Waislamu tuwe makini na watu kama akina Ponda na mfanowe

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
11,170
15,851
Habarini za kutwa wadau,natumai muwazima wa afya tele.kwanza kabisa naruhusu mapovu kwa wale wote ambao wataona mimi ni jasusi ama ni kafiri ambae natumia mgongo wa uislamu kuwatukana mashekhe lakini hapa situkani nazungumza hali halisi.

Katika watu ambao wanaonekana na sura ya ushekhe katika madhhabu ya kiislamu ponda huwezi kumkosa,na amekuwa ni mtu ambae anasauti kwa waislamu wengi pale anaposema jambo fulani basi watu huliitikia jambo hilo.

Lakini jambo ambalo nataka niwajuze watu kwa ufupi ni kwamba huyu anayeitwa shekhe ponda iissa ponda ni muislamu wa kawaida tu ambae amekuwa mzungumzaji mzuri na wala hakupaswa kuvikwa vazi la ushekhe na etii asimame kusemea maslahi ya waislamu.hili mtukane mpasuke habari ndo hiyo.

Ponda sio mwanazuoni ambae anaweza kutegemewa katika baadhi ya mambo ya kiislamu,lakini tu amekuwa mwanaharakati musialmu,mzungumzaji mzuri na hapo ndo akapewa ushekhe kwa sababu ukiwa na hayo mambo katika uislamu utaonekana shekhe tu.

Nakupa mfano wa wasomi ambao tunaweza kusema ni wasomi wamekaa wakasoma usialmu,mfano ni SHEKHE KUNDECHA huyu bwana ni msomi wa dini kinyume na ponda japo kuwa na yeye ni mwanaharakati.mfano tu.

Sasa bwana ponda huyu ndigu zangu waislamu mnatakiwa kuwa makini nae kwa sababu anafanya na kusema mambo ambayo hata uislmau wenyewe una mkataa kama vile kuwatia hamasa waislamu kuandamana eti kudai baadhi ya mambo alafu katika maandamano hayo unakuta waislamu wanapigwa na kuwagwa damu,hivi anajua thamani ya damu katika uislamu?

Uislamu unaruhusu hata kumkufuru Mungu ikiwa tu umeambiwa kama hautokufuru unakufa,uislamu unakuruhusu kukufuru kwa ajili ya kulinda hishma ya damu yako.lakini mtu kama ponda lini aliwahi kukemea mambo ya maandamano kutokana na hasara za watu kuumia na kufa?

Alafu katika mambo mbali mbali ya kijamii huyu bwana amekuwa anatoa matamko ambayo huwenda yakaashiria na kupelekea hali mbaya,huyu bwana ni hodari wa kudai usawa katika serikali kwamba waislamu nao wawe wemgi huko sijui atapata faida gani.

Juzi juzi kumetokea tokeo ya UDOM huko ambako naye katoa tamko ambalo ukiliskiliza linaitupia lawama fulani na sio ajabu baadae akaja juu tena huyu ponda kuhusu hili sakata na kuwatia hamasa waislamu.

Ponda ni mtu wa kupuuzwa,anawapotezea muda sana waislamu na kuwatia katika mlango wa chuki baina ya waislamu na serikali jambo ambalo litazidi kuwafanya waislamu kuzidi kuishi kwa dhiki kuliko mwanzo.

Ponda hana uelewa wa kujua kwamba jambo hili akilifanya madhara yake ni makubwa kuliko faida na hivyo liepukwe,ponda haelewi hilo,anachojua yeye kila jambo kuja nalo juu tuu.
KUNDECHA ALILIZUNGUMZIA SUALA LA MSIKITI PALE UDOM MBELE YA RAIS ikulu na likasikika lakini ponda naye amekuja majuzi kulisemea,anatafuta nini huyu?

Ponda ni mwanasiasa aliyejificha katika mlango wa dini na ndiyo maana huwezi kumkuta anafanya harakati za kufundisha waislamu mambo ya dini yao,yeye na serikali tu alafu matokeo yake faida chache na hasara ni kubwa miongoni mwa hasara hizo ni uislamu kuonekana dini ya fujo fujo tu.

Ponda ni muislamu ambaye hatakiwi kuitwa mwnazuoni,ni muislamu mwanasiasa tu ambaye hana tofauti na watu wengine kama akina lissu au mbowe,lakini tu yeye hulenga katika mambo ya dini.

Huyu ponda anapenda sana huko serikalini kuwe na usawa kati ya wakristo na waislamu,zanzibar ambako kuna waislamu tupu serikalini kimefanyika nini ambacho yeye ponda kasimama akakisifia kwa wingi wa waislamu hao?

