Bongolander
JF-Expert Member
- Jul 10, 2007
- 5,067
- 2,197
Sasa nafahamu sababu kwanini wanchama wa JF wanahamia 'Issa Michuzi blog'.
Nyie endeleeni hivyo tu na mawazo ya kuwagawa watanzania kwa misingi ya dini, wakati watanzania wanafahamu dhati kuwa Sheria za kanisa haziwahusu waendao Msikitini. Na hali kadhalika kwa mahakama ya kadhi haitomuhusu mzee wa kanisa. Hilo ndilo la msingi, na kwa wale wataobahatika kutembelea Issa michuzi blog hawataona au kusoma upotoshaji wa maudhui kupitia udini.
Na ukifanikiwa kuingia huko nakuhakikishia kuwa JF utaingia kwa nadra sana. Mkitaka kuuwa Blog endeleeni na mambo kama haya, mimi siwahukumu, ni wakati ndio utawahukumu.
Mkuu ungefafanua kidogo hapo unaposema sheria za kanisa, sijui kama Tanzania tuna kitu kinachoitwa sheria za Kanisa. Najua kuwa makanisa yana taratibu mbalimbali, lakini taratibu hizo sina hakika kama zilipitishwa kwenye ilani ya chama chochote, na sina hakika kama na kama zilipitishwa na serikali au bunge, na kama zipo kwenye katiba ya nchi. Kwa misngi huo sioni kama kuna haja ya mambo ynayohusu waislamu yalipiwe na kodi za watanzania. Kama waislamu wakitaka kuvunja ndoa au wakiwa na matatizo ya ndoa, hawana haja ya kwenda kwenye mahakama nyingine waende tu kwa masheikh hiyo itawasaidia kukwepa mahakimu wakristo na wapagan.
Mkuu kuna mambo mengine yanatia shaka, unataka kusema JF ni blog? is it? it does not look like that to me. Inaonekana kama ni web forum ambayo inaendeshwa semi professionally (sooner to be professionally). Na sijui maana yako nini unaposema ukienda blog ya michuzi hutarudi huku. Do you mean ya michuzi ni ya kiislamu na JF ni ya kikirsto? i can not believe udini unaanza kuonekana hata kwenye blogs, i hope nimeelewa vibaya.