu, anayejua matatizo makuu ya nchi na wananchi na mjuzi wa kuyatatua.
Matatizo makuu ya nchi ni udini, ubaguzi dhidi ya Waislaam au baadhi ya watu, rushwa, uchafuzi wa mkataba wa Muungano na ukosefu wa maadili kwa viongozi," inasema sehemu hiyo katika ukurasa wa 65.
"Awe kiongozi mwenye utashi wa kuwasaidia wananchi wote bila ya kujali tofauti zao, ajali zaidi maslahi ya umma kuliko ya chama chake, awe tayari kusaidia urejeshaji wa haki za wananchi zilizotaifishwa na serikali ikiwa ni pamoja na shule, ardhi na majengo."
Kitabu hicho kinaeleza kuwa ili mgombea apigiwe kura, anapaswa awe anafahamu haki na dhuruma walizofanyiwa Waislaam kwa kutotendewa haki sawa na dini nyingine na awe tayari kufuta makubaliano baina ya serikali na kanisa.
"Kiongozi huyo lazima awe tayari kutomwaga damu ya Waislaam kama ilivyotokea mara kadhaa katika misikiti, maandamano ya kudai haki au katika mahubiri ya kidini."
Kuhusu chama kinachostahili kuingia madarakani, kitabu hicho kinafafanua kuwa ni kile ambacho serikali yake haitawazuia Waislaam kufuata na kutangaza dini yao kwa uhuru na ambayo haitabadilisha sheria za Waislaam zinazohusu mambo ya mirathi, ndoa na talaka.
Kamati hiyo ya siasa ya Shura ya Maimamu, ilikumbushia migogoro mbalimbali baina ya serikali na Waislaam na kwamba chama kinachofaa ni lazima kiwe tayari kuunda tume huru kuchunguza mauaji ya Waislaam yaliyotokea miaka iliyopita.
"Kiwe chama ambacho serikali yake, itakubali kufanyika kwa uchunguzi wa mauaji ya waislaam katika maandamano ya kutetea Qur-an 1988, mauaji ya msikitini Morogoro 1994, mauaji ya kinyama msikitini Mwembechai 1998, mauaji ya imamu wa msikiti wa Mwembetanga 2001 na mauaji katika maandamano ya Waislaam ya kupinga kufungwa kwa mwenzao aliyesema Yesu si Mungu mwaka 2001," inafafanua sehemu ya kitabu hicho.
"Kiwe chama ambacho serikali yake haitakuwa tayari kupokea maagizo, sheria na misamiati mipya dhidi ya Waislaam kama vile magaidi au siasa kali na kuwasikiliza masheikh na maimamu pamoja na viongozi wengine wa taasisi za kiislaam."
Awali katibu wa kamati ya siasa ya Shura ya Maimamu, Sheikh Ponda Issa Ponda alisema: "Muongozo (wa awali) umefanikiwa sana hasa mikoani, katika mikoa ya kanda ya kusini zaidi ya asilimia 90 ya viongozi walishinda katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji ni Waislaam wanaojielewa."
"Asilimia 75 ya wilaya zote za Tanzania zimefanya warsha na makongamano kuuchambua mwongozo, hotuba za Ijumaa zenye mwelekeo mmoja zimeanza jijini Dar es Salaam, Baraza Kuu la Wanawake wa Kiislaam limetanga kura ya maslahi kuwa ajenda yao kuu 2010 na Taasisi 15 zimesaini makubaliano ya pamoja kuelekea uchaguzi mkuu."
Kwa mujibu wa sheikh Ponda, program mpya ya elimu ya uraia itatekelezwa katika mifumo ya machapisho, warsha, semina, makongamano, mikutano ya hadhara na hotuba kali za Ijumaa zenye mwelekeo mmoja katika miskiti yote nchini.
Source: Mwananchi