Povu ruksa
 
Ngoja tuwasubiri ummah Muhammad kuja kusema chochote kuhusu hii mada mkuu, nashukuru tu umejitanabaisha nawe ni mmoja wao
Hapa tegemea maneno kama kuitwa kafiri,mnafiki,nimetumwa na serikali au kibaraka,au sijilewi au najikomba kwa wakristo,hayo yote nitatuhumiwa katika uzi huu.

Lakini mfano mzuri kule zanzibar ni waislamu tupuu ila wakatokea UAMSHO wametia chokochoko baina ya waislamu hao hao alafu huku ponda anataka usawa na siasa kama hizo.
 
Mkuu nimekuelewa sana,yani unajielewa..mara chache sana kuwa na watu kama wewe mnaojielewa,ngoja waje wenzako kina FaizaFoxy
 
Mkuu nimekuelewa sana,yani unajielewa..mara chache sana kuwa na watu kama wewe mnaojielewa,ngoja waje wenzako kina FaizaFoxy
Ndege wafananao..
Anayemtetea mtu kama ponda ni mjinga wa dini yake au mwanasiasa tu anayejificha katika mgongo wa dini.
 
Wewe nilitegemea utakuja tu hapa.

Kstika mashekhe hawajielewi uislamu wao ni ponda.kisiasa sawa ila asijitie ati anafanya kwa maslahi ya waislamu.

Kama anajielewa kisiasa hilo halina neno.
Hii mada ni character assasination haina mantiki yoyote.

Binafsi ninaona katika Masheikh viongozi wa waislamu wanaojitambua ni Sheikh Ponda!

Huyu hayumbishwi, siyo kama wale akina Sheikh Alhadi
 
Huyu jamaa kuna uzi alijitambulisha kama mkristo ila sasa kutwa kuingilia mada za waislamu sijui hana imani mpaka kuukana uislamu wake kisa sakata la udom
Wewe nilitegemea utakuja tu hapa.

Kstika mashekhe hawajielewi uislamu wao ni ponda.kisiasa sawa ila asijitie ati anafanya kwa maslahi ya waislamu.

Kama anajielewa kisiasa hilo halina neno.
 
Ana durusisha msikiti gani na kitabu gani huyo shekhe pinda kama kweli ni mwanazuoni?

Unaweza kutuambia video zake za mawaidha akifundisha uislamu mbali na kuzungumzia siasa?

Huyo ni mwanazuoni wa siasa sio mwanazuoni wa kiislamu.
Huyu ni msomi mwanazuoni,siyo lazima awe Bakwata.
BAKWATA ni jumuiya ya CCM siyo chombo cha waislam,ni jumuiya iliyoundwa na serikali ya mwalimu ili kudhibiti waislam na kupigia kampeni tu.
 
Kibaraka wa ccm wewe,huna uislam wowote una jina tuu la kiislam lakini hujitambui.
Bora ukale nao nguruwe tuu hao unaowaona wanafaa kuwa wanazuoni
Hivi unadhani kula nguruwe ndiyo dhambi kubwa sana duniani?kuna watu wazinzi,wezi,wafitini,wadhulumaji mbona kung'ang'ana na nguruwe tu hizo nyengine huzioni?

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Hata mimi alinambia kwamba yeye ni mfuasi wa yesu kristo,nashangaa hapa kumuona kila sehemu.

Si aseme tu yeye muislamu
Huyu jamaa kuna uzi alijitambulisha kama mkristo ila sasa kutwa kuingilia mada za waislamu sijui hana imani mpaka kuukana uislamu wake kisa sakata la udom
 
Mkuu hao watu ni waisilamu wa jazba jazba.
Wanachojua wao dhambi ni kula nguruwe tu.

Huku nilipo ukizini kawaida ila ukionekana unakula nguruwe maneno mengi,sasa unauliza kuzini ni ibada sasa hivi?
Hivi unadhani kula nguruwe ndiyo dhambi kubwa sana duniani?kuna watu wazinzi,wezi,wafitini,wadhulumaji mbona kung'ang'ana na nguruwe tu hizo nyengine huzioni?

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Mkuu wewe si mkristo ya waislamu hayakuhusu
Jamaa ni muislam hilo halina ubishi tatizo wakiambiwa ukweli na mwezao hujigeuza kama samaki ili kumu-attack msema ukweli ila likiwa la heri kwao hujikusanya pamoja kupongeza na kushambulia.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Jamaa ni muislam hilo halina ubishi tatizo wakiambiwa ukweli na mwezao hujigeuza kama samaki ili kumu-attack msema ukweli ila likiwa la heri kwao hujikusanya pamoja kupongeza na kushambulia.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
Mkuu si ndo hapo sasa.kwa watu kama sisi tunajua tu kwamba comment hii ya muislamu na hii ya mkristo.
 
Back
Top Bottom