TBC ni TV ya waislam na wakristo wakatoliki?

Mto Songwe

JF-Expert Member
Jul 17, 2023
6,026
12,326
Binafsi kuna jambo sielewi kuhusu hii television ya umma/taifa- TBC

Hii ni television ya kutangaza dini ya Uislam na Ukristo kupitia ukatoliki au ni television ya umma isiyo na mafungano na dini yoyote ?

Nashindwa kuelewa kwamba hawa waislam na wakatoliki wamelipa pesa ili dini zao zitangazwe kupitia television ya umma au ni tabia ya kijinga tu ya uongozi wa TBC na serikali kulifungamanisha hili taifa na hizi dini mbili Uislam na Ukristo ?

Binafsi naomba kupewa muongozo ni nini kipo nyuma kwa TBC kwa utaratibu huu wa miaka nenda rudi kwa television ya umma kutangaza dini hizi mbili Uislam na Ukristo huku ikitambuliwa kama television ya umma wote ?

Na hawa waislam na wakristo kwani wao wenyewe hawana television zao binafsi za kurusha maudhui yao huko na sio kwenye television ya umma ?
 
Huu ni utaratibu wa kijinga wanaishi kwa kodi za wananchi mpaka wasio na dini ila wanaleta upuuzi wa kututangazia mambo ya waislam na wakristo kama vile taifa zima ni la waislam na wakristo pumbavu
Ila mkuu kuna vipindi pia vya bongo fleva, kilimo n.k
Ni kama wanajaribu kubalance
 
Huu ni utaratibu wa kijinga wanaishi kwa kodi za wananchi mpaka wasio na dini ila wanaleta upuuzi wa kututangazia mambo ya waislam na wakristo kama vile taifa zima ni la waislam na wakristo pumbavu
🤣Asa si usiangalie tu... bana... ungekuwa forced kwenda church jumapili au kuswali Sala Tano sawa..if ungekuwa forced kufollow religious rules kisa katiba sawa Ila Sasa jamani TV...
 
Sijawahi kuona mahubiri ya wapentekoste CPCT kwenye hizi media, walau jana jumamosi kuna kipindi kinaitwa maranatha ni cha wasabato hurushwa TBC. Ifike muda TBC isionekane inarusha ibada za wakatoliki na waislam tu haipendezi wafanye mabadiliko ya kurusha ibada za makanisa yote
 
Dawa ni kuacha kuangalia
 
Back
Top Bottom